Arsenal (The Gunners) | Special Thread


Ninyi bado underdog kwenye uefa
 
Ngoja tukusaidie kutag🔥😂
 
wapi mkorea [emoji16][emoji16][emoji16]ili jukwaa ni la comedy sana inabidi wasafi iwe inakuja kuchukua vipaji hapa kuvipeleka kwenye cheka tu.
 
Nikikumbuka wakati pinga pinga fans niliposema Porto anaweza kutuletea matatizo wakawa wanakuja na maelezo ya mambo ya system ya uchezaji huku wanabisha kuwa timu tishio UCL ni Real Madrid and Manchester City naishia kucheka tu anyway we still have 90 minutes pale Emirates za kucheza sema Arsenal ataingia na presha ya kutaka results na Porto atakuwa anacheza counter attack sijui itakuwaje?but lazima game tuiangalie COYG!

La kuongeza ni kuwa kuna fan alisema Odegaard kwake ni bora kuliko KDB nataka kumwambia kuwa game kama hizi za Champions league (big games)ndizo zinaoneshaga who is who
 
Pingapinga akina Mkorea wanakwambia tunashinda tu
Walevi wa matokeo
 
Ndio maana tunawaita FALSE HOPES F.C
Hapa unaonyesha ni jinsi gani nyinyi KONDOO ni VICHWA VYA PANZI. Msimu ulopita na SPORTING LISBON mshasahau kabisa.

Porto anaweza kuja kwenu hapo, na kufanya defensive work kama ya first hapa, na shughuli ikaishia hapo.
 
Kwa nilichoona jana

Brighton
Westham
Liva
City

Zote zikicheza kama Porto alivyocheza zinaweza kuchukua points.

Against Liva au City hua wanaacha beki wawili nyuma wakiwa wanapiga kona au set piece yoyote. Porto alikua anaacha wanne na kiungo mmoja. Hupigi counter.

Saka anakutana na beki anamkaba traditional na nyuma ya huyo beki kuna mabeki wawili huku kiungo anakuja kucommit na pressing.

Mbele haendi akitoa sidewaypasi yule kiungo kafika.

Sasa Porto aliamua kupaki basi, kumsusia mpira ili afunguke ngumu ana watu wana pace si mchezo. Jorginho kwakua anagawa mipira vizuri ilibidi aingie mapema, Trossard asitoke, Jorginho afocus na kusambaza mipira ulinzi afanye Rice.

I honestly think walichotuzidi Porto ni nidhamu ya defense, roho mbaya, kumdanganya refa and then basi. That's it
 
La kuongeza ni kuwa kuna fan alisema Odegaard kwake ni bora kuliko KDB nataka kumwambia kuwa game kama hizi za Champions league (big games)ndizo zinaoneshaga who is who
KDB yupo kwenye level nyingine, kuna vitu inabidi uweke ushabiki pembeni ili uone uhalisia wa vitu. Siyo Bruno wala Ø anafikia uwezo alionao KDB.
 
Vijana wangu mlioanza kushabikia arsenal miaka ya 2010s msiache kuwa mnasoma hii post. Itakuwa inawasaidia from time to time.

Aina yetu ya mpira kamwe hatuwezi kubeba makombe makubwa. Kaeni chini msikilize tunachowaambia maana tumeshabikia arsenal kwa karibu miaka 30 sasa.
 
Unaweza kubadili mfumo lakini sio msingi wa mawazo yako ambao ni : COMPACT : Hakikisha wachezaji wanakuwa karibu karibu sana iwe kwenye kushambulia na kuzuia hii inasaidia timu kuwa imara uwanjani , FC Porto wameonesha hili kwa ustadi wa hali ya juu sana
1: Compact 4-4-2 hakuna space kabisa katikati ya mistari yao yote mitatu na kuwalazimisha Arsenal kwenda pembeni kutumia wingers
2: Uzuri kwa Porto fullbacks wao wazuri kwenye 1v1 na pia hata Arsenal wakifanikiwa kupiga krosi Pepe , Otavio na Golikipa wao Costa wanacheza mipira yote wao tu .... goli linatokea wapi ???
3: Viungo wawili wa kati Nico na Varella walikuwa muda wote wame switch ON kuzuia namba 8 wawili wa Arsenal Kai na Odegaard ( Track runners ) na hata wakipata mali wanapasia vizuri sana , ni msingi mzuri wa kufanya counter attacks
Arsenal walifanya kila kitu kwa usahihi , rotations za wachezaji uwanjani , Trossard akishuka , Kai anasogea juu hivyo hivyo wanabadilishana , Odegaard alishuka kuwa karibu na Rice , Ben White anasogea juu ili tu kujaribu kuharibu muundo wa ulinzi wa Porto , kufungua spaces ili wapate kupita ndani zaidi badala ya pembeni . Lakini pongezi unawapa Porto kwa ustadi wao . Porto wamefanya Arsenal wacheze vile leo hii . Full Stop
NOTE
1: Kwenye timu hutakiwi kuwa na abiria kama unataka matokeo mazuri tena kwenye mechi za daraja la juu Ulaya , Porto wamefanya hivyo
2: Odegaard akiwa na mali mguuni , kafundi sana kale kajamaa
3: Saka , Martinelli ,Trossard na Kai kazi yao ilikuwa ngumu sana leo
4: Diogo Costa : Mipira ya hewani alikuwa anaicheza vizuri sana na akiwa na mali mguuni kushoto au kulia bila wasiwasi anapiga mipira vizuri
5: Galeno kwanza alivyogongesha nguzo halafu baadae alivyomtungua Raya ... umaliziaji mzuri sana .!
6: Arsenal wamemaliza mechi bila shot on target hata moja
FT: FC Porto 1-0 Arsenal
#ambangille
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…