Wafanyabiashara wa soko la SIMU2000 wagoma asubuhi hii, Oktoba 19, 2023

SE-CHANDO

Member
Oct 18, 2023
5
2
Baada ya kutokea sintofahamu hali ni kama ilivyo hivi sasa

20231019_090045.jpg


===​

Wafanyabiashara wa Soko la Simu 2000 lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, Dar es Salaam mapema Leo, Alhamisi Oktoba 19, 2023 wameandamana sambamba na kufunga Barabara wakishinikiza Mamlaka za Serikali kuwapatia taarifa rasmi kuhusu tetesi zilizokuwepo awali kuwa wanatakiwa kuhama kwenye eneo hilo ili kupisha Karakana ya Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka (DART).

Wakizungumza kwa nyakati tofauti Wafanyabiashara hao wameeleza kuwa wamelazimika kuchukua maamuzi hayo baada ya awali kutopata majibu ya kuridhisha kutoka kwa Diwani Kata na Meneja wa Soko hilo.

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Hashim Komba aliyefike eneo hilo akiwa ameambatana na Maafisa wa Jeshi la Polisi, Viongozi wa Halmashauri na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya hiyo ameeleza masikitiko yake kwa hatua iliyochukuliwa na Wafanyabiashara hao kwakuwa wamechukua maamuzi ambayo hayastahili na yaliyoko kinyume cha sheria.

Amesema taarifa hizo hazina uhalisia wowote kwakuwa hazijatoka kwenye Vyanzo rasmi vya Serikali na kwamba kama suala hilo lingekuwepo au litakuwepo Wafanyabiashara hao wangeshirikishwa kwa kufanya Vikao rasmi na wamiliki wa Soko hilo ambao ni Halmashauri ya Manispaa Ubungo.

Katika hatua nyingine Komba ameagiza Vijana waliokuwa wameshikiliwa awali na Maafisa wa Jeshi la Polisi kutokana na maandamano hayo waachiliwe ili waendelee na shughuli zao, sambamba na kutoa onyo kwa yeyote atakayeanzisha vurugu, mgomo au maandamano bila kufuata taratibu.

Hadi Jambo TV inaondoka eneo hilo hali ilikuwa imetengamaa na Wafanyabiashara baadhi yao walikuwa wameanza kufungua Biashara zao.

Jambo TV
 
Back
Top Bottom