Ana kwa ana na Mwigulu Nchemba: Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020

Alitakiwa alete ufafanuzi hapahapa.

Kwanini atake ufafanuzi pembeni?

Sent using Jamii Forums mobile app

Si ndio hapo sasa. Kimsingi Mwigulu hana hoja na ni mtu anayeweza kwenda kuhutubia watu wenye uelewa finyu, lakini kwa huku jukwaani kwa watu wenye uelewa mpana amegeuka kituko. Hayo ndio madhara ya kutegemea vyombo vya dola kufanya siasa, siku ukiingia sehemu inayotegemea uwezo unachemsha.
 
Mkuu Freddie Matuja, mpe muda, leo ameshinda humu karibu siku nzima.
P

Humu harudi maana amezoea siasa za mbeleko ya vyombo vya dola. Huku kwenye mijadala huru hana uwezo nayo. Kinachomkimbiza ni jinsi anavyoambiwa ukweli wake kama kiongozi muendesha uovu, hali hiyo inampa wakati mgumu, na hata akirudi ni kuja kujibu hoja nyepesi, maana hata kwenye kampeni huwa hakuna nafasi yeye au wao kuulizwa maswali magumu zaidi ya kuwahubiria watu porojo wazitakazo.
 
Humu harudi maana amezoea siasa za mbeleko ya vyombo vya dola. Huku kwenye mijadala huru hana uwezo nayo. Kinachomkimbiza ni jinsi anavyoambiwa ukweli wake kama kiongozi muendesha uovu, hali hiyo inampa wakati mgumu, na hata akirudi ni kuja kujibu hoja nyepesi, maana hata kwenye kampeni huwa hakuna nafasi yeye au wao kuulizwa maswali magumu zaidi ya kuwahubiria watu porojo wazitakazo.
Tuwe na shukrani katika madogo ili tuweze kupatiwa makubwa, Mhe. Mwigulu leo sio tu kajitokeza bali kajitoa sana, na kajibu maswali mengi na kwa muda mrefu sana, tumshukuru kwa hilo, hayo yaliyobaki atayajibu siku nyingine akipata nafasi.
P
 
Pascal Mayalla, P. Nakuona unavyompaka mafuta kwa mgongo wa chupa !!. Unadhani amri hizo zilitolewa na nani na kwa faida gani ?!. Imefikia Leo Tanganyika tunanyooshewa vidole, kwa kuacha kuheshimu haki za binaadamu, na kwa sababu za amri za hovyo kama hizo

Mwigulu alikubali kutumika, acha aione taswira yake watu wanavyomchukulia mitaani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tuwe na shukrani katika madogo ili tuweze kupatiwa makubwa, Mhe. Mwigulu leo sio tuu kajitokeza bali kajitoa sana, na kajibu maswali mengi na kwa muda mrefu sana, tumshukuru kwa hilo, hayo yaliyobaki atayajibu siku nyingine akipata nafasi.
P

Tunamshukuru kwa lipi boss, kaulizwa maswali mengi ya msingi lakini anayakwepa. Unaposema tumshukuru kwa kujitoa kujibu maswali, mbona kama unamgeuza kuwa Mungu? Paskali umeanza lini kuabudu sanamu? Yeye ni wa kawaida sana japo ww au yeye anadhani ni wa maana sana.

Hadhi yake ingepanda iwapo angejibu maswali ya msingi. Sawa acha tu nikukubalie kuwa acha tumshukuru kwa hayo madogo, lakini nina hakika kupitia uzi huu, amejua kuwa jamii kubwa ya watanzania wanamjua ni mtenda uovu dhidi vya raia wa nchi hii, ajibu asijibu lakini habari ndio hiyo.
 
P. Nakuona unavyompaka mafuta kwa mgongo wa chupa !!. Unadhani amri hizo zilitolewa na nani na kwa faida gani ?!. Imefikia Leo Tanganyika tunanyooshewa vidole, kwa kuacha kuheshimu haki za binaadamu, na kwa sababu za amri za hovyo kama hizo

Mwigulu alikubali kutumika, acha aione taswira yake watu wanavyomchukulia mitaani

Sent using Jamii Forums mobile app
Je, unajua ni kwasababu gani alitumbuliwa?.
Mambo mengine acheni!, hata ikitokea Mungu akampenda zaidi na akamuita KWAKE leo, Mwigulu anakwenda straight peponi, zipo taarifa kuwa wakati akiwa waziri, Mwigulu alibatizwa, na ubatizo ni kumkataa shetani na mambo yake yote aliyakataa!.
P
 
Huna taarifa hata kidogo, fuatilia upate ukweli ndio uje uandike. Kama kawaida nadhani unatamani niishi kama mbwa koko. nikuhaikikishie watafute wenye taarifa wakwambie nani aliwasaidia walipokuwa na matatizo
Wewe mwigulu mpu.mba.vu sana. Msengerema. Ulipopewa kichaka ukajiona. Sasa maisha yako yako mikononi mwa uliowauwa. Upo kwenye mende (kilengeo)

Utajijua tu siku yako, itakuwa afadhari ya Tundu Lissu.

Ulisema una ushahidi duniani na mbinguni

Hiyo mbingu inakusubiri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunamshukuru kwa lipi boss, kaulizwa maswali mengi ya msingi lakini anayakwepa. Unaposema tumshukuru kwa kujitoa kujibu maswali, mbona kama unamgeuza kuwa Mungu? Paskali umeanza lini kuabudu sanamu? Yeye ni wa kawaida sana japo ww au yeye anadhani ni wa maana sana.
Japo humu jf tunatumia hadhi ya kanuni za mwana TANU kuwa binaadamu wote ni sawa na ni ndugu zangu. Lakini kiukweli naamini unajua in reality katika jamii, kuna watu wana hadhi tofauti, Mhe. Mwigulu aliwahi kuwa mgombea urais, mpaka sasa ni mbunge, tuna wabunge wangapi active humu?

Aliwahi kuwa nweka hazina wa CCM, na Naibu Katibu Mkuu CCM Bara, amekuwa naibu Waziri, amekuwa waziri, ni Ph.D holder, alisoma shule ya vichwa Ilboru akatoka na 1 kali O level, akaenda Mazengo akatoka na 1 kali, ajaenda UDSM akapiga 1st Class ya uchumi, akaunganisha masters na kuajiriwa BOT kama mchumi grade 1.

Hivyo huyu sio member wa kawaida ni mtu muhimu na ni mtu wa maana sana, sio sawa na kajamba nani Pasco, hivyo tumheshimu kwa hilo na usimuite sanamu!.
P
 
Vipi suala la uchafuzi wa mazingira ulilofanya la kuchora kwenye mawe, miti, madaraja kwa kuandika MWIGULU RAIS 2015, Unawajibika nalo vipi?
Mwigulu Nchemba
Mbona kama yele maandishi ndio yamependezesha na kuwa kivutio cha scenery seeing, mimi nimekuwa nikisafiri sana terrestrial kabla michoro ile sikuwahi hata ku notice yale majabali, nilikuwa napita nimesinzia, sasa watu tunapita tuko attentive ku notice hivyo kujipatia scenery Tourism ya bure!.
P
 
Pascal Mayalla,
Huyo ni sanamu kama sanamu nyingine, hizo sifa zote unazompaka nazo mafuta kwenye mgongo wa chupa zina nguvu tu hapa Tanzania kwenye nafasi za mbeleko. Angekuwa amewahi kufanya kazi kwenye taasisi ya kimataifa na tukaona uwezo wake kama Mwele Malecela,

angalau huu utetezi wako ungekuwa na nguvu. Lakini sijui amewahi kugombea urais, au kuwa naibu waziri sijui waziri kamili hapa Tanzania ni mtu wa kawaida sana. Hivyo vyeo vyote ulivyotaja kuanzia urais wa nchi hii mpaka vingine, vinahitaji tu mtu mwenye akili timamu. Cheo ambacho JK na Magufuli wameweza nani mwenye akili timamu atashindwa boss?
 
Jee unajua ni kwasababu gani alitumbuliwa?.
Mambo mengine acheni!, hata ikitokea Mungu akampenda zaidi na akamuita KWAKE leo, Mwigulu anakwenda straight peponi, zipo taarifa kuwa wakati akiwa waziri, Mwigulu alibatizwa, na ubatizo ni kumkataa shetani na mambo yake yote aliyakataa!.
P
Ahahahaaaa . P
Straight wapi ?!.

Kwa hiyo kwenye ubatizo alikiri. Na kupelekea kutumbuliwa ?! Daima tenda uwema na ukweli .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"P
ascal Mayalla, post: 34462355, member: 17813"]
Kujua nani kamwaga damu ya nani on a line of duty na kutomtaja, hakupelekei karma yoyote na kujua huko hakumfanyi yeye kuwa responsible or an accessory before the fact or after the fact.
Mkuu P, somo la Karma ni pana sana.

Karma haijitokezi kama watu wanavyotarajia, hujitokeza kwa namna nyingi na tofauti sana.

Mfano 1: Marekani mtu aliua mkewe na kumzika uani. Imepita miaka zaidi ya 20 hakuna aliyejua nini kilitokea.

Nyumba imeuzwa, mnunuzi akaamua kuchimba uani katika kutengeneza na kuimarisha nyumba yake.
Alikutana na mabaki ya marehemu, uchunguzi ukabaini mumewe alimuua. Karma ikajitokeza jamaa kanaswa.

Mfano 2. Same Kilimanjaro kuna tukio la mtu aliyepotea baada ya kuchukua mafao yake.
Mkewe alipofariki akataka azikwe eneo X. Wakachimba pale pale mumewe alipozikwa.

Ikabainika aliyetenda unyama ni mwanae miaka zaidi ya 10.
Mama kutaka azikwe eneo X ilikuwa ni 'Karma' ili mwanae inamrudi leo hii.

Mfano 3; Marekani kuna wimbi la askari kupata matatizo wakiyaita PSTD(Post stress traumatic disorder)
Idadi ya askari wanaojiua kila siku inaongezeka na hata kuwa ''janga''. Je, hii si karma ?
Hata waliotekeleza uovu huo, kama wametekeleza kwa amri halali on the line of duty, pia wanakuwa hawana hatia yoyote kwasababu wao walikuwa wanatimiza wajibu wao, na kama wameajiriwa kumwaga damu na hiyo ndio kazi yao, wakimwaga damu yoyote kwa amri halali, huko ni kutimiza wajibu wao na damu hiyo haitakuwa juu yao, ni kama mnyongaji, au wanajeshi vitani, sheria ya vita inataka wa target military targets na kama ni kuua, waue wanajeshi na sio civilians, lakini vita haina macho, au kombora halichagui nani mwanajeshi na nani civilians kama Hiroshima na Nagasaki, hadi sisimizi hakusalia, sasa wanajeshi vitani wanapoua innocent civilians damu yao haiwi juu ya wanajeshi hao bali aliyeanzisha vita hiyo au aliyetoa amri hiyo.
Amri halali ndiyo subject hapa.Vitani ni amri halali.

Mnyongaji anatenda kwa amri halali tena mchana kweupe baada ya process nzima ya uhalali kufanyika.

Wanaokabiliwa na adhabu ya kunyongwa kamwe hawalaumu wanaotimiza wajibu.Ni amri halali.

Swali, amri halali mipaka yake ni ipi?

Kuna sababu inaitwa halali, kwa maana imepitia hatua halali, imeelezwa kihalali, imeidhinishwa kihalali.

Hata vitani kuna kitu kinaitwa ''rule of engagement' kwamba, kuna abcd za kufanya na kutofanya.

Uwepo wa 'rule of engagement' unalenga kuhakikisha askari wanatimiza amri halali kama ilivyoelezwa.

Kwahiyo amri halali ina namna zake na mipaka yake si ''open season''

Mkuu P huku mitaani watu hujitoa katika baadhi ya maamuzi ya Familia au Ndugu yenye utata.
Kauli kubwa unayoisikia ni moja '' wana nawa mikono yao'', kwa maana wanajiepusha na ''karma''

Hoja yangu hapa ni maoni tu ya jumla juu ya Karma. Hailengi kuhusu tukio au watu kwa namna yoyote
 
Back
Top Bottom