Updates- Usajili Arsenal
Andrea Berta ameingia soko la Ujerumani na sasa hivi Arsenal wafanya mazungumzo na Bayern Leverkusen kumsajili beki wa Uingereza Jarell Quansah.
Hiyo ni baada ya kukumbana na ugumu wa Aston Villa ambao wataka pauni milioni 60 kwa Ezra Konsa.
Kabla ya kwenda Bayern Leverkusen Quansah alikuwa ni beki wa Liverpool na alisajiliwa kwa kiasi cha pauni milioni 35.
Mwaka huu Quansah alichezea Uingereza kwenye fainali za kombe la Dunia na beki huyo mwenye umri wa miaka 23 amechezea Bayern mara 44.
Arsenal ina tatizo kwenye safu ya ulinzi ambapo mabeki William Saliba na Jurrien Timber bado ni majeruhi. Pia beki Ben White hana uhakika kwani amekuwa akisumbuliwa na tatizo la majeruhi sugu.
Beki Cristhian Masquera si beki "Verstile" ambae aweza kucheza nafasi mbalimbali na ndiye aliesababisha penalty kwa PSG kwenye champions League kwa kucheza nafasi iso yake.
Wachambuzi wa Arsenal (team analysts) wamemtambua Quansah kuwa aweza kucheza nafasi zote ama pembeni au katikati hivyo "he fits the bill".
Quansah kwa asili ni beki wa kati yaani mkoba lakini alipokuwa Liverpool ambao walikuwa wakitumia mfumo wa 4-3-3, alichezea upande wa kulia.
Lakini pale Bayern amekuwa mara nyingi akichezea upande wa kulia.
Beki wa Beyern Leverkusen na timu ya taifa ya Uingereza Jarell Quansah. Picha na PA.