Anaweza kuondolewa Madarakani, Iwapo...

Anaweza kuondolewa Madarakani, Iwapo...

Hivi Job Ndugai waliwezaje kumpokonya uspika? Kuna utaratibu wa kisheria uliotumika au ni wahuni wa mfumo walipewa kandarasi ya kumpiga chini
Hivi Kasim Majaliwa alizuiwa na nani kwenda kuchukua form ya kugombea tena baada ya kuahidi kugombea akiwa anaaga bunge?
Labda walimuambia watazima betri inayopump mashine ya Moyo wake kwa remote akina isiwe taabu
 
Makamu wa Rais lazima awe mwanchama wa chama cha siasa. Ndiyo maana CCM ilibadili katiba yake ili Rais awe pia Mwenyekiti wa Chama. Kwani ukitaka kumuondoa Rais, unamfukuza uanachama. This is simple
Kwani ukimfukuza uanachama na akapewa uanachama wa chama kingine muda huo huo bado sheria au katiba itamlazimisha aondolewe umakamu?
Hapa nauliza sijui kitu.
 
Sidhani ni jambo la kupotezea. Kuweka RIP baada ya jina, kwa mtu aliye hai ni jambo linalohitaji kurekebishwa. Ndiyo nilichofanya mimi, nimemwa-alert ili afanye marekebisho. Pengine alikuwa anadhani Malecela alishafariki?
Namchanganyaga Malecela na Msuya.
Ni kweli Malecela yuko hai.
Komradhi.
 
Kwani ukimfukuza uanachama na akapewa uanachama wa chama kingine muda huo huo bado sheria au katiba itamlazimisha aondolewe umakamu?
Hapa nauliza sijui kitu.

Unajua Makamu tumemchagua kwa kura.

akijiuzulu au kufariki ni sawa. Atapendekezwa mwingne na Raisi alaf Bunge litampitisha.

Ila hii kuvuliwa uanachama katiba inamlinda.
 
Kugombea Makamu wa Raisi ni lazima uwe Mwanachama wa chama cha siasa.

Ukishaupata . Alaf ukawa sio mwanachama. Haikomi ww kuwa makamu wa Raisi.

Kumbuka kachaguliwa na Wananchi.
Yaan walimpa kura ya Ndio.

Sasa ukichagua Makamu wa Raisi mwingne ambaye hajachaguliwa na wananchi unaenda kinyume na katiba.
Unapwaya ndugu kuna mazingira yanaruhusiwa na katiba .
Rais anateua makamu wa Rais na anapitishwa na bunge.
Ilishatokea hapa Tz.

Katiba haijasema moja kwa moja makamu wa Rais akikoma uanachama inakuwaje.
Ila imesema Mtu hatakuwa makamu wa Rais mpka awe na chama.
Wajanja wanaweza kuutumia huo mwanya kukunyan'ganya cheo.
 
Halafu kitu kingine.

Makamu Rais akiondolewa madarakani kupitia mchakato wa Bunge.
anakosa sifa za kuwa Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, au Rais wa Zanzibar.
Maisha yake yote.
Ibara ya 50(5) Katiba ya JMT.
 
Acheni ndoto za mchana, mtakuja kata gogo bure kitandani. Samia yupo hadi 2030 kwa mujibu wa Katiba. Kama na wewe hukupiga kura kwa kuiamini NRNE shauri yako.

Hizo bad wishes mnazo mombea kumbukeni Mungu haishi mtaani kwenu. Kadri mnavyomtakia mabaya ndivyo Mungu anamuinua.
Anayeongelewa ni Imma wewe chawa, hata kuelewa hili umeshindwa kweli!!??

Mungu yupi na anamuaonuaje huyo Samia wako?
Shetani ni mungu wa dunia hii na watawala wengi wanainuliwa naye kwa "mikataba".
 
Si imezoeleka ukienda kinyume na yeye anakuvua vyeo.

waziri wa mambo ya ndani,George Simbachawene baada ya kutoka hadharan na kusema polisi wakienda kumkamata mtu wafuate taratibu na wavae sare za kiaskari na waseme wanampeleka wapi yule mtu.

Baada ya siku 2 akapoteza uwaziri.

Kuna yule mwingne alisema Mama anakopa kopa na deni la taifa ni kubwa. Kesho yake akaandikiwa barua ya kujiuzulu Uspika.

Sasa huyu, kuna kaugumu kidogo.
Ndio maana anajiamini.
Tuna katiba ya kipuuzi sana, rais ndio Mungu. Hukumbuki CAG alitolewa kwa mizengwe ya bei rahisi kabisa pamoja na kinga zake zote?
 
Kuna Ugumu ndio Maana anajiamini atakaa hadi 2030.

Ingawa Inawezekana akaondolewa madarakani.

Iwapo amefanya vitendo vinavyovunja Katiba au Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Pale anaposhindwa au kuacha kutekeleza kazi na majukumu ya kiti chake.

Kama amepatikana na hatia ya kosa la jinai linaloonyesha utovu wa uaminifu.

Njia pekee ni kuanzisha Mchakato Bungeni

Raisi mwenyewe anaweza kuwasilisha Bungeni hati ya kuliomba Bunge lipitishe azimio la kumwondoa kwa madai ya kushindwa au kuacha kutekeleza kazi zake.

Au Mbunge yeyote anaweza kuwasilisha hoja binafsi Bungeni ya kutaka kumwondoa madarakani kwa misingi ya kuvunja katiba au kukiuka maadili ya umma, na endapo taratibu na idadi maalum ya kura za wabunge zitafikiwa kwa mujibu wa sheria.

Au Yeye mwenyewe aandike barua ya kujiuzulu .

Ila Kumvua uanachama hakumwondoi moja kwa moja madarakani, kwani Katiba haina kifungu kinachomfuta kazi. kiongozi huyo papo hapo kwa kupoteza kadi ya chama chake.

au pengine Labda Itumike njia nyingne ya kumuondoa.
sijasema Kumuwekea Sumu.

Na hili halihusiani na Makamu wa Raisi.

Nimewaza tu.
Nasikia kale kadubwana ka Kisarawe kameshapewa kandarasi hiyo.
 
Tumngoje baba levo na Taletale kama watatimba na hujja binafsi ya kumfurumusha kazini kipenzi wetu
 
Back
Top Bottom