Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Sasa ndugu yangu Castr kwa ile michezo ya kina Lacazette, Ordegaard, Pepe na Bellerin kwenye vyumba vya kubadilishia nguo mtaachaje kulaanika?
1746711164572.jpg
 
Jamaa kaongea ukwel mtupu

Shida sio wachezaji wa Arsenal shida ni Mashabiki wanaamini mno kuwa team yao ni team bora😃😃kumbe ni version ya Tottenham iliyochangamka
Arse8 na Makolokolo ni mapacha kabisa, wote ni kamdomo wala huwa hawana hata sekunde ya kuheshimu wapinzani wataokutana nao kimchezo.

Ubinadamu ni kazi/The humanity is work.
 
Mna nini Cha kutuambia baada ya kupoteza mchezo?
verifaidi yuza wewe ni wa kukimbia jukwaa?😃
mkorea ungeingilia kati na karate uwavhape PSG maana ndugu zenu arse8 walianza kukabia hadi mikono
Castr nilikuambia ni rahisi ngamia kupenya tundu la sindano kuliko aseno kuchukua UEFA
Do you see?
Nikakuahidi Aseno akichukua UEFA mwaka huu najitoa jf 😂
HENRY14 njoo tu angalau usafishe nyota ya kupiga picha na PL yetu maana dah
Kikombe mnachoweza nyie ni Cha kahawa tu
Tuache kidogo 😂🙌🏾
 
Ukitaka kujua hawa watu kuna mahali kuna shida. subiri wiki ipite,warudi kudanganyana tena. yaani kama watoto vile.

Watakwambia mafanikio yao wamejitahid wamefika nusu fainali na kumfunga madrid, utawasikia wakikwambia EPL hawajaweza kuchukua kisa marefa wa EPL wanawaonea, ukiwauliza vipi mashindano mengine ambayo hamuonewi mbona hamjachukua?

Ukiwaambia pia Arteta ni tapeli watakukatalia.
 
Mimi ni United, shida ya Arsenal si kwamba ni timu mbaya hapana ni timu Bora sana, lakini wanachokosa Arsenal ni ile Personality na Maturity, unajua kwenye mpira kuna ile mentality Fulani ya kubeba majukumu as if una share ya umiliki kwenye timu, kama utakuwa unaangalia vizuri na unaujua mpira bila mapenzi utaona timu zote zinazochukua makombe zina hizo sifa, unaweza kuona timu hii mbona haichezi vizuri lakini inachukua makombe ni kwasababu ya burning desire iliyo kwenye mioyo ya wachezaji.

Vipaji na mifumo haitoshi, Inahitaji uwe na wachezaji wa aina hiyo ambao wao Kila nafasi ama dakika ina maana kwao, Juzi Inter Milan na Barca Kila timu ilikuwa inajua muda wowote tunaweza kufunga goli, Kila mara ni keep pushing, Sasa Arsenal wao wanafuata tu njia za kocha na kucheza vipaji vyao lakini wamesahau kuwekeza kwenye akili, pindi tu Arsenal players wakiwa na ile akili ya kibingwa watavunja gundu lao na kufika mbali sana.

Arsenal wameziacha mbali timu nyingi hasa kiuchezaji, Inahitaji uwe na timu kuifunga Arsenal. Vipaji na mbinu havitoshi , good personality ndiyo iliwafanya Madrid wachukue UEFA back to back na si kwamba Zidane alikuwa ni kocha Bora sana hapana bali wale jamaa Kina Toni kroos, Modric, Cristiano, Casemiro, Ramos, Marcelo walikuwa wanajua tunaenda kufanya Nini kiasi ambacho hata bila kocha wanacheza.
Comment bora kabisaa hii. 👏👏👏👏
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom