The Bee Gees: As long as you're having fun, that's the key, Sehemu ya Pili

Damaso

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
1,662
2,219
Tumalizie sehemu ya mwisho ila kama hujasoma sehemu ya kwanza unaweza kuisoma hapa The Bee Gees: As long as you're having fun, that's the key, Sehemu ya Kwanza
Karibu sana
Kwenye kipindi mubashara cha The Midnight Special mwaka 1975, The Bee Gees waliipatia dunia kionjo kizuri sana kwa kuimba wimbo wa "To Love Somebody" wakiwa pamoja na Helen Reddy, sauti zilizoimbwa siku ile ilikuwa ni fire bin fire! kisha The Bee Gees walifanya marudio ya covers tatu za bendi ya Beatles kwa hakika walionesha uwezo wa ajabu.
KISS.Midnight Special.1975.She.MSYT.04-23.jpg

Albamu iliyofuata ilikuwa ni Children of the World ambayo ilitoka Septemba 1976 huku kukiwa na ufundi wa Sanaa mkubwa kutoka kwa Barry pamoja na Weaver. Wimbo wa kwanza "You Should Be Dancing" ulikuwa ni moto sana, huku kukiwa na ushiriki kutoka kwa Stephen Stills katika ala yake ya muziki. Wimbo huu uliwasukuma zaidi the Bee Gees kufika viwango vikubwa zaidi vya kimuziki ndani ya Marekani. "Love So Right" ilishika namba tatu kwenye chart, "Boogie Child" ilishika namba 12 na albamu hii ilishika namba nane kwa Marekani. Ubabe wa the Bee Gees ukarejea kwa kishindo katika burudani.

Baada ya kupata mafanikio makubwa sana kwenye albamu zao pamoja na albamu mubashara ya Here at Last... Bee Gees... Live ambayo ndani yake ilikuwa na nyimbo zilizoimbwa mubashara, basi the Bee Gees wakamshauri Stigwood kuwa washiriki kwenye kutengeneza wimbo wa utambulisho wa filamu ya Saturday Night Fever, na hapa ndo Maisha yao yalibadilika kabsa. Kuhusika kwa the Bee Gees katika filamu haikuwa kazi rahisi hata kidogo, hata John Travolta alidai kuwa alifahamu kuceza nyimbo za kina Stevie Wonder pamoja na Boz Scaggs ila akakutana na midundo ya the Bee Gees, na ajabu ni kwamba walivyopewa tenda hiyo tu wakaingia kazini huku wakitumia siku mbili kuandika wimbo huo pale kwenye studio za Château d'Hérouville studio huko Ufaransa, Stigwood aliongozana na Bill Oakes na walidhani kama ni masihara vile ila walivyosikiliza wimbo ule walibakia midomo wazi.

MV5BMTAxNTM2Mjc2OTZeQTJeQWpwZ15BbWU4MDE4NDQ3MjUz._V1_.jpg

Kiuhalisia bendi ya the Bee Gees walikuwa ni kama wamechoka ila hakukuwa na namna ya kufanya kazi vibaya, hivyo walipiga kazi kama ndo kazi yao ya mwisho, Bill Oakes alikuwa ni msamizi wa muziki na midundo katika filamu hiyo aliona ajabu saa kusikiliza wimbo mara moja ya kutoa nyota zake tano bila kuonesha udhaifu wowote, binafsi aliona kuwa wimbo huu utaibeba zaidi filamu hii.
How_Deep_Is_Your_Love.jpg

Nyimbo tatu za The Bee Gees, —"How Deep Is Your Love" (Marekani ilishika namba. 1, Uingereza Namba. 3), "Stayin' Alive" (Marekani ilishika namba. 1, Uingereza ilishika namba. 4) pamoja na "Night Fever" (Marekani ilishika namba. 1, Uingereza ilishika namba. 10 huku katika nchi zingine zikitikisa charts zao kwa kishindo kikubwa sana haswa ukizingatia kuwa midundo ya sasa ilikuwa na ala za R&B pamoja na Disco fulani hivi. Pia The Bee Gees waliandika wimbo wa "If I Can't Have You", ambao uliimbwa na Yvonne Elliman na ulishika namba moja kwa Marekani

Kwa kifupi ni kwamba katika kipindi cha miezi tisa kuanzia Krismas 1977, The Bee Gees walikuwa na nyimbo saba ambazo wameziandika zimepata kushika namba moja ndani ya Marekani kwa wiki 27 kati ya wiki 37, nyimbo tatu zilikuwa ni za The Bee Gees moja kwa, mbili zilikuwa ni za Kaka yao Andy Gibb, wimbo mmoja wa Yvonne Elliman pamoja na "Grease", ambao uliimbwa na Frankie Valli. Ajabu sana hii!

maxresdefault.jpg

Kutokana na mafanikio ya filamu hiyo, wimbo huo ulikwenda kuweka rekodi kubwa, huku ikiwa ndo albamu yenye mauzo amiubwa zaidi katika historia kipindi hicho, ikiwa na mauzo ya nakili zaidi ya milioni 40 kwa hakika Saturday Night Fever ni miongoni mwa albamu tano zenye mauzo makubwa, kwa mwaka 2010 ilikuwa nafasi ya nne kidunia.

Machi 1978 the Bee Gees walikuwa wameshika nafasi mbili za juu za charts za Marekani wakiwa na nyimbo za "Night Fever" pamoja na "Stayin' Alive", mara ya kwanza kutoka tangu the Beatles walipofanya hivyo. Kwenye chart za US Billboard Hot 100 za Machi 25 1978, nyimbo tano zilizoandikwa na Kaka kutoka familia ya Gibbs zilikuwa kwenye chart za nyimbo bora 10 kwa wakati mmoja: "Night Fever", "Stayin' Alive", "If I Can't Have You", "Emotion" and "Love Is Thicker Than Water". Kitu kama hiki kutokea kwenye chart hizi sio rahisi hata kidogo, na hakikuwahi kuonekan tokea Aprili 1964 pale ambapo the Beatles walipokuwa na nyimbo tano pia.

the-bee-gees-l-r-maurice-gibb-robin-gibb-and-barry-gibb-pose-for-a-live-portrait-session-in-th...jpg

Barry Gibb akaenda mbali na kuvunja rekodi ya John Lennon pamoja ile ya Paul McCartney iliyowekwa mwaka 1964, Barry akapewa taji la kuwa mtunzi pekee mwenye nyimbo nne ambazo zimeshika namba moja kwenye charts za US, "Stayin' Alive", "Love Is Thicker Than Water", "Night Fever" and "If I Can't Have You", hapa ndo utaona kuwa Robin alikuwa na wivu kwa kaka yake ambaye nyota yake ilikuwa ni angavu (tuache wivu wa kijinga tuache kuonea watu gere).
grammy_rewind_hero.jpeg.jpg

The Bee Gees walishinda tunzo tano za Grammy kupitia wimbo wa Saturday Night Fever katika kipindi cha miaka miwili: Albamu bora ya mwaka, Mzalishaji bora wa mwaka wakiwa na Galuten pamoja na Karl Richardson, tunzo mbili za Best Pop Performance by a Duo or Group with Vocals (Moja ilikuwa ni 1978 kupitia wimbo wa "How Deep Is Your Love", na nyingine ni 1979 kupitia "Stayin' Alive") pamoja na tunzo ya Best Vocal Arrangement for Two or More Voices kupitia wimbo wa "Stayin' Alive", basi Kuna sehemu wanasema “Well, you can tell by the way I use my walk……. I'm a woman's man, no time to talk……………. Music loud and women warm………… I've been kicked around” safi sana!
Katika kipindi hiki pia Barry pamoja na Robin walishirikiana kuandika wimbo wa Emotion kwa ajili ya swahiba yao, Samantha Sang, wimbo huu uliingia na kushika nafasi za juu za chart za Australia pamoja na Marekani huku pia the Bee Gees wakitoa msaada kama waimbaji wa ziada. Barry fundi wa kuandika mistari aliandika wimbo kwa ajili ya filamu ya muziki ya Grease for Frankie Valli, wimbo ambao ulikwea na kufika namba moja.

SWAHIBA.jpg

Mwaka 1978 The Bee Gees walikuwa nyota pamoja na Peter Frampton wakiwa na muongozaji Robert Stigwood katika filamu ya Sgt. Pepper's Lonely Hearts Club Band, filamu hii ilitangazwa kwa uzito mkubwa sana, ingawa haikupata mafanikio kama wengi walivyo tarajia. Ila Sgt. Pepper's Lonely Hearts Club Band haikuwaacha patupu The Bee Gees kwani wimbo wa "Oh! Darling", ambao uliimbwa na Robin Gibb ulifika mpaka nafasi ya 15 kwenye chart za Marekani.

Spirits Having Flown ni albamu nyingine ambayo ilitoa vyuma vizito pia, nyimbo kama vile "Too Much Heaven" (Marekani ilishika namba 1, Uingereza ilishika Namba. 3), "Tragedy" (Marekani ilishika namba. 1, Uingereza ilishika namba 1), pamoja na "Love You Inside Out" (Marekani ilishika namba 1, Uingereza ilishika namba 13). Kwa mara nyingine tena The Bee Gees wakaweka rekodi ya kipeke, ya kuwa na nyimbo sita mfululizo zilizoshika namba moja ndani ya Charts za Marekani ndani ya mwaka mmoja na nusu, rekodi ambayo pia wanayo The Beatles huku wakiwa wamezidiwa tu na Whitney Houston.

maxresdefault (1).jpg

January 1979 the Bee Gees walifanya onyesho la kuimba wimbo wa "Too Much Heaven" ikiwa ni sehemu ya mchango wao kwenye muziki katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa wakiwa na UNICEF. Majira ya joto the Bee Gees walifanya ziara kubwa sana za muziki ndani ya Marekani na Canada. Ziara ya muziki ya The Spirits Having Flown ilitosha kufanya mauzo ya tiketi kumalizika siku mbili kabla ya tamasha katika Majiji zaidi ya 38. The Bee Gees walitengeneza na kutoa video kwa ajili ya wimbo huu wa "Too Much Heaven", video ambayo iliongozwa na mtengenezaji wa filamu Martin Pitts huku mzalishaji akiwa ni Charles Allen, na hapa ukawa mwanzo wa mahusiano mazuri ya karibu baina ya Pitts pamoja na Allen kwa bendi ya The Bee Gees.
images.jpg

The Bee Gees walipotoa wimbo wa "Rest Your Love on Me", ulibamba sana ndani ya Marekani na kuwa hit song kwa ukubwa wake, wismbo ambao uliingia kwenye chart za nyimbo bora 40. Baada ya kutesa sana soko la muziki haswa kuanzia 1975 mpaka 1979, walibakia na chuma kimoja tu kwenye chart ya nyimbo 10 ndani ya Marekani, mpaka mwaka 1989 ambapo wimbo wa "One" uliposhika namba saba kwenye chart hiyo. bInafsi Barry alidai kuwa mafanikio yao enzi za Saturday Night Fever ulikuwa nusu baraka na nusu mkosi, kwa sababu moja, wimbo wa fever ulikuwa ni nambari moja kila wiki, kwa wiki zaidi ya 25 hakuna wimbo ambao ulionesha hadhi zaidi ya Fever, watu walitamani kupata saini za The Bee Gees, mapaparazi kuwasumbua muda wote kutafuta habari na mahojiano, na walishukuru kuona kuwa Fever sio namba moja tena kwenye chart.

Machi 1980 Barry Gibb alifanya kazi na Barbra Streisand katika albamu yake ya Guilty, ambapo Barry alikuwa kama mzalishaji na kuandika utunzi wa nyimbo tisa zote za albamu hiyo (nyimbo nne aliandika akiwa na Robin huku wimbo mkuu akiandika na Robin pamoja na Maurice). Katika picha ya cover alitokea Barry aiwa na Streisand. Albamu hii ilikwea mpaka kushika namba moja ndani ya Marekani na Uingereza sawa na wimbo wa "Woman in Love" ambao uliandikwa na Barry pamoja na Robin, wimbo huu uikuwa ndo wimbo bora zaidi kutoka kwa Streisand na ndo ulitia nakshi albamu yake kwa upana zaidi.

403d02-20130806-bee-gees.jpg

1981 wazee wa kazi, the Bee Gees waliachia albamu yao ya Living Eyes ikiwa ni albamu yao ya mwisho kutoa wakiwa na record label ya RSO, na kwa upekee albamu hii ilikuwa ni albamu ya kwanza kuwa na CD kuchezwa na hadhira, mwanzo albamu zilikuwa zinatolewa kwa mfumo wa Cassete, mbaya zaidi albamu hii ilifanya vibaya kwani haikuingia kwenye chart za Marekani wala Uingereza, hivyo kuvunja ile rekodi yao ya kuingia albamu bora kwenye chart kuanzia ile albamu ya "Jive Talkin'" mwaka 1975. Nyimbo mbili tu ndo zilipata nafuu, —"He's a Liar" ambayo ilishika namba 30 huku "Living Eyes" ikishika namba 45.
Queen.jpg

1982 Dionne Warwick alipiga pesa na umaarufu mkubwa kupitia wimbo wa "Heartbreaker", kwa kushika namba mbili Uingereza na namba moja ndani ya Marekani, wimbo ambao ulikuwa ndani ya albamu yake ya "Heartbreaker", albamu ambayo nyimbo zake ziliandikwa na bendi ya the Bee Gees na kuzalishwa na Barry Gibb, albamu hii ilishika namba tatu Uingereza na kuingia kwenye albamu bora 30 ndani ya Marekani ambapo ilipata kupewa gold certification.
dolly-parton-kenny-rogers-021623-ab3da58ae50a48c297de712c6610ef64.jpg

1983, maguru wawili Dolly Parton pamoja na Kenny Rogers walirekodi na kuurudi wimbo wa the Bee Gees, "Islands in the Stream", na unakwa namba moja kwenye chart za Marekani na Autralia huku ukiingia kwenye chart za nyimbo 10 bora Uingereza. Albamu ya Rogers ya 1983 ya Eyes That See in the Dark iliandikwa na bendi ya The Bee Gees huku Barry akiwa ndo mzalishaji, albamu hii iliingia kwenye albamu bora 10 ndani ya Marekani na kupewa Double Platinum certification. Hapo ikaonesha kuwa The Bee Gees ni kama maji, usipokunywa basi utayaoga! Usipowasikiliza wakiimba basi utasikiliza mashairi yao matamu kama Asali. 1983 The Bee Gees walipata mafanikio kupitia wimbo uliotumika kuitambulisha filamu ya Staying Alive ambayo ilikuwa ni muendelezo wa Saturday Night Fever, wmbo huu ulipewa platinum certification ndani ya Marekani na huku wimbo wao wa "The Woman in You"ukiingia kwenye chart za nyimbo bora 30.
gees.jpg

1983 kulitokea sitofahamu mara baada ya Ronald Selle kudai kuwa The Bee Gees waliiba ala ya muziki kutoka moja ya nyimbo yake ya "Let It End", ambapo The Bee Gees walitumia ala hiyo kwenye wimbo wa "How Deep Is Your Love", The Bee Gees kwa kukosa mtaalamu wa masuala ya muziki walishindwa kesi, ingawa miezi michache baadaye Mahakama iliwapatia haki The Bee Gees kuwa hawakufanya wizi wa aina yoyote.
8d538092fafa959f6b06b586ade66b16.jpg

Agosti 1983 Barry alitia saini na kuingia makubaliano MCA Records na kutumia miezi ya mwisho wa 1983 pamoja na 1984 kuandika nyimbo kwa ajili ya albamu yake ya Now Voyager, huku Robin aliachia Albamu zake tatu binafsi ndani ya miaka ya 1980, How Old Are You?, Secret Agent pamoja na Walls Have Eyes. Maurice aliachia albamu yake ya pili, "Hold Her in Your Hand" baada ya ile ya mwanzo kuachiwa 1970.
54-Diana-Ross-1200x834.jpg

1985, Diana Ross aliachia albamu yake ya "Hold Her in Your Hand" albamu ambayo nyimbo zake zote ziliandikwa na the Bee Gees huku wimbo mkuu ukiandikwa na Michael Jackson, albamu hii ilizalishwa na Barry huku wimbo wa "Chain Reaction" ukimpatia nafasi kubwa sana Diana Ross ya kuingia kwenye chart za Uingereza na Australia kwa kuwa namba moja.

1987 The Bee Gees waliachia albamu yao ya E.S.P ambayo iliuza nakala zaidi ya milioni 2, hii ilikuwa ni albamu yao ya pamoja kwa zaidi ya miaka sita, na pia ikawa albamu yao ya kwanza wakiwa na Warner Bros. wimbo wa "You Win Again" ilishika namba moja kwenye chart za Uingereza, Uholanzi, na nchi nyingine nyingi za Ulaya. Hii ikawa ni heshima tosha kwamba The Bee Gees ndo bendi ya kwanza na pekee kuwa na nyimbo zilizoshika namba moja kwenye chart za Uingereza katika miongo mitatu tofauti, 1960, 1970, pamoja na 1980. Wimbo huu haukupata mafanikio ndani ya Marekani kwani ulishika namba 75 na The Bee Gees walitoa dukuduku lao kuhusu vituo vya redio vya Marekani. Ingawa wimbo huu uliwafanya The Bee Gees kushinda tunzo ya Ivor Novello Award for Best Song Musically and Lyrically katika tunzo za British Academy za 1987 huku Februari wakipata kutajwa kuingia kwenye tunzo za Brit Award katika kipengele cha Best British Group.

the-bee-gees-would-argue-constantly-during-recording-sessions-says-new-book-01.jpg

The Bee Gees waliungana na Eric Clapton kuunda kundi la 'the Bunburys' kwa ajili ya kuchangisha fedha kwa ajili ya wahitaji ndani ya Uingereza, katika kundi hili walirekodi nyimbo tatu, "We're the Bunburys", "Bunbury Afternoon", pamoja na "Fight (No Matter How Long)" ambapo wimbo huu ulishika namba nane kwenye chart za muziki wa rock pamoja na kuwa miongoni mwa nyimbo katika albamu ya Michuano ya Olympics ya majira ya joto ya 1988.

1989 The Bee Gees walitoa albamu yao kwa jina la One huku kukiwa na wimbo maalumu, "Wish You Were Here", ambao ulikuwa ni kwa ajili ya kaka yao, Andy ambaye alifariki dunia 1988 kutokana na maambukizi ya ugonjwa wa myocarditis, waliimba wimbo huu kwa hisia na huzuni sana. Baada ya kutoa labmu hii walifanya ziara yao ya kimuziki ikiwa ni zaidi ya miaka 10 ya kutokufanya ziara yoyote.

Huko Uingereza Polydor walitengeneza mkusanyiko wa vyuma vizito kutoka kwenye nyimbo bora za the Bee Gees, nyimbo ambazo zilitikisa chart za Uingereza, kupitia mkusanyiko wa nyimbo hizi walipata umaarufu mkubwa sana, huku albamu hii ikipata Triple Platinum certification (Hatari sana hii)

maxresdefault (1).jpg

High Civilization ikafuatia 1991 ambayo ndani yake kulikuwa na chuma kizito sana cha "Secret Love", ambacho kiliingia kwenye top 5 ya nyimbo bora za Uingereza, punde tu baada ya kuachia albamu hii the Bee Gees walienda kwenye ziara ya kimuziki wakizunguka Ulaya, na baada ya kumaliza ziara, Barry Gibb alianza kupatwa na matatizo ya mgongo, tatizo ambalo lilihitaji kufanyiwa upasuaji, afya yake ilianza kuzorota na ilitia shaka kama angeweza kuendela kufanya shughuli za kimuziki tena. Mdogo wake, Maurice akaanza kupiga pombe kama sharubati vile kiasi ikahitajika kupatiwa msaada wa rehab.

1993, the Bee Gees walirudi kwenye record label yao ya Polydor na kuachia albamu ya Size Isn't Everything ambayo pia ndani yake kulikuwa na chuma kizito cha "For Whom the Bell Tolls" ambacho kiliingia kwenye chart ya nyimbo tano bora Uingereza, huku Marekani mambo yakiwa magumu kwani wimbo wa "Paying the Price of Love" ukifanikiwa kufika amba 74 tu, jambo ambalo liliwaumiza sana the Bee Gees

403d02-20130806-bee-gees.jpg

1997 waliachia albamu ya Still Waters ambayo ilishika namba mbili kwenye chart Uingereza ikiwa ni nafasi ya juu zaidi kuwahi kushika tokea 1979, kwa Marekani ilishika namba 11, wimbo wa kwanza katika albamu hii, "Alone" ulitosha kuwapa heshima nyingine kwani uliingia kwenye nyimbo 5 bora Uingereza na moja ya nyimbo bora kwenye chart ya nyimbo 30 Marekani.

1997 kwenye tunzo za BRIT zilizofanyika London bendi y
a the Bee Gees ilishinda tunzo ya Outstanding Contribution to Music, Novemba 14 1997 walifanya onyesho lao mubashara pale Las Vegas onyesho ambalo lilipewa jina la One Night Only. Katika onyesho hilo waliimba wimbo wa "Our Love (Don't Throw It All Away)" ambapo kulikuwa na sauti ya marehemu kaka yao Andy huku pia Celine Dion akiimba wimbo wake wa "Immortality". Ni katika onyesho hili ndipo walipotangaza kuwa kutokana na kuzorota kwa afya ya Barry basi hilo ndo onyesho la mwisho kama The Bee Gees, na machozi ya mashabiki siku ile yalitosha kumfanya Barry aone kuwa bado ana deni kubwa katika talanta yake ya muziki, na hapo ndipo kukazaliwa wazo la kuwepo kwa ziara ya muziki duniani yenye jina la "One Night Only".

Watu zaidi ya elfu 56 wakiwa kwenye Uwanja wa Wembley Septemba 5 1998 walifika kutazama maajabu ya bendi ya The Bee Gees, kisha watu zaidi ya elfu 72 walioingia kwenye Uwanja wa Olympic Stadium pale Sydney Australia walifurahia burudani ya kukata na shoka. Usiku wa kukaribisha Milenium mpya yaani Disemba 31 1999 The Bee gees walifanya onyesho lao la mwisho lililopewa jina la BG2K.

View-of-audience-and-stage-at-Queen-Live-Aid-1985-Wembley-UK-Note-the-relatively-small.png

2001 The Bee Gees waliachia albaum ambayo ilionekana kuwa ni albamu ya mwisho, This Is Where I Came In, albamu ambao ilikuwa ni ya mafanikio kwani iliingia kwenye chart za nyimbo 10 bora Uingereza na kupewa Gold Certification pmoja na kuingia kwenye orodha ya nyimbo 20 bora Marekani. Onyesho la mwisho la The Bee Gees wakiwa watatu lilikuwa ni kwenye Love and Hope Ball la 2002 huku Maurice akifariki dunia Januari 12 2003 akiwa na miaka 53 mara baada ya kupata mshtuko wa moyo wakati akisubiria kupatia upasuaji wa dharura wa utumbo kujikunja; hata hivyo Kaka zake walikubali kuendelea kutumia jina la The Bee Geeskwa heshima ya Maurice ila muda kidogo waliona ni vyema kuacha kutumia jina hili la The Bee Gees kwani lilikuwa likiwakilisha kaka watatu na sasa wamebaki wawili.
licensed-image.jpg

Wiki ambayo Maurice alifariki dunia, Robin aliachia albamu yake ya Magnet, na Februari 23 2003 The Bee Gees walitunukiwa tunzo ya Grammy Legend Award na kuwa watu wa kwanza kabsa kwa karne ya 21 kupata tunzo hiyo kubwa ya mafanikio, kwa majonzi makubwa Barry na Robin pamoja na mtoto wa Maurice, Adam walipokea tunzo hiyo. Mei 2 2004 Barry pamoja na Robin Gibb walipokea nishani ya CBE huku mpwa wao Adam akipokea nishani kwa niaba ya baba yake.

Mwishoni mwa 2004 Robin alianza ziara yake ya muziki Ujerumani, Urusi na mataifa ya Asia huku Januari 2005 yeye, Barry pamoja na wasanii wengine wa Rock walirekodi na kuimba wimbo wa "Grief Never Grows Old", kwa ajili ya kuwatia moyo waathirika wa Tsunami wakiwa pamoja na Kamati ya Maafa na Majanga. 2006, Barry aliungana tena na Barbra Streisand katika albamu yake ya Guilty Pleasures, ambayo ilifanya vizuri sana. 2004 Barry alishirikiana na Cliff Richard kurekodi wimbo wa "I Cannot Give You My Love" wimbo ambao ulibamba sana kwa kuingia kwenye orodha ya nyimbo bora 20 Uingereza huku ala ya muziki iliyotumika kwenye wimbo huu ilikuwa ni kazi ya Marehemu kaka yake, Maurice.

Grammy_Rewind_Bee_Gees_Hero.jpg

Februari 2006, Barry na Robin waliungana tena kwenye jukwaa moja kwenye onyesho la kuchangia kituo cha Utafiti wa Kisukari, na hii ikawa ni onyesho lao la kwanza la wazi toka Maurice afariki, Machi 14 2009 Barry aliungana na "I Cannot Give You My Love" kutengeneza onyesho bomb asana la saa moja kwenye tamasha lililofanyika katika uwanja wa Sydney Cricket Ground ili kusaidia waathirika na wahanga wa moto wa Victorian Bushfires uliozuka Kusini Mashariki mwa Australia, sehemu ambayo waliwahi kuishi mwanzo kabla ya kurejea Uingereza.

Mwishoni mwa 2009 Barry pamoja na Robin walitangaza kurudi na mpango wa kurekodi na kufanya maonyesho wakiwa kama the Bee Gees, huku wakifanya onyesho kubwa kwenye kituo cha BBC onyesho lililopewa jina la Strictly Come Dancing kisha Novemba 17 2009 walitokea kwenye kituo cha ABC-TV katika kipindi cha Dancing with the Stars.

robin-gee.jpg

Novemba 20 2011 ilitangazwa kuwa Robin mwenye miaka 61 amekutwa na Saratani ya ini, tatizo ambalo amekuwa akilifahamu miezi michache tu, alianza kukoda sana na alikata kufaya baadhi ya mahojiano kwa sababu ya maumivu. Aprili 14 2012 Robin alikutwa na homa ya mapafu na kuingia kwenye coma, April 20 alitoka kwenye coma lakini afya yake iliendela kuwa maya Mei 20 2012 alifarii dunia kutokana na ini na bandama kushindwa kufanya kazi. The Bee Gees ikawa imebakia na mtu mmoja tu Barry.
the-bee-gees-would-argue-constantly-during-recording-sessions-says-new-book-01.jpg

Septemba na Oktoba 2013 kwa machungu sana Barry alifanya ziara yake kwa heshima ya kaka zake Maurice na Robin. Warnr Bros walitoa hifadhi yao kwa 2014 ambayo ilipewa jina la The Warner Bros Years: 1987–1991 ambayo ndani yake ilikuwa na ile albamu matata ya E.S.P, One pamoja na High Civilization; huku pia kukiwa na maonyesho yote waliyofanya 1989 huko Melbourne, Australia, Disemba 19 2014 Makala maalumu kuhusu bendi hii iliyoitwa The Joy of the Bee Gees ilionyeshwa BBC Four.
The_Beatles_BBC_Mark_Colleen_Hayward_Referns_Getty_Images.jpg

Ukiachana na the Beatles basi The Bee Gees walikuwa ni moto fire, kuanzia uandishi wa tenzi na mashairi yao ilikuwa ni kusikiliza moyo ukizungumza katika redio, nimepata kusikiliza nyimbo za the Everly Brothers na kuukubali uwezo wao ila wanaokuja kulinganishwa na The Bee Gees hapo wanakaa pembeni kabsa. Wapo wahenga watakaodai kuwa the Mills Brothers walikuwa ni moto, ni kweli kabsa ila binafsi ukiacha na the Beatles pamoja na the Rolling Stones basi The Bee Gees walikuwa wanafahamu kuwavuruga mashabiki kwa mahaba ya muziki wao. Paul Gambaccini pamoja na Gavin DeGraw wanafahamu mchango na ukubwa wa madini ambayo The Bee Gees walipata kuyaweka kwenye nyimbo zao. Sio kazi rahisi hata kidogo kuwa na vyuma 13 kwenye orodha ya nyimbo 100 huku ukiwa na vyuma 12 kwenye orodha ya nyimbo 40! Ni Impossible!
Asante sana The Bee Gees, Staying Alive! Ahh Ahh Ahh Staying Alive! Staying Alive! Ahh Ahh!

Mpaka wakati mwingine! Kaa tayari kwa simulizi ya Maisha ya bendi ya
The Sugarhill Gang Kutoka Marekani ambayo inaimba muziki wa hip hop.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom