Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

daah jamaa walituadhibu na ilikuwa ni poor perfomance from the Gunners.
Monaco pia walikuwa vizuri katika deffence na kama kawaida Arsenal wanapocheza na timu yoyote kubwa wakitangulizwa wanapanda kushambulia na kusahaau nyuma na hapo ndipo unawapiga magoli ya counter attack.
Yote kwa yote hongera sana kwa Monaco.
 
  • Thanks
Reactions: Nzi
Mwenzako kasema QF sasa hiyo ilikua QF au Group Stages??

Haters mmefurahi mpaka hamfikirii vizuri, pamoja na mdau kusema QF na sio group stage, ila scenario zinafanana, ni mechi ya away kwa Arsenal ambayo watatakiwa washinde si chini ya gepu ya goli 3 kuweza kuwa na chance ya kupita au kupita.
 
Monaco wana miss five first team players na bado wamewa outplay gunners home!!

sasa sipati picha watakaporudiana wakiwa kamili na wakwa nyumbani kwao. usidhani kwamba moto huu ambao watoto wameanza nao emirates utazimika watakaporudi kwao. thubutu! tena nyumbani kwao ndipo watatafuta sifa kabisa. acha kabisa ndugu yangu.
 
Mpira sio mchezo wa kubahatisha

Soka ni mpira wa bahati mida fulani.
Kama Manu, hawachezi vizuri lakini kwenye msimamo wapo pazuri kabisa. Walipocheza Manu na Southampton pale St. Mary's, Manu walitawaliwa balaa, walipata 2 shots on target na mechi ikaisha 2-1 kwa Manu.
 
daah jamaa walituadhibu na ilikuwa ni poor perfomance from the Gunners.
Monaco pia walikuwa vizuri katika deffence na kama kawaida Arsenal wanapocheza na timu yoyote kubwa wakitangulizwa wanapanda kushambulia na kusahaau nyuma na hapo ndipo unawapiga magoli ya counter attack.
Yote kwa yote hongera sana kwa Monaco.

Huwezi amini, ila defense ya Monaco ilikuwa na makinda wawili wasio na uzoefu kabisaaaaa, ila walicheza vizuri na pia hawakuwa tested hata kidogo!
 
Kuna mahali Wenger ameshindwa, Kuna sehemu tactics za Wenger zimefeli. Ni fedheha sana...

wenga is always using same tactics and expecting different results....malizia kusoma kwenye signature yangu hapo chini.
 
sasa sipati picha watakaporudiana wakiwa kamili na wakwa nyumbani kwao. usidhani kwamba moto huu ambao watoto wameanza nao emirates utazimika watakaporudi kwao. thubutu! tena nyumbani kwao ndipo watatafuta sifa kabisa. acha kabisa ndugu yangu.

Let's face it, AS Monaco sio giant katka european football, jana wameshinda na wao wamekiri, hadi prince wao walikuwa pia uwanjani, wamekiri kuwa walikuja kuitafuta droo ila wamevuka mipango, sasa issue kwao inakuja kisaikolojia sasa hivi wao ni favorites kusonga, na watajiona wamemaliza kazi, hapo ndo ugumu wa mechi ya pili unapokuja kwao. Ni kama Ndanda FC wameifunga Barca round ya kwanza, lazima wataenda likizo kusheherekea na kujisahau kidogo round ya pili.
Hii gemu bado ipo mbichi, tunaenda kwao na kipindi cha kwanza tutatoka 2-0 tunaongoza, na ngoma itaisha 4-1, HII SIO NDOTO, ndo habari yenyewe.
 
Hivi kocha aliyekaa miaka yote hiyo, hajaweka tactics zake sawa?!?

taktikis na tageti zake bado ziko sawa...lazima ataingia TOP 4 ili atashiriki tena msimu ujao. hizi ndizo TAGETI za aseno kila mwaka. wala hawajakosea, bado wapo kwenye njia sahihi waliyojipangia.
 
  • Thanks
Reactions: Nzi
Kwa kweli babu sub zake ni utata! Ila ye ndo anawajua wachezaji wake vizuri, tumuachie hilo.

wachezaji wenyewe wananunuliwa sh 5, kama mafungu ya nyanya, unategemea apate wapi wachezaji wa maana wa kusabu?
 
  • Thanks
Reactions: Nzi
2-1 mngejipa tamaa, 3-1 ni kibarua kizito, almost impossible.
3 Away goals for Monaco, tayari wameshinda bahati nasibu.

aseno wajihesabu wametoka. unadhani watoto hawawezi kupata goli 1 nyumbani?
 
Ahsante sana Mkuu inawezekana kabisa lakini kazi ngumu hasa ukitilia maanani hawa jamaa wamepata magoli matatu ya ugenini. Tunaweza kuwafunga goli tatu lakini wameshagundua ngome yetu ni uchochoro tu unakatiza tu je tukifunga hizo goli tatu tutaweza kuwazuia wasipate hata goli moja!? Maji marefu Mkuu ila inawezekana kuishangaza dunia ya wapenda soka.

mkuu BAK watoto tayari wanaujua udhaifu wa aseno. hawawezi kukubali kufungwa nyumbani kwao, ila endelea kujipa matumaini feki lakini siku wakirudiana watoto hawatakubali kufungwa nyumbani kwao.
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
Kwa Arsenal hii wakienda Monaco hata sare hawapati

Hawa wameisha tolewa wajiandae tu na Europa League yao maana kikosi chao hiki hawawezi qualify CL mwakani

Sasa funga kazi ya kituko ni Liverpool msimu huu wa UCL, nilishangaa walipocheza na Real Madrid pale bernabeu, Liver walikuwa wanahitaji matokeo, walichofanya ni kupumzisha key players kwa ajili ya mechi iliyofuata ambayo ilikuwa ni Chelsea ili waqualify UCL. Matokeo ni kwamba mechi zote walichezea.
Yaani wanaingia UCL, alafu wakishaingia wanapumzisha wachezaji muhimu ili wawachezeshe ktk mechi "muhimu" za ku-qualify UCL, logic iko wapi?
Kwa lugha nyingine, Liver wanaona raha kushiriki UCL, sio kushindana, hawapaswi kuwacheka Arsenal kwa sasa!
TAFADHARINI ndugu zangu wa Liver, nakuombeni msiwe predictable hapa, msianze kutoa historia ya miaka ya 80s.
 
Mpira haupimwi hivyo!
Ebu cheki, Swansea inaifunga Manu, Liver inafungwa na Manu, na Liver inaifunga Swansea!!
Kwa tafsiri yako, Liver hapa haikutakiwa kufungwa na Manu.
Mpira unadunda, Arsenal tumewahi pigwa 3-0 Highbury na Internazionale ktk UCL kama kumbukumbu zangu zipo sahihi zaidi, tukaenda Italy tukawakung'uta 5-1 na kusonga mbele, wala sio mbali saana, kizazi cha Henri, na Henri alipiga hat trick, nachojaribu kusema ni kwamba mpira unadunda na matokeo hayo yanawezekana!

yanawezekana but kwa huu mpira waliocheza hawa watoto ugenini, there's a very slim chance kuwafunga nyumbani kwao...watacheza kwa sifa hata ikibidi wafie kiwanjani lkn hawatakubali kufungwa kibwege at home ground.
 
Sasa funga kazi ya kituko ni Liverpool msimu huu wa UCL, nilishangaa walipocheza na Real Madrid pale bernabeu, Liver walikuwa wanahitaji matokeo, walichofanya ni kupumzisha key players kwa ajili ya mechi iliyofuata ambayo ilikuwa ni Chelsea ili waqualify UCL. Matokeo ni kwamba mechi zote walichezea.
Yaani wanaingia UCL, alafu wakishaingia wanapumzisha wachezaji muhimu ili wawachezeshe ktk mechi "muhimu" za ku-qualify UCL, logic iko wapi?
Kwa lugha nyingine, Liver wanaona raha kushiriki UCL, sio kushindana, hawapaswi kuwacheka Arsenal kwa sasa!
TAFADHARINI ndugu zangu wa Liver, nakuombeni msiwe predictable hapa, msianze kutoa historia ya miaka ya 80s.

Kama 3-1 na Monaco basi Weupe wa Madrid si ingekua 6 jamani au?
 
.......there's a way! Keep the faith bro.
Kama wao wameweza, sie kitatushinda nini?.....

na nyie leo mmeshindwa nini kuchomoa? leo watoto hawakuwa na wachezaji muhimu kiwanjani lakini wamekuvurugeni, je mkirudiana wakiwa kamili mtawafunga? mna ubavu wa kushinda 4-1 ufaransa? nimesema 4-1 kwa sababu msitarajie kwamba watoto watashindwa kupata goli nyumbani kwao.
 
Back
Top Bottom