Sikubahatika kuangalia live gemu la leo ila nitaangalia highlights, nilikuwa kijisafari kidogo, ila nimefarijika kuona tumeshinda na huku akina Almunia,Arshavin,Denilson, Traore na hata Diaby/Nasri wakipata mapumziko, ushindi huu ni mzuri katika kuendeleza momentum, katika mechi 6 tumeshinda 5 na kutoka sare 1, sio mbaya kwa mwezi wa desemba na ukizingatia na majeruhi kwa big guns wetu. Kinachofuata ni ushindi j/tano tunaanza kuwatia tumbo joto KGBs na Manure.
Bosi amesisitiza kwa mara nyengine kwamba atanunua m/wachezaji 1 ama 2. Ningependa kumuona Chamakh lakini inaonekana huyu atakuja Summer kwa ajili ya season ijayo. Chamakh anadai Arsenal wanamtia pressure ajiunge nao January lakini hilo bosi ameshakanusha na namuamini Wenger kwa hili kwa sababu Chamakh yuko cup-tied in CL.
Naona tutanununua mchezaji atakayefiti mojakwamoja premier league, tutegemee suprise pengine Babel kama bei itakuwa poa, around 6-7millions. Wenger alimzimia Babel kitambo (2007 season) lakini kimbelembele cha Rafa aliposikia bwamdogo anakuja Arsenal aliwazidisha kidau Ajax matokeo ameuwa kipaji chake bure. Dzeko vilevile yupo kwenye rada ila bei inaweza ikawa kizingiti.
On Dzeko. I like the player, but they fly too high now, price-wise. he said
Kuna rumous ameshaweka target kwa Suarez wa Ajax. Itakavyokuwa tutegemee biashara ya kimyakimya kutokana na huko nyuma kila Wenger akipointi mchezaji watajitokeza akina Mannure,Madrid,Chelski kwa vile wanajua AW ana jicho la 3 wanapaisha dau.
Nakumbuka mwaka jana waliposikia anamuwinda Arshavin wakaanza kutaka kuchafua kama kawaida yao na Wenger alikanusha kuwa hamuhitaji Arshavin, alisema kwenye Arsenal.com:
I loves Arshavin but no, we wont buy him"
Kufumba na kufumbua hii AK-47 ilionekana mitaa ya Emirates
😀