Anadai ana mimba yangu, kutoa hataki, kulipa kodi hataki, kuhama hataki

Umemlala mama mchungaji wakati si mkeo? Loooh tunaelekea wapi sijui!
Mambo yameivaaaaaaa........
Polisi mwenyewe, jambazi mwenyewe, hakimu mwenyewe, mfungwa mwenyewe askari magereza mwenyewe.
Kweli waliosema akili nyingi huondoa maarifa hawakukosea.
Screenshot_20210907-172551_Chrome.jpg
 
Nina kajinyumba kangu kadogo kakushikia kiwanja Goba kunguru, kana vyumba viwili vya kulala, sebule, chumba kimoja kina choo na bafu ndani na pia kina choo cha wageni jirani na sebuleni.

Yaliyonikuta najuta kuzaliwa jamani, natamani nilie, kilio hakitoki, natatamani niende kwa Mwamposa nikanywe lori zima la maji ya upako, na nikitoka huko niende kwa Sharifu Majini, maana mambo yamenifika pabaya.

Kwenye kajumba kangu haka, kuna jamaa yangu pia ni dalali wa nyumba, nilipokuwa nakamalizia akaniambia kuwa anataka kuniletea mpangaji wa kunilipa laki 4 kwa mwezi, nikacheka kizungu, nikasema mlete fasta asije akalaghaiwa na madalali wenye nyumba za mbavu za mbwa wamuharibu na kunghiribu akili.

Kweli akamleta binti mmoja mkali sana, amemliza chuo, kapata kazi kampuni moja ya fedha hapo Mlimani City. Binti kaja na kibunda chake mkononi, kasema anataka kulipa miezi sita.

Nikakubali, nikabeba mzigo na kuondoka.

Kutokana na usasa wa mifumo ya umeme na maji na ya kiulinzi binti alikuwa akinipigia simu mara kwa mara kuniuliza kile na hiki.

Tukazoeana tukawa tukikutana mara kadhaa mwisho wa wiki, na taratibu taratibu nikajikuta kamoyo kanadondokea upande wa mashariki ya uwanja.

Halaula, mara penzi likawa jau, mambo moto moto, yakaongezeka hadi yakawa mpwitompwito.

Siku zikaenda, binti mwili unabadilika, tumbo linaongezeka, hasemi kuwa ana mimba, mimba ilipofika miezi sita ndio anasema ana ujauzito wangu, kuhama hataki, kutoka hataki, kulipa kodi hataki, anasema hiyo ni nyumba yake yeye na kiumbe wake ajaye.

Jamani, hivi huyu Mpalestina anataka kunipora nyumba hivihivi mchana kweupe, ananionea kwasababu mimi ni msukuma Mshamba...

Sasa hajui, nimeenda kuwatafuta madalali wa kupiga minada nyumba, watangaze na gari yao kuwa hiyo nyumba inadaiwa na benki na Jumamosi ndio mnada wenyewe. Tayari nimesha mseti mnunuzi feki. Kuanzia kesho gari inapita mitaani na maspika jioni mida ambayo amerudi kazini, na mlangoni wataweka notice yao ya mnada.

Jumamosi atake asitake atatoka.

Sanasana atapata grace period ya siku moja tu...

Hiiiiiiiiiiiii baghoshaaaaa
Kodi laki NNE kwa mwezi!!!!! naenda kupata chai ntarudi
 
S

Hiiiiiiiiiiiii baghoshaaaaas
Sasa kama yumo humu si umeliwa popoma🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Umetumia njia mbaya Sana ulipaswa kupangisha Tu mtu unasuka mtu WA kuja kupanga harafu wewe unakuja kumhamisha na kumpangishia nyumba nyingine bila yeye kuwepo unakodi Gari unamfuata Kwa mbwembwe zote unampeleka kwenye nyumba ulohamishia vitu, atalia wee atatulia huko nyumba unepangisha mtu . Akiuliza unamwambia ni Kwa ajiri ya matumizi yake maana pango lake ni pesa kidogo Kwa hiyo ukilipwa kule unalipia pango lake na chenchi inabaki yake ya matumizi

Fitina kwishinia kama kweli mtoto ni wako akizaliwa fanya mpango sasa maana siku hizi kubambikiwa ni normal
 
Back
Top Bottom