Azoge Ze Blind Baga
JF-Expert Member
- Mar 8, 2019
- 366
- 1,376
Nashindwa sometimes kuelewa nini faida na umuhimu wa ndoa kama mambo yenyewe huwaga hivi.
Kuna mzee mmoja alikua jirani yangu, alikua mhandisi wa shirika moja kubwa hapa nchini
Mzee huyu kutoka kule migombani alioa mke wa migombani pia. Maisha yalikua mazuri wakati mzee bado anafanya kazi.
Alijenga nyumba mikoa mbalimbali na alijitahidi kuwasomesha watoto wake shule nzuri hizi za saint saint.
Watoto wake wote wana shughuli zao nzuri tu.
Baada ya kustaafu hapo ndo akaanza kuona rangi halisi ya mke wake. Kwanza alimtumia wakora wamfanye kitu mbaya ili mke arithi mali mapema bahati nzuri ndugu wa mume wakashtukia mapema mission ikabuma.
Tangu wakati huo mke akaanza kumtenga mume wake na kibaya zaidi hadi watoto wake aliowasomesha wakamtenga baba yao na kumsahau kabisa(sijui mama yao aliwaambia nini)
Dingi akaanza kunyimwa chakula, dingi akakimbiwa chumba na mke wake(alikua anatuambia vijana na kutuhasa juu ya makabila ya kuoa)
Baada ya muda mzee kaanza kurukwa na akili kwa maisha aliyokua anaishi.
Kwa sasa mzee karudi kwao lakini akili yake haiko sawa kaacha mali zote anaishi kijijini kwao. Watoto wake wamemtupa hawana time na baba yao
Je nini hasa wamama wanawaambia watoto wao kiasi cha watoto kuanza kumchukia baba yao na kumtenga ili hali aliwasomesha na kuwalea vizuri na juhudi zake waliziona.?
Hili ni janga kwenye familia nyingi baba akistaafu anaishi maisha magumu ya kunyanyasika juhudi zake zote alizofanya kujenga familia bora zinakua kazi bure anaishia kutengwa na kupata msongo wa mawazo na mwisho kufa.
KATAA NDOA NI UUAJI NA UTAPELI