TBS Arusha ni wanyang'anyi, serikali iwatupie jicho la ukaribu

ngaiwoye

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
1,748
2,437
Umofia kwenu wanajamvi na poleni sana na misiba ya waziri mkuu mstaafu na mawaziri waandamizi wastaafu. Hakika kwa mola tutarejea.

Naandika bandiko hili kwa masikitiko makubwa sana, kwakuwa naona kama kuna viongozi ambao wanashindwa kumsaidia mh. Rais kwa dhati kwa kushindwa kufatilia utendaji wa taasisi za serikali.

Wiki iliyopita jirani na biashara yangu nilishuhudia watumishi wa TBS Arusha wakivamia maduka ya vipodozi MAWILI yaliyopo eneo la karibu na benki ya NMB soko kuu, Arusha mjini. (Almaaruf kwa mtumishi, na duka la jirani yake). Walichukua Mali iliyojaa kwenye gari ya kubebea mizigo(maarufu kama kirikuu) jambo ambalo lilituacha wananchi vinywa wazi, kwa kuwa bidhaa walizokamata zilikuwa na stakabadhi halali, zimelipiwa kodi na zimeingizwa kwa uhalali kabisa nchini kwetu pia zimethibitishwa na TBS kama ilivyo ada.

Watumishi hao walijitambulisha kwa majina Faustine J, na Maganga D. Walikamata bidhaa za vipodozi ambazo sisi kama wafanyabiashara hatujawahi kufahamishwa kwamba hazitakiwi kuuzwa, na zipo zimejaa kwenye maduka yote hapa Arusha na sehemu zingine nchini, na haziuzwi kwa kificho.

Kwa uchache baadhi ya bidhaa walizokamata ni bodyspray za Rasas, mafuta ya nywele ya radiant, sabuni za karambola na bidhaa nyingine kedekede.

Jambo ambalo lilitustaajabisha na kutufanya tuone kinachofanyika ni aina ya unyang'anyi ni hili: mwenye duka aliamua kumwita supplier mkubwa wa bidhaa za radiant na movit aitwae Doreen na alifika na kukiri yeye ndie msambazaji na alithibitisha bidhaa hizo zimeingia nchini kwa uhalali na zimekaguliwa na TBS na zimefata utaratibu wote ikiwemo ulipaji wa ushuru na kodi zote. Faustine na Maganga hawakuelewa na walikuwa wakali sana na bila kujali usumbufu na mitaji ya wafanyabiashara waliamua kuchukua caton zote za mzigo.

Hatukuishia hapo, tulitoa stakabadhi za bodyspray za Rasas na kumpigia wakala mkuu aliepo Dar es salaam na akathibitisha mzigo ule aliuuza na umeingia nchini kihalali na kufata utaratibu wote ikiwemo kuthibitishwa na TBS na kulipa ushuru na kodi zote. Cha kushangaza watumishi hawa wa TBS walikataa kuangalia nyaraka na kuwasikiliza hao waliouza mizigo hiyo kwa wafanyabiashara na kusema haiwahusu. Wakaendelea na jukumu la kuchukua bidhaa dukani hali ambayo ilisababisha usumbufu mkubwa sana na hasara kubwa sana.

Wafanyabiashara tumeshtuka sana na kubaki na maswali haya:

Bidhaa hizi zinaletwa bandarini kwa uwazi na kusafirishwa na magari makubwa ya mizigo ambayo hayawezi kupitia njia za panya, hao TBS walikuwa wapi mpaka bidhaa kuingia na kutufikia sisi wauzaji wa mwisho??

Wakala wakubwa walizungumza nao na kuthibitisha kwamba wao ndio wameuza mali hiyo kwetu na ndio wasambazaji na mmoja (Doreen) alifika kabisa mpaka eneo la tukio, na nyaraka zake zote lakini hawakutaka kumsikiliza, je ni halali?

Ikiwa maagent wanaoingiza bidhaa hizi wapo na wanajulikana na wapo tayari kutoa ushirikiano, kwanini hawa watumishi hawakwenda kuwafuata hawa mawakala na badala yake wakaamua kutunyang'anya bidhaa zetu ambazo tumezinunua kihalali na kutusababishia usumbufu mkubwa mbele ya wateja wetu?? Ina maana TBS wapo kwa AJILI ya kuuwa biashara zetu ama wapo kwa ajili ya kuzilinda na kutusimamia? Sisi tutalipaje marejesho?? Huu SI ndo mwanzo wa kufilisika?

Ni wazi Mh.waziri pamoja na serikali mnafahamu kwamba biashara hizi tumeweka mitaji mikubwa na tuna mikopo mikubwa, kwanini mnaacha watu kama hawa ambao hawana weledi wanakuja kuharibu biashara za watu?? Kitendo kile kilifanyika hadharani na kwa hali yoyote kitatupotezea wateja kwani wateja wetu hawatatuamini na wataamini sisi tunauza bidhaa ambazo sio salama kwa watumiaji. Ni nani wa kubebea hasara hii?

Ni rai yangu kwamba swala hili lifanyiwe uchunguzi yakinifu na wahusika hawa ambao ni Faustine pamoja na Maganga wakibainika na MAKOSA wachukuliwe HATUA kali Ili iwe mfano kwa wenzao.

Pia natoa ushauri kwa serikali kuifuatilia hii taasisi kwani wamekuwa na tabia ya kunyang'anya mali na kuzipoteza, je wakichukua bidhaa hizi hua zinapelekwa wapi? Usalama wa mali zetu na hasara zake nani wa kubeba? Nani wa kutufuta machozi sisi??
 
Mmmh, hao ni TBS kweli?? Arusha kuna tabia ya wahuni kujifanya maafisa wa serikali kisha wanawapiga wafanyabiashara mali / fedha zao. Mlojihakikishia kuwa hao ni watumishi wa TBS?
 
Mmmh, hao ni TBS kweli?? Arusha kuna tabia ya wahuni kujifanya maafisa wa serikali kisha wanawapiga wafanyabiashara mali / fedha zao. Mlojihakikishia kuwa hao ni watumishi wa TBS?
Mkuu ndio na majina yao ni J.Faustine na D. Maganga
 
Mtu hawezi kuja kwenye Biashara yangu akaleta ubabe kipumbavu, sasa watu wawili wanachukua vitu maduka mawili alafu bila maelezo ya maana nyi mnawaangalia tu.... Aisee watanzania mtaacha lini ukondoo... Mi kwenye kutetea Haki yangu alafu najua kabisa nipo sahihi hao kenge wangejuta

Nenda polisi wafungulieni kesi ya unyang'anyi, tafuta mwanasheria mzuri buruza hao watu mahakamani, kama kweli unasema bidhaa zilizochukuliwa zilikua hazina magumushi itakua fundisho kwa hao kenge maji....

Nilishakaa ndani wiki mbili kwa kumpiga mtendaji kibao na mgambo wake,japo pesa ilinitoka ila heshima mpaka Leo ipo, ashakua mshkaji tunapiga wote bia ila anajua kabisa sipendi ujinga..... Acha uoga kwenye Haki yako.

Labda kama ulikua unauza vitu vya magumashi
 
Mkuu tusingeita supplier na kama vingekiwa ni magumashi supplier asingekubali kabisa kufika. Tunajiamini na ndio sababu tulitoa stakabadhi halali na supplier anaeingiza mzigo huo Tanzania alifika na nyaraka zake
 
Sasa mliruhusu hao jamaa wachukue vitu vyenu kwa kigezo Gani? Kwanini hamjawashtaki mpaka sasa? Na je mlijiridhisha pasipo shaka hao ni watu wa tbs? Mlimtafuta bosi wao?
 
One sided story.

Mkuu mimi naelewa kuwa vipodozi vilivyopigwa marufuku ndio vina faida na vinapendwa sana ingawa vina madhara.

Kama vipodozi hivyo vimethibitishwa na nyaraka zote zipo, nashauri beba nyaraka zote muhimu, timba ofisini kwao na uombe kuongea na meneja wa kanda

Hapo ukweli utafahamika.
 
Mkuu nenda duka lolote utapata body spray za Rasas, nenda Kila mahali utapata mafuta ya nywele ya radiant
 
Kama hawajaja na polisi na seizure order msinge kubali wachukue mali yenu
Aisee Chugastan mmekuwa makondoo siku hizi 😡
 
Back
Top Bottom