Anti-Social wenzangu tujuane tabia zetu

Anti-Social wenzangu tujuane tabia zetu

Sisi ambao tunaenda kusalimia ndugu kila inapobidi, tunawasiliana na majirani zetu, tunahudhuria harusi za watu wetu wa karibu, misibani hatukosi. Kazini zikitokea get together hatukosi pia,nk. Tunaitwaje?
Jina sahihi ni Extrovert wewe una tabia kama zangu ingawa kuna kipindi pesa zilitaka zilitaka kunibadilisha tabia yangu hiyo ambayo ni urithi kutoka kwa babu mpaka kwa baba,mimi ni mtu na familia yangu na mtaani naheshimika ila siku za weekend ni kawaida sana kunikuta kijiweni na vijana wa bodaboda tunakula story,msibani watu wanashangaa ninavyoshika chepe kufukia kaburi wakati wa kumzika marehemu maana imezoeleka watu wa aina yangu kwenye misiba huwa hawashiki jembe,mimi ni mtu peace sana kiasi ambacho sometimes inanicost maana vijana njaa wa dar es salaam huwa hawakauki home kupata kitonga cha msosi Hapa mtaani hakuna mchango wowote ninaolipa kuanzia ulinzi shirikishi na mchango wa aina yoyote wa namna hiyo
 
Anti-social halafu una smart phone!!!??? Wewe una matatizo yako ya kisaikolojia tu, katafute mshauri nasihi akusaidie.
Tena mwingine anasema ni anti-social lakini anashinda kwenye social media. Watanzania kuna tatizo mahali.
Kaomngea ukweli wake,kuwa kwenye social media SII saw hiyo kujumuika
 
Niende moja kwa moja kwenye mada, nina vitabia ambavyo ni ngumu kunibadilisha na kujibadilisha,
(1) Sipendi kuangalia TV, utaniona kwenye TV hasa kukiwa na mpira wa miguu vinginevyo mie ni mtu wa redio kwa sana, tena hasa TBC TAIFA na vipindi vyangu vile taarifa za habari, hotuba za baba wa taifa, muziki wa zilipendwa ukichambuliwa na MASOUD MASOUD mie kwangu burudani kabisa.

(2) Mwanamke/Msichana akijipodoa sana kwangu anaboa. Akijitoboa pua yake hata kutazama sura naogopa kabisa, akijifunga vikuu miguuni ananiboa, n.k.Napenda sana Mwanamke awe Natural, yaani aoge zake apake mafuta yake ya nazi na kumchana nywele zake au asile twende kilioni[emoji1787][emoji1787]

(3) Sherehe Sherehe hizi sijui za Ndoa, Birthday DAAAH hizo ndio sizipendagi kabisa, kama ndoa nitaishia kutoa mchango tu lakini ukumbini hunioni. Kichwani naona kama kupotezeana muda tu, watu wanaonyeshana uzuri wao, mavazi yao, na ratiba nyingi zisizo na kichwa wala miguu.

(4)Nipo DSM kwa zaidi ya miaka 20 tokea nipo Form 1 sijatoka tena lakini kwenda Beach kujipumzisha hata mara 10 hazifiki. Hayo maonyesho ya Sabasaba hata viwanja vyenyewe sijawahi kukanyaga, n.k.

Kwa ufupi kama sina Issue ya kunitoa Home, nitakaa tu na watoto wangu wanafanya home work zao za shule mie nipo pembeni yao nasoma vitabu vyangu vya riwaya tu vya akina Willy Gamba, Ben Mtobwa,Hammie Rajab, John Simbamwene, n.k nikichoka Riwaya nitarukia vitabu vya akina Kiyosaki,Robin Sharma.

NAENJOY maisha yangu
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Una mambo ya kizamani..wewe ni mkoloni
 
Mimi sipendi mijumuiko ya watu huwa napenda kukaa peke yangu rafiki yangu mkubwa ni simu napenda game na kuingia kwenye social network tena kusoma vitu vya msingi.

Sipendi vichekesho, hapa kwenye Radio tumefanana kipindi nipo shule ilikuwa asubuhi nawasha nasikiliza BBC swahili mpaka wanafunzi wenzangu wakawa wananishangaa.

Wanawake sipendelei mpaka nilivyokuja kuoa na mkewangu ananiona naboa maana huwa simuongeleshi sana au kumchekesha na akiniambia kitu cha luchekesha wala huwa sicheki
Kwa hiyo mkuu kutokumchekea mke wako hiyo nayo Sifa?Nchi ina safari ndefu sana asee

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Jina sahihi ni Extrovert wewe una tabia kama zangu ingawa kuna kipindi pesa zilitaka zilitaka kunibadilisha tabia yangu hiyo ambayo ni urithi kutoka kwa babu mpaka kwa baba,mimi ni mtu na familia yangu na mtaani naheshimika ila siku za weekend ni kawaida sana kunikuta kijiweni na vijana wa bodaboda tunakula story,msibani watu wanashangaa ninavyoshika chepe kufukia kaburi wakati wa kumzika marehemu maana imezoeleka watu wa aina yangu kwenye misiba huwa hawashiki jembe,mimi ni mtu peace sana kiasi ambacho sometimes inanicost maana vijana njaa wa dar es salaam huwa hawakauki home kupata kitonga cha msosi Hapa mtaani hakuna mchango wowote ninaolipa kuanzia ulinzi shirikishi na mchango wa aina yoyote wa namna hiyo
Mkuu wewe ni social sana mkuu tunalandana kwa personality.
 
Niende moja kwa moja kwenye mada, nina vitabia ambavyo ni ngumu kunibadilisha na kujibadilisha,
(1) Sipendi kuangalia TV, utaniona kwenye TV hasa kukiwa na mpira wa miguu vinginevyo mie ni mtu wa redio kwa sana, tena hasa TBC TAIFA na vipindi vyangu vile taarifa za habari, hotuba za baba wa taifa, muziki wa zilipendwa ukichambuliwa na MASOUD MASOUD mie kwangu burudani kabisa.

(2) Mwanamke/Msichana akijipodoa sana kwangu anaboa. Akijitoboa pua yake hata kutazama sura naogopa kabisa, akijifunga vikuu miguuni ananiboa, n.k.Napenda sana Mwanamke awe Natural, yaani aoge zake apake mafuta yake ya nazi na kumchana nywele zake au asile twende kilioni[emoji1787][emoji1787]

(3) Sherehe Sherehe hizi sijui za Ndoa, Birthday DAAAH hizo ndio sizipendagi kabisa, kama ndoa nitaishia kutoa mchango tu lakini ukumbini hunioni. Kichwani naona kama kupotezeana muda tu, watu wanaonyeshana uzuri wao, mavazi yao, na ratiba nyingi zisizo na kichwa wala miguu.

(4)Nipo DSM kwa zaidi ya miaka 20 tokea nipo Form 1 sijatoka tena lakini kwenda Beach kujipumzisha hata mara 10 hazifiki. Hayo maonyesho ya Sabasaba hata viwanja vyenyewe sijawahi kukanyaga, n.k.

Kwa ufupi kama sina Issue ya kunitoa Home, nitakaa tu na watoto wangu wanafanya home work zao za shule mie nipo pembeni yao nasoma vitabu vyangu vya riwaya tu vya akina Willy Gamba, Ben Mtobwa,Hammie Rajab, John Simbamwene, n.k nikichoka Riwaya nitarukia vitabu vya akina Kiyosaki,Robin Sharma.

NAENJOY maisha yangu
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
3 na 4 tuko pamoja
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom