Mwanaume mke wako akija kukulalamikia kuhusu mfanyakazi ambaye hamtaki fanya uchunguzi kwanza

passion_amo1

JF-Expert Member
Dec 3, 2023
1,687
3,405
wasaalamu ndugu Watanzania?

Ndugu zangu wanaume wote ambao tupo ndani ya ndoa, mahusiano na mwanaume yoyote anayeelekea huko, naomba niseme kitu kuhusu wanawake hawa tunaoishi nao.

Mimi binafsi huwa siamini kuhusu uwepo wa mungu ila kuna baadhi ya stori kwenye biblia huwa zina mafundisho mazuri sana katika dhana nzima ya mantiki. Yusuphu alipokuwa uhamishoni nchini misri aliingia katika jaribu la kutakwa kimapenzi na Mke wa mkuu wake Potipha.Lakini yusuphu alikimbia mtego ule na Mke yule akamsingizia kwamba yusuphu alitaka kumbaka na kuishia kutupwa ndani ya gereza.

Leo nimesikia stori ya ndugu mmoja aliyekuwa akifanya kazi kwa kibopa (Tajiri) mmoja hapa Dar-es-salaam imenisikitisha sana.

Tajiri huyu ana kampuni inamilika magari kwenye nyanja tofauti tofauti, kama usafiri wa kawaida, na Basi za utalii. Huyu ndugu alifanya kazi kwa uaminifu sana kama kwenye vipengele vya mkataba vinavyomueleza, basi akiwa katika majukumu ya kila siku akapokea simu kutoka kwa mama wa familia akimuomba aende nyumbani kuna mahala anahitaji kumuagiza, alishangaa sana sababu mara nyingi huwa akimpeleka mzee hapo na kuondoka lakini sasa mzee hayupo na ninahitajika kufika hapo kinyume na taratibu za kazi yake.

Akamwambia mama nafikiri kwa muda huu hautawezekana labda kama kuna njia ambayo naweza shauri ili jambo lako litimie, mama akawaka akasema njoo mimi nahitaji kukuagiza. Basi ikabidi aende kwa kulazimishwa.

Baada ya kufika pale nyumbani mama yule alitoka akmpa ki parcel(mzigo mdogo) akampa maelekezo huku akisema nimeshindwa kuongea kwenye simu sababu nilihitaji nije kukuelekeza zaidi. Mama baada ya kutoa maelekezo ni wapi kinapaswa kupelekwa jamaa akawasha gari na kuelekea mitaa fulani ya ushuani huko mjini pembezoni mwa bahari.

Baada ya kufika sehemu aliyoelekezwa akampigia mama simu na kumuelezea kuwa nimefika, mama akasema subiri kuna mtu atakuja hapo na akakata simu. Baada ya muda akaja jamaa wakasalimiana akampatia parcel ile na yeye akaondoka.

Basi siku zikaendelea, akiwa anafanya kazi zake vzuri, mama akampigia simu akamwambia nahitaji kukuagiza mara moja uelekee airport ukamchukue mgeni, safari hii jamaa ikabidi awe na msimamo, akamwambia madam nakuheshimu sana ila kwa sasa sitaweza sababu Nipo na kazi na boss ni mtu ambaye hapendi mchezo na kazi sababu gari zote zimefungwa GPRS na zina kuwa tracked hivyo kuonekana muda huu huko bila sababu kutaniweka matatizoni, madam akamwambia sawa tutaona na akakata simu.

Basi jamaa jioni mzee akamuagiza nyumbani apeleke baadhi ya vitu, akafunga safari na gari mpaka pale nyumbani lakini alipofika getini akakutana na gari imepaki kwa nje kidogo na madam yupo pale kasimama baada ya kuchunguza zaidi akagundua ni jamaa aliyempeleka parcel(mzigo) kule ushuani baada ya kuona ametoa kichwa kwa nje. Ikabidi apige honi kimya na wakati huo madam yupo pale pembeni, akashuka kuingia akakutana na mlinzi ila ni mgeni si aliyezoea kumkuta pale. Basi ikabidi tu afungue geti lile asiulize kwann mlinzi yule yupo pale na hajafungua.

Akaingiza gari ndani, na kuanza kutoa vitu baadhi ikiwa ni vya nyumbani kama vya kupandia maua vile vyungu na vitu vingine vya urembo wa nyumba. Akaviweka pale na wakati huo madam akiwa anarudi ndani.

Alipofika pale alimsalimia madam lakini hakuitika, alimpita na kuingia ndani ikabidi apige simu kwa mzee na kumuambia kwamba mzigo umefika. Mzee akamuuliza mama kauona akasema ndio na kafurahi sana, akasema sawa akatoa gari na kuondoka.

Tangu hapo visa vikaanza, madam mume wake alipokuwa anarudi toka kazini akamuambia sasahiv huyu kijana Amekuwa na tabia mbovu na chafu sana, mzee akauliza Kwanini unasema hivyo akamwambia siku moja kaleta mizigo ndani akaingia jikoni na kukaa nyuma yangu akiniangalia matako yangu, najisikia vbaya sana huyu mtu hafai muulize hata mwanao, mzee alikuwa na watoto wakike wawili mkubwa alikuwa anaenda na kurudi. Kumbe madam alishampanga binti yake.

Basi mzee kusikia hivyo alighadhibika sana akamuita binti yake na kuongea nae nje kuhusu asemalo mama yake binti akakubali akasema ni kweli kabisa.

Mzee kusikia hivyo akanyanyua simu kumpigia jamaa akamwambia naomba hapo ulipo sasahivi zima gari halafu natuma mtu aje kuchukua hiyo gari utajua utapoenda wewe, akabaki anashangaa ni nini hichi? Ikabidi awe mpole akazima gari akatulia na baada ya muda akaja jamaa akashuka na jamaa akabaki pale anashangaa ni nini kimetoka!

Ikabidi baadae ampgie boss, lakini simu zilipigwa na hakupokelewa, baada ya siku mbili jamaa akaja kuchukuliwa home kwake na watu waliojitambulisha polisi, wakaondoka nae mpaka kituoni, walipofika pale akaambiwa una tuhuma za upotevu wa pesa za ofisi katika kampuni fulani. Akabaki anashangaa! Baada ya kuunganisha matukio akaona kwamba madam kwa namna yoyote kanichoma kwa mzee.

Basi baada ya siku moja mzee alifika pale, amekasirika sana sura ameikunja misiri ya mashabiki wa simba kwenye kipigo cha goli tano.jamaa akatolewa na kwenda kwenye chumba cha mahojiano kule lakini akasema mimi mzee sijui chochote mzee akasema ngoja kwanza nikuache tuendelee uchunguzi. Basi pale muda anaondoka akamwambia mzee lakini naomba niseme jambo moja, naomba umchunguze madam kama kweli nimeingia hapa sababu yake naomba mzee umchunguze kwa karibu.

Mzee akapotea hapo kituoni jamaa akarudi selo, basi mzee kweli alianza kumchunguza mke wake kwa kumuekea ma spy akaja kugundua mke ana mahusiano ya kimapenzi na jamaa ambaye alipelekewa parcel(mzigo) kule ushuani.

sasa mzee kaja kugundua ukweli akarudi kumuomba radhi jamaa, akamuambia amsamehe na anOmba arudi kazini hayo yote wasahau wagange mambo mapya.

Wanawake ni viumbe tunapaswa kuishi navyo kwa makini na nyinyi wanawake muwe na huruma!

Una mshauri nini jamaa huyu?
 
Nafikiri hujasoma kwa ufahamu.

Mimi nimesema siamini, sina haki ya kufanya huyu yaliyomkuta asiamini!

Unalelewa lakini ulichoandika?
Aliyeleta ndiye anayejibiwa kama alivvoandika. Na ndie aliyeomba ushauri.

Hapo nina maana nimesoma kwa ufahamu.
 
Wapi ushauri umeombwa uwe specified?

Ulikwenda shule kufanya nini mkuu?

Unamshauri nini huyu jamaa?
Una upeo mdogo sana au una tatizo la kutoelewa.
Hapo ndio utajua wewe ndio upeo mdogo. Yeye hajakutuma kuja kuomba ushauri. Kuelimika kuna umuhimu kuliko kwenda shule harafu usielimike.

Wewe ndio unasema unamshauri nini huyu jamaa?
Kwenye gazeti lako haujaandika jamaa anahitaji ushauri!
 
Hapo ndio utajua wewe ndio upto mdogo. Yeye hajajutuma kuja kuomba ushauri. Kuelimika kuna umuhimu kuliko kwenda shule harafu usielimike.

Wewe ndio unasema unamshauri nini huyu jamaa?
Kwenye gazeti lako haujaandika jamaa anahitaji ushauri!
Hukuona boss akimuomba arudi kazini?

Harafu ni kitu gani?

Ipo sentensi inayosema unamshauri nini huyu jamaa.

Kama huna la kushauri soma jifunze tulia.
ahsante
 
Back
Top Bottom