Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Acacia wanadai Trilioni 5

Ile meli ya samaki za Magufuli,wenyewe wameamka wanadai Trilioni 1.2

Jumla trilioni 6.2, hii no hasara tuliyopata kutokana na wewe kuvunja mikataba na taifa litatakiwa kulipa,

Hizi trilioni ni sawa na makusanyo ya kodi ya miezi sita

Bado bilioni 87 za wale jamaa waliokamata bombadia

Ile sheli ya MWARABU uliyovunja mwanza tulilipa mamia ya mabilioni

Wizara ya ujenzi inaongoza kwa kushtakiwa na wananchi na kudaiwa matrilioni

Sasa Mimi nakuuliza,tangu tupate Uhuru,ni maamuzi ya waziri gani/kiongozi yaliyolitia hasara taifa zaidi ya trilioni 6? Na huyo ni waziri mmoja/kiongozi

Tumesikia mawaziri wanaofata sheria na taratibu wakiitwa wapumbavu kwa kuchelewa kuamua,je wafanye maamuzi kama yako yatakayoitia serikali hasara ya matrilioni? Kufata sheria na taratibu imekuwa upumbavu siku hizi?

Sasa kila waziri akikurupuka na mwishowe akaishia kuleta madeni ya trilioni 6,na nchi INA mawaziri zaidi ya 30,si nchi itakuwa inadaiwa trilioni 180?

Sisi tunataka utuambie wewe mwenyewe,wewe binafsi,bila kutumia kodi zetu,umejipangaje kuwalipa hizo trilioni 6

Binafsi naamini madeni yote ya kuvunja mikataba kutokana na maamuzi yako yanaweza kufika trilioni kumi,zikikusanywa kesi zote za pale wizara ya ujenzi na sasa ukiwa mkuu,

Hii no hasara iliyoletwa na mtu mmoja tu!
Huyu anaipeleka nchi kuzimu
 
Kuna viongozi wavuta bangi WAPOO kwani wanamaamuzi kii." Ney wa mitego.
 
maskini watz wanaodaiwa kodi mitaani,wauza mitumba na sahani za njugu ndio watakaolipa madeni na kuendea kudidimia kwa hali za maisha yao na watoto wao kwa miaka 50 ijayo.
sasa tusubiri hilo deni la mchanga wa dhahabu hilo litakuwa trilion 10 peke yake
 
Hayo madeni yatalipwa kwa kutumia misaada mbalimbali tunayopokea kutoka kwa wahisani, mfano pesa ya Thisisbillgates.

Sent from my Priceless H40-D00 using JamiiForums mobile app
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom