Arsenal anzeni kwa kumtimua Arteta na kuleta kocha. Yule Edu naye pamoja na wamiliki wa timu wanazingua tu.
Arsenal ni wachezaji 4 tu wanastahili kuwa starters kama mnataka kushindania makombe: Odegaard, Partey, Saka & Trossard wengine wote siyo wachezaji wa kutegemea ukianza na Jesus, wale mabeki wenu wote ni wachezaji wa kuanzia bench pamoja na kipa wao.
Niliwahi kusema kinachowagharimu Arsenal ni wachezaji wa mafungu. Mchezaji kama Caicedo mngempata angeimarisha sana eneo la kiungo. Mlipata nafasi ya kumsajili Martinez mkashindwa na United kufika dau.
Kwenye project yenu mnatakiwa mjue kuwa hiki kikosi mlichonacho sasa ni wachezaji 4 tu wanastahili kuanza ila kama Arteta anahisi hapa ndiyo anamalizia basi bado sana.