𝐅𝐎𝐎𝐓𝐁𝐀𝐋𝐋 𝐌𝐀𝐃𝐄 𝐈𝐍 𝐀𝐑𝐒𝐄𝐍𝐀𝐋. [emoji2][emoji3578]
[emoji3578]Hawa Kenge tumewapiga 4 na Mpira mwingi wakagawane na vibaraka wao shubaamitt
[emoji3578] Michezo sawa and FIVE POINTS CLEAR.Umenisikia au niirudie?
[emoji3578]Kama utasema team yako inacheza mpira mzuri,nitakuuliza kama Arsenal? Watu wanapasiana kutoka nyuma haijalishi Kuna Presha kiasi gani.Kila mchezaji yupo kwenye movement muda wote kuhakikisha Kuna options ya pasi haijalishi ni Eneo gani la uwanja.I ,You,We they call it Football organism
[emoji3578]Arsenal ndo team ya kwanza msimu huu kuwa na wachezaji 2 wenye Goli 10+ , Bukayo Saka na Gabriel Martinelli
[emoji3578]Kwenye magoli 10 ya Bukayo Saka, magoli 6 Yalikuwa niya kuipa Arsenal Uongozi kwenye Mechi.Na magoli 4 niya Kusawazisha.Ni Harry Kane peke yake ndo amefunga Magoli ya maamuzi zaidi ya Saka (11)
[emoji3578]Let's talk kidogo kuhusu lile bao lake.Ile Movement ya Zinchenko ndo exactly alitakiwa kufanya.Kupunguza watu Peke yake ili kuifungua Ile Midfield ya Everton.Then Bukayo Saka anapokea na Mguu wa kushoto,on the turn na ule Mguu wake wa kuvukia Barabara.Baaaaang.
[emoji3578] Infact Bukayo Saka amehusika kwenye goli 19 katika michezo 25 msimu huu.Ni ulimwengu wa Bukayo Saka tuishi humo.
[emoji3578] Everton walikuja na Plan kama ya mechi ya kwanza.Arsenal wacheze ,sisi tuharibu.Waliziba Space na 4-5-1 kama kawaida,Lakini Arteta alikuwa na Plan nyingine.Kivipi?
[emoji3578] Leandro Trossard amechukua tena nafasi ya Eddie ENKETIAH kikosini.Movement yake Kushuka kwenye Midfield,maana yake ilikuja ku Overload Midfield ya Everton.Ikawa ni Zinchenko, Jorginho/ Partey, Xhaka, Trossard vs Onana,Gana GUEYE na DACOURE.
[emoji3578] Leandro Trossard pia Kuna Wakati alikuwa anabadilishana nafasi na Gabriel Martinelli, pembeni na katikati.Hii ilivuruga kabisa Muundo wa kuzuia wa Everton.Nafikiri Gabi Martinelli akicheza ndani kidogo na kuingia kwenye box anakuwa hatari zaidi kuliko kucheza kwenye mstari wa pembeni anakabika kwake urahisi.Na amefunga goli 2 Leo kufikisha goli 11 na assist 3
[emoji3578] Nafikiri hii Plan ya LEANDRO TROSSARD Kwa team ndogo zinazopaki bus.Na Eddie ENKETIAH kwenye Mechi zile kubwa Kubwa itakuwa saafi tu
Note; Nia Yetu ni kukaa Kileleni Mpaka mwezi wa 5 halafu ubingwa mtaamua wenyewe wakumpa Kenge nyiee [emoji1787]