Anatomy of Incompetence; A Pattern of Mediocrity

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
1984- Masange JKT (Tabora) (Operesheni Nguvu Kazi) mlipuko wa baruti katika kutishia simba wala watu. Walijeruhiwa Luteni Usu Msange, Mwangupile (alikatwa mkono) na wengine kunusurika miongoni mwao mwandishi mashuhuri Chemi Che Mponda.

Januari 5, 1999 – Bomu lalipuka pembeni ya Ofisi ya CCM, Kata ya Bulele, Muleba huko Kagera, jengo laharibiwa upande.

Disemba 25, 2005 – Bomu laua 1, na watano wajeruhiwa kijiji cha Mlela Kigoma

Disemba 27, 2006 – Bomu la mkono lalipuka Kurasini kwenye eneo la kukusanyia vyuma chakavu, mmoja afariki, 5 wajeruhiwa. Baada ya uchunguzi zaidi Mengine 43 yaligundilika kiwanda cha Quaim Steel Mills Chang’ombe, Dar na lingine moja lililookotwa ndani ya kiwanda cha Dabaga.

Mshangao mkubwa ni pale bomu mojawapo lilipokutwa linatumika
kama mfuniko wa rejeta ya kijiko cha kupakia/kupakua mizigo ndani ya ghala la Hahrour Enterprises.

Oktoba 15, 2007 – Bomu laua 4 wa familia moja huko Bukoba baada ya mtoto kuokota bomu hilo na kuliweka motoni akidhania kiazi. Mmoja ajeruhiwa.

Disemba 10, 2007 – Watoto 3 wauawa na bomu Makutopora Dodoma, 6 wajeruhiwa

Mei 20, 2008 – Kundi la Majambazi wapatao 15 wavamia basi walilipua kwa mabomu kwenye msitu wa Kimisi, Karagwe huko Kagera. 2 wauawa papo hapo. Mmoja ni askari mwenye silaha aliyekuwa akilisindikiza basi hilo. Aliuawa kishujaa lakini jina lake halikuimbwa kwa sifa kama alivyofanyiwa yule aliyeokoa mamilioni pale Ubungo!

Juni 9, 2008 - Helikopta ya Jeshi yaanguka na kulipuka, watu sita wafariki

Novemba 12, 2008, Mama na Mtoto wauawa na Bomu Kilosa wakiwa shambani.

Disemba 21, 2008 – Watoto 4 wa jamii ya Kimasai walipuliwa na Bomu kijiji cha Embokoi, Siha huko Kilimanjaro karibu na bonde la Kilelepori ambapo Polisi hufanyia mazoezi ya silaha za moto

Januari 3, 2009 – Bomu lalipuka Kambi ya Raha, mji wa Bomang’ombe huko Hai Kilimanjaro, 2 wajeruhiwa.

Feb 13, 2009 – Washtakiwa 2 walipukiwa na Bomu Mahakamani Kasulu, Kigoma na mmoja kujeruhiwa katika jitihada za kutaka kutoroka.

Aprili 29, 2009- Mlipuko mkubwa wa mabomu ya kawaida na makombora watokea ghala ya silaha ya JWTZ kikosi cha 511 Mbagala ambapo watu 15 wauawa na zaidi ya 600 wajeruhiwa.
 
Bila shaka kuna sheria inayosema ghala la mabomu haliwezi kuweko sehemu za makazi ya raia. Hakuna aliyeijali. Ajali imetokea sasa, na bila shaka hakutakuwepo na auditing ya usalama wa maghala yote ya jeshi. Tusibiri ajali zaidi
 
What a pattern, MKJJ umeitoa wapi? What else would you call this other than sheer incompetence and utter negligence?

kwa kifupi ni kuwa sisi hatujifunzi. Ngoja msikie ajali nyingine za moto ukiwaoka watoto wetu tena mwaka huu na wote tutabakia kushtuka na kuimbiwa "mapenzi ya Mungu".
 
kwa kifupi ni kuwa sisi hatujifunzi. Ngoja msikie ajali nyingine za moto ukiwaoka watoto wetu tena mwaka huu na wote tutabakia kushtuka na kuimbiwa "mapenzi ya Mungu".

Unajua jana nilikaa nikafiria, kama pale Dar kuna kituo kimoja tu cha zimamoto, je kule Kyela viko vingapi?

Sijui zile hela zote za EPA zingeweza kujenga vituo vingapi vya zimamoto...
 
Unajua jana nilikaa nikafiria, kama pale Dar kuna kituo kimoja tu cha zimamoto, je kule Kyela viko vingapi?

Sijui zile hela zote za EPA zingeweza kujenga vituo vingapi vya zimamoto...

kujiuliza maswali namna hiyo kunaweza kukufanya uwe depressed.. mara nyingi ni rahisi kwa watu kukubali kilichopo kuliko kufikiria kile ambacho kinapaswa kuwa.
 
When I saw this tittle, I thought MJJ was bringing an anatomical breakdown of the JK government which is completely Incompetent and full of Mediocre.

However, what you have highlighted is one of many catastrophies that are bound to repeat themseleves in our beloved country, because those in power have considered them to be unavoidable, but are they realy unavoidable? Well done MJJ.
 
Tatizo ni kuwa hivi vyote havionekani katika picha moja.. tunaviona vipande vipande na kuamini vyote ni bahati mbaya, mapenzi ya Mungu, ajali haina kinga n.k Tukiviweka pamoja na kuviangalia kwa ukaribu tunaweza kuona kuwa nyuma yake kuna kitu cha kutisha zaidi!
 
Kama kweli serikali yetu inatujali na sisi wenyewe wananchi tunathamini maisha yetu, napendekeza hatua zifuatazo zichukuliwe:

1. Serikali ichukue hatua ya kuelimisha wananchi kupitia vyombo vya habari miundo (forms) na athari za silaha za moto haswa mabomu. Kama wananchi wanadhani mabomu ni viazi, mahindi, kifuniko cha rejeta, chuma chakavu, toy, n.k hii inaashiria kutokuwepo kabisa kwa maarifa katika jamii.

2. Polisi na Jeshi wawe makini zaidi wanapofanya mazoezi ya kutumia silaha za moto. Aitha, kila silaha inayotumika kwenye mazoezi iwe na namba na baada ya mazoezi tathmini ifanyike kuoanisha matumizi ya silaha kulingana na namba zilizotolewa. Lazima awepo wakuwajibika iwapo silaha/bomu itapotea.

3. Serikali ichukue hatua kuhakikisha watu hawajengi makazi, shule, zahanati na biashara karibu na maeneo ya polisi, jeshi na maghala ya kuhifadhia silaha. Katika hali ya sasa ambapo ni dhahiri kabisa serikali ilizembea mpaka makazi ya watu yamezingira maeneo ya polisi/jeshi, serikali ichukue jukumu la kuhamisha maghala ya silaha na maeneo ya mazoezi kwingineko ambako hakuna makazi ya watu.
 
tunaishi kwa nasibu sana; tunaishi kwa kutegemea "mapenzi ya Mungu" na hivyo tunaoombea mambo hayatakuwa mabaya.

Nilitoa pendekezo zamani sana kwenye "Taifa lisilojiandaa kwa Majanga" na kusema kuwa milango ya mashule yote na maeneo yote ya hadhara (public accommodation facilities) ifungukie kwa nje. Mabweni, mahospitali, n.k Hadi leo hakuna kiongozi anayefikiria jambo hilo kulifanya.

Siku watu wakiokwa tena au kufa katika mazingira ya kizembe kama wale watoto 19 Tabora utasikia watawala wanavyokimbia kwenda kutoa pole na rambi rambi wakija na tume mpya ya kuchunguza!
 
Thank you Mzee Mwanakijiji for so painstakingly listing the explotion accidents that have become so widespread in our beloved country. After the Mbagala disaster, I expected the authorities to demostrate their alarm and concern by taking drastic action, both political and administrative, but it appears that they have forgotten. Even Parliament is treating this latest conflagration as "matters as usual".

It is obvious that in this country, leadership is mediocre in the extreme resulting in ineptitude and incompetence in fullfilling their functions and responsibilities, especially that of safeguarding the lives of the people. It is not a matter of organizing demonstrations, as suggested by JF Member Shy. It is a question of studiously planning the removal from power, the party that has relinquished its responsibility to fellows only mindful of filling their pockets and bank accounts with ill-gotten fortunes.

It is a political question and has to be tackled politically. Rally up to the parties that can save us from this impasse.
 
Mwananchi

Askari walipua mabomu 250 shambani kwa mkulima Kagera Lilian Lugakingira,Bukoba
JESHI la Polisi mkoani Kagera kwa kushirikiana na Jeshi la Wananchi (JWTZ)wamefanikiwa kulipua mabomu 250 yaliyogunduliwa na mwananchi mmoja katika kijiji cha Bisole kata ya Muhutwe wilayani Muleba.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa Henry Salewi alisema kuwa mabomu hayo ya kutupwa kwa mkono yaligunduliwa na mwanakijiji hicho, Reticia David ambaye aliyachimbua mabomu zaidi ya 20 ya kutupwa kwa mkono kutoka ardhini wakati akilima katika shamba lake.



Kamanda Salewi alisema kuwa mabomu hayo ambayo yalilipuliwa jana yaligunduliwa Julai 30 mwaka huu na mwanakijiji huyo.

Kamanda alisema mama huyo alichimbua mabomu hayo wakati akilima matuta ya viazi na kuwa baada ya kuyachimbua alimwita mme wake wakaendelea kuchimbua wakidhani ni dhahabu.

Wakati wanandoa hao wakiendelea kuchimbua waliona visanduku ambavyo viliwafanya kuwa na wasiwasi na kuamua kutoa taarifa polisi.

Kamanda wa polisi mkoani Kagera Henry Salewi alisema baada ya polisi kupata taarifa hizo waliwahi sehemu ya tukio na kubaini kuwa sio dhahabu bali ni mabomu ya kutupwa kwa mkono.



Kamanda Salewi alisema kuwa polisi waliwasiliana na Jeshi la Wananchi Tanzania kwa lengo la kupata msaada zaidi na eneo hilo lilizingirwa na polisi ili kuzuia wananchi wasifike katika eneo hilo hadi jana mabomu hayo yalipolipuliwa.

Hata hivyo, mabomu aliyochimbuliwa na mwanakijiji huyo yalikuwa 20 lakini mabomu mengine zaidi yalichimbuliwa na polisi kwa kushirikiana na JWTZ hadi kufikia mabomu 250.

Kamanda huyo alitoa tahadhari kwa wananchi katika mkoa wa Kagera hasa waishio maeneo ya mipakani kuwa makini na vitu vinavyopatikana katika maeneo yao ambavyo havieleweki na kuwa endapo vitaonekana watoe taarifa polisi ili vifanyiwe uchunguzi kabla ya kuleta madhara zaidi.

My Take:
Mabomu 250!? hivi hao watu wa mikoa ya kanda ya ziwa wamewahi kuona picha ya mabomu ya mkono?
 
Back
Top Bottom