Mkurya mweupe
JF-Expert Member
- Aug 10, 2023
- 227
- 742
Kwanza nipende kutoa shukrani kutokana na maboresho yaliyofanywa na mwekezaji katika kuboresha soko la CCM, Katoro Geita, Changamoto kubwa iliyoibuka baada ya Mwekezaji kushika hili soko ni unyanyasi mkubwa unaofanyika kwa wafanyabiashara wadogo wadogo, ikiwemo;
1. Mkuu wa mkoa wa Geita, ndugu Martin Shigela alikuja na kuhutubia mbele ya soko akiwaambia wafanyabiashara wadogo walioko kwenye road reserves hawahusiki na mwekezaji inabidi watozwe tu hela ya ushuru ,mfano wa usafi, lakini mwekezaji alikiuka agizo la mkuu wa mkoa akidai kuwa yeye labda atafute soko lake na watu wakatozwa kodi kubwa, kulipia meza hyo, pia mkuu wa Mkoa aliomba wamama wauza mboga wanaotandika chini mfano wauza mchicha, wasitozwe Kodi kubwa ambapo mwekezaji anawatoza elfu 20,000, lakini agizo hilo la mkuu wa mkoa lilikiukwa? Nani yupo nyuma ya Mwekezaji huyu hadi kudharau amri ya mkuu wa mkoa?
2. Kuna machinga waliokuwa wamewekwa na mwekezaji mwenyewe wakimlipa kodi kwa mwaka kwa ajili ya kufanya biashara katika eneo hilo mfano wapo waliokuwa wamelipia pembezoni mwa kuta lakini baadae yeye amevunja makubaliano na kuamua kuwakata hela za miezi iliyotumika na kuwaambia watafute maeneo mengine na kuweka watu wengine kwa bei kubwa zaidi, wakati mkataba nao haujaisha , Je kisheria ipo sawa kuvunja mkataba kabla ya Kodi haijaisha au kumpandishia Kodi mteja wako katikati ya mkataba akiwa hajamaliza mwaka wake?
3. Mwekezaji alipewa ajenge soko kwa kufata ramani iliyokuwa imetolewa ,lakini cha kushangaza ramani imekiukwa ameamua kuongeza baadhi ya vyumba ambavyo vingine vinaingia kwenye road reserves ,je wasimamizi wa miradi hawaoni kinachofanyika ,nani yupo nyuma ya Mwekezaji hadi kumfanya akiuke ramani ya soko na kufata maslahi yake binafsi?
martin Shigela dorothy Gwajima ccm TAKUKURU