Mamlaka Iringa shughulikieni ukosefu wa miundombinu ya vyoo Soko la Machinga

Bull Bucka

Member
Oct 5, 2023
34
46
Wafanyabiashara katika Soko la Machinga, lililopo kata ya Mlandege, mkoani Iringa, wanakabiliana na changamoto kubwa ya kukosa miundombinu ya vyoo. Hali hii inawalazimu kutumia eneo la nyuma ya soko, ambalo ni la makaburi, kama sehemu ya kujisaidia. Hii ni hali ya hatari kwa afya, kwani eneo hili linatumika na watu wengi na kukosa huduma muhimu kama vyoo ni jambo la kusikitisha.

Ni jambo la kushangaza kwamba mamlaka husika hazioni umuhimu wa kutatua suala hili haraka. Kabla ya kuhama na kupelekwa katika soko hili, wafanyabiashara walikuwa wakifanya biashara zao kwenye barabara za Soko la Mashine Tatu, karibu na stendi kuu ya zamani.

Kulikuwa na ulazima wa kushughulikia suala hili la miundombinu ya vyoo kabla ya kuwahamishia wafanyabiashara hao katika eneo jipya. Hali ya kutumia eneo la makaburi kama vyoo haipaswi kuendelea na inapaswa kutatuliwa haraka ili kuhakikisha usalama wa afya ya wafanyabiashara na umma kwa ujumla.

Soko.jpg

Soko 2.jpg
 
Back
Top Bottom