April Fools

Status
Not open for further replies.
Breaking news France24 kwamba Baba Mtakatifu ameamua kujiuzulu madai kuwa uongozi wake,akiwa kardinali na baada ya kuwa Papa haukufanyia kazi tuhuma za sexual abuse zinazowakabili watumishi kadhaa wa Kanisa Katoliki.Tamko rasmi litafuata.
 
SIKU mbili baada ya aliyekuwa Mbunge wa Kishapu, Fred Mpendazoe kujiondoa CCM na kujiunga CCJ, chama hicho kipya kimenasa viongozi wengine watatu wa kisiasa nchini na wanatarajia kujiunga rasmi leo.

Viongozi hao ambao ni wenyeviti watatu wa vyama vya upinzani, walithibitisha hilo jana. Nao ni James Mbatia wa NCCR-Mageuzi, Augustine Mrema wa TLP na James Mapalala wa Chausta.

Akizungumza na gazeti hili jana, Mrema alisema sababu za kuhama vyama vyao ni kutokana na kukosekana kwa ushirikiano imara wa kuiondoa CCM madarakani na kuwapo mitafaruku ya hapa na pale katika vyama hivyo.

Alisema maandalizi ya kurudisha kadi za vyama vyao na kuvikabidhi kwa Mwenyekiti wa Muda wa CCJ, Richard Kiyabo, yamekamilika, ikiwa ni pamoja na jukwaa kupambwa na rangi ya njano ya chama hicho.

Alisema kikundi cha futuhi cha Za Komedi nacho kimealikwa katika hafla hiyo inayotarajia kuanza saa nne asubuhi katika viwanja hivyo.

Hili linatazamiwa kuwa pigo kubwa kwa vyama hivyo vya siasa, kwani kuondokewa na wenyeviti watatu kutaviyumbisha na huenda vingine vikatoweka, endapo wanachama wataamua kuwafuata viongozi hao.

Mbatia alipotakiwa kuzungumzia kama haoni kuwa atapoteza kitu kwa kuacha uenyekiti, alisema cheo si tija, bali nia ni kujenga demokrasia ya kweli nchini.

Aliongeza kuwa wamebaini kwamba kuwa na utitiri wa vyama hakuna tija na hivyo wanakumbuka maneno ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere wa kuwa na vyama vichache vya upinzani lakini vyenye nguvu.

Kiyabo alipoulizwa juu ya hatua hii ya kupokea vigogo hao wa kisiasa kujiunga na chama chake, alitabasamu na kushindwa kuzungumza zaidi ya kumwambia mwandishi wa habari hizi: "Nina furaha sana lakini kwa kuwa kesho (leo) ni Aprili mosi, tuonane Mnazi Mmoja baada ya kazi hiyo, tuzungumze zaidi, ingawa hutaniamini."

Mpendazoe juzi alitangaza kuihama CCM na kujiunga CCJ kwa maelezo kuwa chama hicho kikongwe kimeshindwa kupambana na ufisadi na kwamba CCJ ndicho chama mbadala. Habari zaidi zilisema viongozi wengi waandamizi wa vyama vya upinzani na tawala wako kwenye foleni ya kutangaza kujiunga na chama hicho na sasa wanaangalia upepo wa kisiasa unavyovuma.

Chanzo: The Guardian

JAMANIEEE! lEO NI APRIL MOSI, INANIPA TAABU KUAMINI KILA KINACHOANDIKWA LEO, KWANI KUNA WATU WATAKAOITUMIA SIKU YA LEO KWA MIZAHA.
 
Breaking news France24 kwamba Baba Mtakatifu ameamua kujiuzulu madai kuwa uongozi wake,akiwa kardinali na baada ya kuwa Papa haukufanyia kazi tuhuma za sexual abuse zinazowakabili watumishi kadhaa wa Kanisa Katoliki.Tamko rasmi litafuata.

Mwe!
Tunasubiri tamko:p!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom