Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Mbona wewe umekesha usiku umeacha ndoa😁
IMG_20230115_223724.jpg
 
Katika gemu ngumu me naiona ya porto ilikuwa ngumu sana kwa arteta. Ukizingatia na upana wa kikosi alichokuwa nacho. Kama amepita jana namtabiria mema. Na nahisi ndo ilikuwa target yake kubwa kupita kweta rrobo. Kuvunja miiko kwanza. Ila urejeo wa wachezaji wake muhimu. Hakuna timu yoyote itakayomsumbua hasa ukizingatia uwepo wa wachezaji Kama timber, tomiyasu, partey, martinel, jesus, yan Ana wigo mpana wa wachezaji walirejea
 
Halafu refa alikua anamlea sana Havertz sijaamini kama amemaliza dakika zote 120 bila kula umeme wakati tayari alikua na kadi ya njano.
Refa wa jana alikuwa fair sana, kwa maana alikuwa hovyo kwa timu zote, ingawa alizidisha kupendelea Porto. Jamaa alikuwa hataki kutoa kadi hovyo kabisa. Angekuwa mtoa kadi mechi ingechezwa na wachezaji 9 kila timu.
 
Odegard sana kaiva, muda mrefu saaana nilikua sijamuona kwenye game ngumu na big games anaichukua timu mabegani anaamua vitu vitokee ile pasi ya goli na ile penalty ya kwanza kabisa vimeamua mchezo wa jana na ndo maana kuna nilikua nabishana na watu mpaka kufa kuhusu kumuweka kundi moja na KDB, ila angalau kwa sasa unaweza kumuweka Nyuma ya KDB.
 
Refa wa jana alikuwa fair sana, kwa maana alikuwa hovyo kwa timu zote, ingawa alizidisha kupendelea Porto. Jamaa alikuwa hataki kutoa kadi hovyo kabisa. Angekuwa mtoa kadi mechi ingechezwa na wachezaji 9 kila timu.
Mimi mwenyewe nimemkubali sana, sijaona refa yoyote wa Epl yuko fair kama huyo mshkaji, kuna baadhi ya faulo alikua anazipotezea tu, yule jamaa hata kwa wachezaji alikua very friendly muda wote anatabasamu.
Angekuwa ni refa wa kiingereza angetembeza kadi kama njugu.

Hongereni sana Arsenyau kwa kuingia robo fainali, Bora ukutane na simba porini anaweza kukuhurumia lakini sio ukutane na Arsenyo hii ya kono la nyani.

#Tetaball burudani kwa wote
 
Back
Top Bottom