Ana kwa ana na Mwigulu Nchemba: Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020

Mwigulu Nchemba aliwahi kukiri na kudai siku Mh. Tundu Antiphas Lissu anamiminiwa risasi za kuweza kumwangusha tembo, alipigiwa simu!


Sawa, siku hiyo Mbunge mwenzake anamiminiwa risasi alipigiwa simu, sasa yapo maswali yanayohitaji majibu pia...
  • Je siku Clouds FM inavamiwa na majambazi yenye silaha usiku wa manane pia alipigiwa simu?
  • Je siku Waziri mwenzake.Nape Nnauye, anatolewa bastola hadharani mchana kweupe alipigiwa simu?
  • Je siku mwanaharakati, Ben Saanane, anapotezwa alipigiwa simu?
  • Je siku mwandishi Azory Gwanda anatekwa na kupotea alipigiwa simu?
  • Je siku mwana muziki Roma na wenzake wanatekwa alipigiwa simu?
  • Je siku maiti zinaokotwa ufukweni mwa bahari kwenye viroba alipigiwa simu?
 
Write your reply...Dah cheo dhamana na dunia hadaa. Mungu yu macho siku zote na kila goti litapigwa, ni suala la muda tu.
 
Wewe ni nani?
Una mchango gani wa kushikika kea taifa letu....
Wewe mzalendo...
.?
Kuna mtu ametupia uzi kuwa siku hizi sivai skafu, huu ni mkutano mkuu wa juzi tarehe 19/2/2020 wakati wa ziara ya mzee Mangula. Skafu nilikuwa navaa hata kabla ya kwenda Ilboru Sekondari haikuwa sare ya Uwaziri.

View attachment 1365715

Kama kuna maswali kunihusu, nitayajibu hapahapa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mtu ametupia uzi kuwa siku hizi sivai skafu, huu ni mkutano mkuu wa juzi tarehe 19/2/2020 wakati wa ziara ya mzee Mangula. Skafu nilikuwa navaa hata kabla ya kwenda Ilboru Sekondari haikuwa sare ya Uwaziri.

View attachment 1365715

Kama kuna maswali kunihusu, nitayajibu hapahapa
Toilet paper Ikishatumika hutupwa.
Mwigulu umeshatumika na umetupwa.

Naamini unasubiri kwa matumaini kufanyiwa recycling kwa matumizi mengine huko mbeleni.

Maana huna akili ya kukuwezesha kumudu maisha nje ya siasa.

Kimsingi katika uongozi wako hakuna mchango significant unaoweza kudhihirisha wewe kufaa kupewa tena dhamana ya kuongoza.

Umeamua kujikomba na kujipendekeza ili upate tena kibali cha kuaminiwa na watawala. (Siyo sifa nzuri kwa Msomi).

Life goes on.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huna taarifa hata kidogo, fuatilia upate ukweli ndio uje uandike. Kama kawaida nadhani unatamani niishi kama mbwa koko. nikuhaikikishie watafute wenye taarifa wakwambie nani aliwasaidia walipokuwa na matatizo
Inaonekana hapa kuna ukweli,na kunauwezekano mkubwa sababu mojawapo ya kukuondoa kwenye nafasi yako ya uwaziri wa mambo ya ndani inaweza ikawa ni hii ya kuwasaidia wapinzani ambao ni wakosoaji wa serekali,japo kuwa hili halisemwi lakini ukifuatilia hakuna sababu yoyote ya maana inayoelezwa ya kukuondoa kwenye nafasi yako.

Kwani kwa uhalisia kabisa nchi kama taifa tumefika mahali ambapo baadhi ya watawala wanaona ni halali kabisa kuwatesa na kuwapiga risasi raia ambao wanatofautiana nao kimtazamo.

Na ukijaribu kuwasaidia na kuwahoji wahusika kwanini wanafanya hivyo,unahesabiwa kuwa na wewe ni mmoja wao uliyekosa uzalendo, mwenye kutumika na mabeberu na zawadi yako ni kama hili lililokupata.

Pia yapo mengine yanayoendelea hivi sasa ya kuwahoji akina Membe, Kinana, Makamba yote hayo yako kwenye mrolongo uleule kuwa kuna watu ambao wamejipachika cheo cha miungu watu hawakosei na hawataki kukosolewa,ukijaribu kuwakirisha mawazo yako yanayokinzana nao ndipo yanapokupata kama hayo.

Hata hawa wanaohojiwa ni kwakuwa tu wanaonewa aibu kwa kuwa ni watu waliotoka mbali na train, na hawa wengine wanaojifanya kuwahoji ni kama vile wadandiaji wa train waliokuta tayari train ilishaanza safari,hiki cha ukongwe ndicho kinacho wafanya waendelee kupumua mpaka sasa.

Tofauti na hapo,wangekuwa wameokotwa msitu wa pande na kwenye viroba,wakihurumiwa sana wangefunguliwa kesi za uhujumu uchumi na kesi maarufu ya sasa ya kutakatisha pesa.
 
OK, but kwa phD uliyo nayo, na research nyingi ulizo fanya. Je ili swala unalichukuaje ki mantiki kama msomi usiseme ni Tatizo kubwa wakti wew umesoma uchumi na umefanya kazi BOT kama mshari was uchumi. Tupe technique issues za kujikwamuwa mkuu,.
Yes, HILI NI TATIZO, HII NI HOJA YA MSINGI.

Tar 20 tulikuwa na mjadala mpana SINGIDA, TATIZO HILI LINAWEZA KUPUNGUA KWA KUWEKEZA KWENYE MODERNIZATION OF PRODUCTION PRICESS MIKOANI KWETU, ILI SHUGHULI ZA UZALISHAJI ZITOE FAIDA ZINAZOLIPA HIVYO ZITENGENEZE AJIRA. HIVYO TULIKUWA NA RCC. TULICHAKATA SANA.

BUT AJIRA NI TATIZO NA NI MADA PANA SANA, HAINA JIBU MOJA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom