Subira huvuta heri wana Gunners wenzangu
Hii safari haikuwa rahisi hata kidogo, tumeambiwa maneno mengi ya kutukatisha tamaa
Ambayo kwa sehemu kubwa yalichangia baadhi ya waliokuwa mashabiki wenzetu wa Arsenal kuhamia timu nyingine za Man City, Chelsea hata wengine kudiriki kwenda Newcastle utd
Kocha wetu amejitahidi sana kurudisha morale ya timu yeye pamoja na benchi lake la ufundi, katika miaka yake 8 akiwa kama Kocha wa timu ya Arsenal, tumeona Mikel Arteta akitumia mbinu mbalimbali kuanzia kucheza mpira wa kuburudisha wa Pep Guardiola hadi kuamua kucheza haram football wa José Mourinho
Iwapo tutafanya maboresho ya kikosi chetu hasa eneo la Kiungo cha Ukabaji na ushambuliaji, tukapata kiungo mshambuliaji mwenye jicho la mwewe kama la Mesut Özil ama Cesc Fàbregas nina amini tutaenda kuwa tishio kwa miaka 4 hadi 6 ijjayo, kwani timu yetu imesheheni wachezaji wengi vijana
Hongereni kwa kila mmoja wetu humu, the waiting is over now 💪
COYGs, Let's celebrate 🥂