Amemchoma Mke wake wa zamani ili afukuzwe kazi. Je, kakosea?

Nyamesocho

JF-Expert Member
May 5, 2023
476
1,244
Jamaa anadai huyu Jenifer ( siyo jina halisi) alikuwa mke wake wa ndoa, walipofunga ndoa jamaa alifanya janja janja ili angalau na mke wake apate sehemu ya kupata kipato chake

Akiwa ndo wana mtoto mmoja jamaa aliandaa mazingira fulani akapata cheti na kufanikisha mke wake kuingia chuo na baada ya chuo akaajiriwa Halmashauri moja ya mkoa wa Mtwara,

Baada ya mke wake kuanza kazi kule huku jamaa akiendelea na biashara zake katika jiji la mwanza mke wake alianza kubadilika.Anasema siku ya mwanamke kuripoti kazini kwake jamaa alimpeleka na kumtafutia nyumba maeneo ya mjini huku akimuahidi akimaliza miaka 3 atamhamishia katika jiji la mwanza
Hata hivyo jamaa naye alikutana na kisanga cha kumpiga mwanamke mwingine mimba na kwa kuwa ana pesa aliamua kumuoa baada ya kukubaliana na mkewe Jenifer

Kadri siku zilivyozidi kwenda Jenifer alizidi kupunguza mawasiliano na baadae kutopatikana kabisa na kumpelekea mwanaume kumfuatilia huko kazini,hata hivyo majibu aliyopata jamaa kutoka kwa Jenifer ni kuwa wasingeweza kuendelea na ndoa yake kwa sababu alishaoa,bora tu amuache apambane na maisha yake

Baada ya majibu ya aina hiyo jamaa aliamua kumchoma utumishi kwamba mtumishi mwenye jina hili anayefanya kazi sehemu fulani vyeti vyake si halali,anatumia vyeti vya marehemu ambapo baada ya mamlaka kumfuatilia Jenifer na kujirisha na kufukuzwa kazi

Je jamaa amefanya jambo sahihi au amebugi?
 
jamaa naye alikutana na kisanga cha kumpiga mwanamke mwingine mimba na kwa kuwa ana pesa aliamua kumuoa baada ya kukubaliana na mkewe Jenifer
images (2)i.jpeg


PambanaZaidi/CottonandMore
 
Huyo jamaa ni mbinafsi. Yani yeye afanye atakavyo kwa matarajio mwanamke akae akimsubiria tu.

Mshauri Jennifer na yeye amchome jamaa kuwa ana biashara ya kughushi vyeti feki.
 
Huyo mwanamke atapitia kipindi kigumu lakini mwisho wa siku atatoboa tu. Huyu mwenzetu mbinafsi kupitiliza.

Kitendo Cha kumpachika mgimba na kuona Mke mwingine ilikua ni kosa lajinai, kama alisamehewa, kwanini iwe ngumu kumwelewa mwenzake?

Na hapa ni upande mmoja wa simulizi, ukiwasikiliza wote, utakuta jamaa ana mambo meusi meusi mengi sana, mzinguaji.
 
Yanini yote hayo!!?na mwanamke umemzalisha mtoto wako mwenyewe!!?

Japo no kweli wanawake wanakera sana wakishapata uhakika was maisha (with personal experience)lakini kama mwanamme unaachilia tu na kusonga mbele coz hujui nani kesho atakua muhimu kwako!!
 
Back
Top Bottom