Ana kwa ana na Mwigulu Nchemba: Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020

Kuna mtu ametupia uzi kuwa siku hizi sivai skafu, huu ni mkutano mkuu wa juzi tarehe 19/2/2020 wakati wa ziara ya mzee Mangula. Skafu nilikuwa navaa hata kabla ya kwenda Ilboru Sekondari haikuwa sare ya Uwaziri.

View attachment 1365715

Kama kuna maswali kunihusu, nitayajibu hapahapa
Maswali yangu Kwako ni mawili tu nayo ni......

1. Lini utaacha kuwa Mnafiki na Ndumilakuwili?
2. Lini utaacha Kujipendekeza kulikopitiliza kwa Mwenyekiti wako Taifa na Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli?

Nitashukuru sana kama utanijibu nami Mdau wako.
 
Mkuu samahani kama nimekukwaza, lakini kutoa tu support kujenga nyumba ya Bwana kunamzuiaje mtu kutubu dhambi zake (kama anazo)? Tafadhali hata wasiomjua Mungu wanaweza kutumiwa kujenga ufalme, karibu na wewe mkuu wangu tusaidiane kuujenga ufalme.
Wewe kweli Ni mchumia tumbo. Yaani unataka kulitumia Neno kujinufaisha kwa kisingizio cha 'kujenga ufalme!!?' Hivi unakumbuka wale akina Sanbalat na Tobia walitaka washirikishwe kwenye ujenzi kule Yerusalemu, Ezra na Nehemia waliwajibu nini!!? Hawana sehemu katika kazi ile!!!
Hawa akina Mwigulu Ni watu wa hila ambao bila toba hawatakiwi kukanyaja hata ua wa pepo.
Jee unajua ni kwasababu gani alitumbuliwa?.
Mambo mengine acheni!, hata ikitokea Mungu akampenda zaidi na akamuita KWAKE leo, Mwigulu anakwenda straight peponi, zipo taarifa kuwa wakati akiwa waziri, Mwigulu alibatizwa, na ubatizo ni kumkataa shetani na mambo yake yote aliyakataa!.
P
Sasa P, Mbona Mwigulu ameanza Tena kujipendekeza kwa Shetani yuleyule, au leo Shetani yule kabadilika na kuwa malaika Gabrieli!!!?
 
URAIS SIO NDOTO ZA MTU BALI NI HITAJI LA WAKATI NA HITAJI LA WATU . HIVYO HII SIO AGENDA KWA SASA. NIULIZE KUHUSU IRAMBA
Mbona Iramba ndo Swali la msingi mzee? Kama Hilo lingine la URAIS ni la kizushi tu.

NB: Binafsi nakumbuka nilishawahi kutoa taarifa za pira la polisi kutumika kubebea beer za maaskari kuendeshea biashara Binafsi huko Tandahimba Mtwara kiasi kwamba Kuna siku iliwahi kusababisha ajali. Hukuwahi kutoa neno.
Sijaona haja ya kupinga ukweli unaoambiwa na wapiga kura wako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"P Mkuu P, somo la Karma ni pana sana.
Karma haijitokezi kama watu wanavyotarajia, hujitokeza kwa namna nyingi na tofauti sana.
Mfano 1: Marekani mtu aliua mkewe na kumzika uani. Imepita miaka zaidi ya 20 hakuna aliyejua nini kilitokea.
Nyumba imeuzwa, mnunuzi akaamua kuchimba uani katika kutengeneza na kuimarisha nyumba yake.
Alikutana na mabaki ya marehemu, uchunguzi ukabaini mumewe alimuua. Karma ikajitokeza jamaa kanaswa.
Mkuu Nguruvi 3, kwanza ni kweli karma haijitokezi direct pale kwa pale na sometimes wewe unaweza kutenda maovu na ukafa vizuri bila kufidia, lakini kikaja kulipa kizazi chako hadi cha 4!, 4th generation!.
Kwa huyo mtu aliyeua mkewe, hakuna mtu aliyekuwa ana keep track aliishi maisha gazi hiyo miaka 20, take it from me, his life was a living hell!, sio watu wote wamejaaliwa kuona ndani ya mioyo ya watu, lakini mimi nawafahamu matajiri wengi tuu, wana furaha machoni lakini huzuni moyoni, hata smile zao, cheka zao ni just superficial, wana kila kitu and yet they are living hell!.
Mfano 2. Same Kilimanjaro kuna tukio la mtu aliyepotea baada ya kuchukua mafao yake.
Mkewe alipofariki akataka azikwe eneo X. Wakachimba pale pale mumewe alipozikwa.
Ikabainika aliyetenda unyama ni mwanae miaka zaidi ya 10.
Mama kutaka azikwe eneo X ilikuwa ni 'Karma' ili mwanae inamrudi leo hii.
Hapa nikama tukio la kwanza, hakuna mtu aliye keep track ya maisha ya huyo kijana katika miaka hiyo 10 baada ya kuua baba yake!. He was living hell!.
Hakuna aliyeuliza kwa mama why alichagua azikwe pale?, kupitia life after life, baba kule alipozikwa alimtokea mama ndotoni akamuamsha na kumpeleka kwa astral travel, mama akaona baba alipo, mama akaelekeza nikifa nizikwe pale, baba akamuita mama aje, akaitika, akaenda, wao wakaendelea na mapenzi yao kwenye ulimwengu wa roho.

Mfano 3; Marekani kuna wimbi la askari kupata matatizo wakiyaita PSTD(Post stress traumatic disorder)
Idadi ya askari wanaojiua kila siku inaongezeka na hata kuwa ''janga''. Je, hii si karma ? Amri halali ndiyo subject hapa.Vitani ni amri halali.
Miaka yangu, ulikuwa ukimaliza A level unakwenda JKT kwa mujibu wa sheria, mimi nilikuwa bingwa wa paredi na shabaha, nikachaguliwa moja kwa moja kujinga na JWTZ straight from JKT, hivyo nikapiga deppo mpya ya JW pale Airwing kabla ya kwenda Cadet Monduli, sasa kwenye somo la mbinu za medani, kuna kitu kinachoitwa "initiative", mkishambuliwa, mkijikuta wenzako wameumia sana, huwezi kusaidia na unatakiwa ku retreat, au atakufa kwa mateso, unatakiwa wewe kuwaalizia bila huruma ili kuwapunguzia mateso, askari wote wanaofanya mauaji ya kikatili hiyo au hata kushuhudia tuu ukatili wa ajabu, ndio huja kupata PSTD, hiyo sio karma bali ni guilt conscious.

Ukiua vitani vifo halali hakuna karma, ila kuna wale wanaovamia kijiji, wana ua wanaume wote, wana rape wanawake kisha kuwaua, kisha wanamalizia kuua vitoto, ili visiteseke, kwenye vita vya Kagera, majeshi yetu pia yalifanya unyama huo Uganda, Generali Ernest Mwita Kiaro, wakati huo akiwa Major General, alikuokoa kitoto kimoja cha Kiganda baada ya wazazi wake kuuliwa na kikosi chake, askari wake wakataka kukimalizia, akatoa amri ya stop, akakichukua kitoto kile na kukipeleka kwake.

Akakipa jina na kutumia ubini wake, amini usiamini, kilikuja kuwa a very rich guy in town, kimemuoa mtoto wa rais, kina roho nzuri hakuna mfano!. Marwa akabarikiwa hadi kuwa CDF na ni darasa la 8 tuu la mkoloni!.
Mnyongaji anatenda kwa amri halali tena mchana kweupe baada ya process nzima ya uhalali kufanyika.
Wanaokabiliwa na adhabu ya kunyongwa kamwe hawalaumu wanaotimiza wajibu.Ni amri halali.
Swali, amri halali mipaka yake ni ipi?

Kuna sababu inaitwa halali, kwa maana imepitia hatua halali, imeelezwa kihalali, imeidhinishwa kihalali.
Hata vitani kuna kitu kinaitwa ''rule of engagement' kwamba, kuna abcd za kufanya na kutofanya.
Uwepo wa 'rule of engagement' unalenga kuhakikisha askari wanatimiza amri halali kama ilivyoelezwa.
Kwahiyo amri halali ina namna zake na mipaka yake si ''open season''
Amri halali ni amri yoyote unayopewa na mkubwa wako, kijeshi usihoji. Kwenye ile idara ya wale jamaa zetu, kuna kitengo kabisa cha covet operations, kinafanya eliminations na kina ma snipers wenye shabaha ajabu, ndio maana nikasema kama wangekuwa ni wale jamaa zetu kwenye tukio la Lissu, wasinge fanya such mercy dirty job!, they have 100 ways plus za kufanya a clean job hata accident look a like na watu wasijue!. Hili nimelieleza vizuri hapa

Mkuu P huku mitaani watu hujitoa katika baadhi ya maamuzi ya Familia au Ndugu yenye utata.
Kauli kubwa unayoisikia ni moja '' wana nawa mikono yao'', kwa maana wanajiepusha na ''karma''
Hoja yangu hapa ni maoni tu ya jumla juu ya Karma. Hailengi kuhusu tukio au watu kwa namna yoyote
Its true watu wengi hujitoa kwa kunawa mikono kuepuka karma, hata Pilato alinawa mikono kabla ya kumhukumu YESU hii haiondoi karma!, pia nilishikwa sikio, kuna mtu alisulubiwa kwasabu ya kunawa mikono kwa tukio la Lissu, naomba msiniulize nani!.
P
 
Sikuwahi kuandika, hata sijui wapi na wapi pameandikwa. Maana ilikuwa kazi ya mashabiki. Tufute tu maana swala la USAFI WA MAZINGIRA NI LETU SOTE
Hayo maandiko ya herufi kubwa yananikumbusha SUALA LA KULINDA KATIBA NI LETU SOTE! Kiongozi hii ni plagiarism au?
 
Bila bila,
Nitafute nikufafanulie maana inaonekana HUJUI KABISA
Kiongozi umesema utajibu maswali sasa haya mambo ya kusema mara nitafute nikujibu yanatoka wapi? Jibu kwa faida ya wana JF wote hapa jamvini na siyo unaulizwa swali unasema nitafute pembeni. Wangapi unataka tukutafute pembeni? Weka majibu hapa mambo yaishe.
 
Jee unajua ni kwasababu gani alitumbuliwa?.
Mambo mengine acheni!, hata ikitokea Mungu akampenda zaidi na akamuita KWAKE leo, Mwigulu anakwenda straight peponi, zipo taarifa kuwa wakati akiwa waziri, Mwigulu alibatizwa, na ubatizo ni kumkataa shetani na mambo yake yote aliyakataa!.
P
Mkuu pascal mayala una uhakika gani kwamba anaenda peponi? Unafanya kazi kuume kwa Mungu Baba? Wewe ndio mwandishi kwenye kitabu cha Uzima? Nenda taratibu acha shiriki.
 
Mwigulu Nchemba, huyu mhanga wa tindikali, Musa Tesha, uliyekuwa ukimtumia kujinadi kwa wananchi, hivi sasa yuko wapi?
Je waliohusika, uliokuwa ukidai ni wanaChadema, walipatikana?
Mwigulu.Musa.gif


Mwigulu.tesha.jpg
 
Utafutwe umfafanulie vipi??lengo lako nini kusema ulizwe na utatoa ushirikiano??nimeona maswali mengi konki logic unayakwepa ila wakijinga jinga ya skafu unajibu fasta balaaa ucpime yaani....wakina ben, azory wanajulikana jinsi walivyotoweka na maiti zile za waamiaji haramu

(uwongo Maiti za operation kibiti na ndo kilichomponza azory gwanda....msituzuge bana mimi ni mmoja wa askari waliokuepo kwenye operation ya kibiti najua kilichotokea kiukweli mwiguli damu zile hazitakuacha salama na hauna amani kwa lile coz I know ur a Christian. though huwezi kukiri apa ila nafsi ako inamajuto balaaa
Bila bila,
Nitafute nikufafanulie maana inaonekana HUJUI KABISA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
P. Nakuona unavyompaka mafuta kwa mgongo wa chupa !!. Unadhani amri hizo zilitolewa na nani na kwa faida gani ?!. Imefikia Leo Tanganyika tunanyooshewa vidole, kwa kuacha kuheshimu haki za binaadamu, na kwa sababu za amri za hovyo kama hizo

Mwigulu alikubali kutumika, acha aione taswira yake watu wanavyomchukulia mitaani

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi Ni Sheria gani anayoisema Pascal Mayalla kuwa inampa Haki aliyeagizwa kumwaga on the line of duty?

Anamaanisha Tanzania Kuna Sheria inayomruhusu mtu kutekeleza umwagaji wa damu bila hatia mbele ya mahakama kwa sababu ameagizwa?

Mi huyu mwandishi sijawahi kumuelewa kwa kweli pamoja kujikuta mjuaji sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jee unajua ni kwasababu gani alitumbuliwa?.
Mambo mengine acheni!, hata ikitokea Mungu akampenda zaidi na akamuita KWAKE leo, Mwigulu anakwenda straight peponi, zipo taarifa kuwa wakati akiwa waziri, Mwigulu alibatizwa, na ubatizo ni kumkataa shetani na mambo yake yote aliyakataa!.
P
Hata bashite kabatizwa na kwa maoni yako atakwenda straight peponi maana hata machozi huwa anayamwaga mazabauni..

Pascal bhana daaah..

Kuna wakati mkoa flani nilikuwa nafanya kazi na waandishi mkoa flani kwa kweli niliwajua kinagaubaga. Mwandishi as long as amenufaika kwa bahasha kupitia kwako anakuwa tayari kukupamba katika kila Hali hata ya kumdhalilisha..

so itoshe kusema hii Ni taswira mbaya mno kwa tasnia hii ya uandishi kwa hapa kwetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi huyu mwandishi sijawahi kumuelewa kwa kweli pamoja kujikuta mjuaji sana
Sent using Jamii Forums mobile app
Huhitaji kumwelewa mtu, bali ni kiwango chako cha uelewa, nimesema unajua wale "jamaa zetu" wana kitengo kabisa cha covet operations na wana ma snipers?.
Kama hujui maana ya covert operation, mtafute huyu jamaa, ni kijana wao, umuulize akuelimishe ili na wewe uweze kuelewa, ila kwa kukusaidia tuu
Serikali zote za dunia nzima, kiusalama
  1. Zina dukukua mawasiliano ya simu
  2. Zina fungua barua
  3. Zina intercept e mails
  4. Zina trail watu 24/7
  5. Zikijiridhisha ni threat to national security, zina ku...kabla hujaleta maangamizi ya kuhatarisha usalama wa taifa!.
Muulize huyu jamaa atakusaidia
P
 
Wanabodi, Hakuna mwanzo usiokuwa na mwisho na mwisho usiokuwa na mwanzo, Mwigulu Nchemba sasa ameshafika mwisho wake wa safari hajui ashike kipi na ajisafishe vipi

Kauli ya Pompeo kuwa wanaushahidi wa kutosha kwa matukio ya watu kunyima Wengine uhai ndio lililomuibua huyu mheshimiwa hapa Jukwaani JF

Asilimia kubwa ya maswali aliyoulizwa na wana JF baada ya yeye kuibuka na uzi wa kwanini siku hizi havai skafu au nguo za Field marshal ameshindwa kujibu, Ameomba watu waongee pembeni awaelimishe kwanini watu walipotea yeye akiwa Msimamizi na Waziri

Mwigulu hakutegemea kwa muda aliojificha na kukaa kimya kuwa watu bado wanamkumbuka kwa ukatili wake hivyo ameshuhudia kundi kubwa ambalo lipo tayari kutoa ushahidi mahakama ya uharifu na haki za binadamu

Mwigulu Nchemba ameamua kuja kupima upepo hapa JF, amejawa na hofu kwa tuhuma za watu kuokotwa mizoga, Watu kupotezwa

Matendo yote machafu yalifanyika Yeye alikuwa Waziri na baadhi ya watu kukutwa kwenye viroba aliyatolea ufafanuzi kuwa vile viroba vilivyowekwa miili ya watu ni wahamiaji haramu

Intelijensia na Rada za Marekani tayari wana mafaili ya mawasiliano na majadiliano ya baadhi ya watu wanaohusika na kunyima wengine haki ya kuishi

Ni suala la muda na wakati tu Mwigulu Nchemba hawezi kukwepa mahakama ya uharifu dhidi ya haki za binadamu aidha kama shahidi au mtuhumiwa

Mtu mwenye PhD kama yeye kuanzisha uzi wa kitoto wa kuvaa skafu au kutokuvaa skafu ni kuweweseka, Na bado atakuja hapa Jukwaani kuanza kujadili mambo ambayo yatamvua nguo kabisa

Suala la kutoa Camera aliposhambuliwa Tundu lissu litazidi kumtesa Katika hatua zake kuelekea mahakama ya uharifu, Nani alitoa order za kung'oa Camera?

Mtu smart na mwenye busara angeamua kuanza kutubu ili kuiweka roho yake huru

Mambo yote ya kikatili na kumwaga damu yalitokea yeye akiwa Waziri mwenye dhamana
 
GUSSIE,
Marekani imesema kuwa ina ushahidi "full" ya yanayotokea nchini Tanzania kuthibitisha madai yao kuwa watu "wananyimwa" haki za kuishi nchini mwetu

Marekani ni Taifa kubwa na hawafanyi mambo yao kwa kubahatisha, wanaposema kuwa wanao ushahidi basi tujue kuwa kweli wanao ushahidi.

Ngoja tusubiri tuone namna Marekani itakavyoanza kuumwaga ushahidi huo na watawala wetu watapopata kiwewe na watakavyotamani ardhi ipasuke ili wajifiche!
 
56 Reactions
Reply
Back
Top Bottom