April Fools

Status
Not open for further replies.
Kwani ni kosa ndugu yangu, uoni hata huyo aliyelitumia hajui maana yake?

Siyo kosa lako kwa kweli rafiki yangu, maana kila kitu ni kujifunza. Naona dada Preta ametoa maana yake na mimi nikaongezea kidogo nafikiri sasa umeelewa maana yake vizuri.
 
Poa, ila Pape alikuwa anaingilia hapa na kutokea pale... Naona katumia neno hata yeye alikuwa alijui maana yake.
 
SIKU mbili baada ya aliyekuwa Mbunge wa Kishapu, Fred Mpendazoe kujiondoa CCM na kujiunga CCJ, chama hicho kipya kimenasa viongozi wengine watatu wa kisiasa nchini na wanatarajia kujiunga rasmi leo.

Viongozi hao ambao ni wenyeviti watatu wa vyama vya upinzani, walithibitisha hilo jana. Nao ni James Mbatia wa NCCR-Mageuzi, Augustine Mrema wa TLP na James Mapalala wa Chausta.

Akizungumza na gazeti hili jana, Mrema alisema sababu za kuhama vyama vyao ni kutokana na kukosekana kwa ushirikiano imara wa kuiondoa CCM madarakani na kuwapo mitafaruku ya hapa na pale katika vyama hivyo.

Alisema maandalizi ya kurudisha kadi za vyama vyao na kuvikabidhi kwa Mwenyekiti wa Muda wa CCJ, Richard Kiyabo, yamekamilika, ikiwa ni pamoja na jukwaa kupambwa na rangi ya njano ya chama hicho.

Alisema kikundi cha futuhi cha Za Komedi nacho kimealikwa katika hafla hiyo inayotarajia kuanza saa nne asubuhi katika viwanja hivyo.

Hili linatazamiwa kuwa pigo kubwa kwa vyama hivyo vya siasa, kwani kuondokewa na wenyeviti watatu kutaviyumbisha na huenda vingine vikatoweka, endapo wanachama wataamua kuwafuata viongozi hao.

Mbatia alipotakiwa kuzungumzia kama haoni kuwa atapoteza kitu kwa kuacha uenyekiti, alisema cheo si tija, bali nia ni kujenga demokrasia ya kweli nchini.

Aliongeza kuwa wamebaini kwamba kuwa na utitiri wa vyama hakuna tija na hivyo wanakumbuka maneno ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere wa kuwa na vyama vichache vya upinzani lakini vyenye nguvu.

Kiyabo alipoulizwa juu ya hatua hii ya kupokea vigogo hao wa kisiasa kujiunga na chama chake, alitabasamu na kushindwa kuzungumza zaidi ya kumwambia mwandishi wa habari hizi: "Nina furaha sana lakini kwa kuwa kesho (leo) ni Aprili mosi, tuonane Mnazi Mmoja baada ya kazi hiyo, tuzungumze zaidi, ingawa hutaniamini."

Mpendazoe juzi alitangaza kuihama CCM na kujiunga CCJ kwa maelezo kuwa chama hicho kikongwe kimeshindwa kupambana na ufisadi na kwamba CCJ ndicho chama mbadala. Habari zaidi zilisema viongozi wengi waandamizi wa vyama vya upinzani na tawala wako kwenye foleni ya kutangaza kujiunga na chama hicho na sasa wanaangalia upepo wa kisiasa unavyovuma.

Chanzo: The Guardian
 
Duh ngoja iendelee kuwa tetesi mpaka siku ipite.
Mbatia na Mrema wakihami wote watataka kuwa wenye viti.
 
Ha ha haa......... nimecheka sana eti Mbatia na Mrema wote watang'ang'ania uenyekiti
 
Mbona imeanza na kasi hiyo mm hapa nimetumiwa sms naaambiwa kuwa Jk naye atarejesha kadi jumatatu...!
 
How come these are rumours....?Yani mna mquote mtu mwenyewe kwamba kazungumza halafu mnesema ni tetesi?
Luteni said:
Akizungumza na gazeti hili jana, Mrema alisema sababu za kuhama vyama vyao ni kutokana na kukosekana kwa ushirikiano imara wa kuiondoa CCM madarakani na kuwapo mitafaruku ya hapa na pale katika vyama hivyo.

Ama ni kwasababu ya maneno haya ya Kyabo?

Luteni said:
Kiyabo alipoulizwa juu ya hatua hii ya kupokea vigogo hao wa kisiasa kujiunga na chama chake, alitabasamu na kushindwa kuzungumza zaidi ya kumwambia mwandishi wa habari hizi: "Nina furaha sana lakini kwa kuwa kesho (leo) ni Aprili mosi,
 
Mbatia na Mrema ni Maaruki wa CCM. Bila shaka wameshatumwa na CCM kwenda kuharibu CCJ. Wasiruhusiwe kujiunga na hicho chama hata kidogo.
 
Museven na Kagame nao ndani. Makubwa haya. Maradona atakuja kucheza mechi kukusanya pesa na watu kwa ajili yaCCJ. Muungwana lazima afike.
 
ahmadnajab Rais wa Iran atakuwa mgeni rasmi wakati wa mapokezi ya akina Mrema, Mbatia na Mapalala
 
SIKU mbili baada ya aliyekuwa Mbunge wa Kishapu, Fred Mpendazoe kujiondoa CCM na kujiunga CCJ, chama hicho kipya kimenasa viongozi wengine watatu wa kisiasa nchini na wanatarajia kujiunga rasmi leo.

Viongozi hao ambao ni wenyeviti watatu wa vyama vya upinzani, walithibitisha hilo jana. Nao ni James Mbatia wa NCCR-Mageuzi, Augustine Mrema wa TLP na James Mapalala wa Chausta.

Akizungumza na gazeti hili jana, Mrema alisema sababu za kuhama vyama vyao ni kutokana na kukosekana kwa ushirikiano imara wa kuiondoa CCM madarakani na kuwapo mitafaruku ya hapa na pale katika vyama hivyo.

Alisema maandalizi ya kurudisha kadi za vyama vyao na kuvikabidhi kwa Mwenyekiti wa Muda wa CCJ, Richard Kiyabo, yamekamilika, ikiwa ni pamoja na jukwaa kupambwa na rangi ya njano ya chama hicho.

Alisema kikundi cha futuhi cha Za Komedi nacho kimealikwa katika hafla hiyo inayotarajia kuanza saa nne asubuhi katika viwanja hivyo.

Hili linatazamiwa kuwa pigo kubwa kwa vyama hivyo vya siasa, kwani kuondokewa na wenyeviti watatu kutaviyumbisha na huenda vingine vikatoweka, endapo wanachama wataamua kuwafuata viongozi hao.

Mbatia alipotakiwa kuzungumzia kama haoni kuwa atapoteza kitu kwa kuacha uenyekiti, alisema cheo si tija, bali nia ni kujenga demokrasia ya kweli nchini.

Aliongeza kuwa wamebaini kwamba kuwa na utitiri wa vyama hakuna tija na hivyo wanakumbuka maneno ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere wa kuwa na vyama vichache vya upinzani lakini vyenye nguvu.

Kiyabo alipoulizwa juu ya hatua hii ya kupokea vigogo hao wa kisiasa kujiunga na chama chake, alitabasamu na kushindwa kuzungumza zaidi ya kumwambia mwandishi wa habari hizi: "Nina furaha sana lakini kwa kuwa kesho (leo) ni Aprili mosi, tuonane Mnazi Mmoja baada ya kazi hiyo, tuzungumze zaidi, ingawa hutaniamini."

Mpendazoe juzi alitangaza kuihama CCM na kujiunga CCJ kwa maelezo kuwa chama hicho kikongwe kimeshindwa kupambana na ufisadi na kwamba CCJ ndicho chama mbadala. Habari zaidi zilisema viongozi wengi waandamizi wa vyama vya upinzani na tawala wako kwenye foleni ya kutangaza kujiunga na chama hicho na sasa wanaangalia upepo wa kisiasa unavyovuma.

-Leo ni Siku ya Wajinga Duniani- Mhariri

Source : http://habarileo.co.tz/kitaifa/?n=6467
 
Well crafted Prank.:rolleyes:
Based on our African folklore on this day’s credulity, this thread is naturally bound to evaporate by the afternoon of today.
 
Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kwamba Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeamua kujitoa kwenye Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC), kwa vile imeona hakuna mantiki ya kuingia kwenye muungano mwingine wa nchi tano, kabla ya kutatua matatizo ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Taarifa hiyo ya serikali ambayo gazeti hili lina nakala yake imesema "kwa kuwa muungano wa EAC ni wa nchi tano, kuondoka kwa nchi moja hakutawazuia wale wengine wa nchi nne kuendelea na muungano huo".

Wachambuzi wa mambo wanasema kujitoa kwa Tanzania kumetokana na kuzinduka kwa Chama cha Mapinduzi, chama tawala tanzania, ambacho majuzi kilifanya mkutano mahususi kujadili hatima ya Jamhuri ya Tanzania kwenye muungano wa EAC, kwamba Tanzania ina rasilmali nyingi na haina haja ya kujiunga na EAC.

"Ushirikiano wa kikanda si lazima uwe EAC, sisi tuko SADC. Wenzetu wako IGAD. Zote hizo ni taasisi za ushirika wa kikanda, sehemu ya taarifa inasema.

SOURCE: http://www.jamboleo.co.tz
 
Status
Not open for further replies.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom