Arsenal (The Gunners) | Special Thread

#coyg#
_20190120_150406.JPG
_20190120_150434.JPG
_20190120_150502.JPG
_20190120_150533.JPG
_20190120_150559.JPG
_20190120_150635.JPG
_20190120_150702.JPG
_20190120_150726.JPG


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umuofia kwenu watu wa Mungu.
Kwa mujibu wa gazeti la Mirror la nchini Uingereza naona uongozi wa arsenal unamtaka Marc Overmas kuja kuchukua nafasi ya Sven Mislintat kama skauti mkuu, hii inachagizwa na kutokuelewana kwa Sven Mislintat na kocha mkuu Unai Emery.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NGOJA NIKWAMBIE KITU KUHUSU MTU HUYU.

Anafahimika kwa jina la Sven Mislintat. Kazi yake ni kuzunguka maeneo mbalimbali duniani kutafuta wachezaji wenye vipaji halisi vya vya kucheza soka. Kazi hii inafahamika kama Skauti. Sven Mislintat kwa sasa anafanya kazi kama skauti mkuu wa Arsenal. Mwaka mmoja umepita tangu aanze kufanya kazi hii akiwa Arsenal.

Mwaka 2009 alimbidi asafiri mara sita kwenda nchini Japan, akiwa kama skauti mkuu wa Borussia Dortmund. Safari za kwenda Japan zilikua ni kwa ajili ya kumfatilia kijana mmoja wa miaka 20. Shinji Kagawa. Alimuona mara ya kwanza, akamuona mara ya pili, tatu, nne, tano, sita bado hakujiridhisha na kile alichokua anakiona.

Akatafuta video zaidi ya kumi za kijana huyu. Akiwa na jopo la maskauti wenzake walijiridhisha na uwezo wake. Baadae akapeleka ripoti yake kwamba Shinji Kagawa asajiliwe. Majira ya kiangazi mwaka 2010, Borussia Dortmund ikalipa Euro laki tatu na nusu kumsajili.

Miaka miwili baadae aliuzwa kwenda Manchester United kwa gharama ya Euro milioni 15. Faida ya zaidi ya Euro milioni 14. Huku nyuma Kagawa aliondoka akiwa ameisaidia Borussia Dortmund kushinda mataji mawili ya Bundesliga. Naam. Hii ilikua ni kazi yake Sven Mislintat.

Mbali na Kagawa, Sven Mislintat alihusika kuwaleta wachezaji wengi kwenye kikosi cha Borussia Dortmund. Robert Lewandowski, Mario Gotze, Matts Hummels, Marco Reus, Pierre-Emerick Aubameyang, Jakub Blaszczykowski, Ilkay Gundogan, Raphael Guerreiro, Ousmane Dembele, Neven Subotic, Sven Bender na Henrikh Mkhitaryan ni baadhi ya wachezaji hao.

May 2016, Sven Mislintat alikamilisha dili la kumleta Osmane Dembele kutoka nchini Ufaransa kwenye klabu ya Rennes. Osmane akajiunga na Borussia Dortmund. Mwaka mmoja baadae, aliuzwa kwenda Barcelona kwa gharama ya Euro milioni 105 ambazo zingeweza kuongezeka hadi Euro milioni 145.

Hii inabaki kuwa biashara nzuri zaidi aliyowahi kuifanya. Ndani ya mwaka mmoja tu, Borussia Dortmund walipata faida ya zaidi ya Euro milioni 100. Ni pesa nyingi sana ambazo zilitokana na kazi kubwa aliyoifanya Sven Mislintat kwa kumleta Osmane nchini Ujerumani.

Ingawaje kwa sasa hafanyi kazi hiyo pale Borussia Dortmund, klabu inanufaika na wachezaji aliowahi kuwaleta. Wiki iliyopita Christian Pulisic alisaini mkataba na kuichezea Chelsea msimu ujao akitokea hapo. Mkataba uligharimu Euro milioni 64.

Pulisic kama ilivyo kwa wachezaji wengi wa Borussia Dortmund ni kijana aliyeletwa na Sven Mislintat. Mahmoud Dahoud, Julian Weigl, Manual Akanji, Dan-Axel Zagadou, Maximilian Phillip, Jacob Bruun Larsen, Alexander Isak na Sergio Gomez ni baadhi ya wachezaji vijana ambao ni ‘potential’ nzuri kwa Borussia Dortmund hivi sasa.

Kuna bwana’mdogo anaitwa Jordan Sancho pia. Ni muda tu unaosubiriwa ili aweze kuondoka Dortmund. Amekua na msimu mzuri hadi sasa. Huyu nae ni zao la Sven Mislintat alimleta kutoka Manchester City. Kama ataondoka, basi Dortmund itapata fedha nyingi pia, kama ilivyokua kwa Christian Pulisic.

Huyu jamaa husafiri nchini nyingi duniani. Husafiri hadi nchi za Afrika pia. Alishawahi kusafiri hadi Afrika Kusini kumuangalia kijana Tashreeq Matthews aliyekua anacheza klabu ya vijana ya Ajax Cape Town. Hivi sasa Tashreeq ni mchezaji wa Borussia Dortmund.

Nchini Ujerumani alifahamika kama ‘diamond eyes’. Macho ya almasi. Alipewa jina hili kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuvitambua vipaji vya vijana wadogo.

Klabu nyingi zilimuhitaji. Bayern Munich ilimuhitaji sana. November 2017 alijiunga na klabu ya Arsenal akiziba nafasi iliyoachwa na Steven Rowley ambaye alikua skauti mkuu wa Arsenal tangu mwaka 1996.

Baada ya Steven Rowley kuondoka, Arsenal ihitataji mtu sahihi atakaye ‘fit’ vizuri kwenye nafasi aliyoiacha. Kumbuka Rowley alikua ‘master’ kwenye kazi. Arsenal ilisifika kuwa timu inayozalisha vijana wengi wenye vipaji halisi vya soka. Kazi kubwa ilifanywa na Steven Rowley. Alipoondoka akaja, Sven Mislintant ambaye ni ‘master’ pia kwenye kazi hii.

Lucas Torreira na Matteo Guendouzi ni wachezaji walioletwa Arsenal na huyu jamaa. Pierre-Emerick Aubameyang, Henrik Mikhtaryan, Konstantinos Mavropanos, Sokratis Papastathopoulos na Bernd Leno ni baadhi ya sajili zilizofanyika baada ya ushauri kutoka kwake.

Anatarajiwa kufanya mambo makubwa akiwa Arsenal pia kama ilivyokua kwa Steven Rowley. Alipokua anafanya mahojiano hivi karibuni alisema atafurahi kama akifanikiwa kumpata mchezaji mwenye akili ya Andres Iniesta.

Huyu ndiye Sven Mislintant. Jamaa iliyebeba mafanikio ya Borussia Dortmund kwa kipindi chote alichofanya kazi. Wachezaji aliowaleta kwa kiasi kikubwa waliisaidia Borussia Dortmund kushinda ubingwa wa ligi kuu nchini Ujerumani, mara mbili mfululizo mwaka 2011 na 2012. Mwaka 2013 Borussia Dortmund iliingia fainali ya UEFA Champions League pia. Sasa anafanya kazi kama skauti mkuu wa Arsenal
View attachment 991708

Sent using Jamii Forums mobile app
Finally ameamua kusepa baada ya kugombana na Emery

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom