CHAMVIGA
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 7,687
- 2,240
Nimemsikia msemaji wa al shabaab asubui hii BBC anasema Jihad is their religion akawa ananukuu vifungu vya Kitabu sina hakika kama ni Quran au la!...Hivi Jihad ni nini hasa maana yake!
Jihadi inatokana na neno la kiarabu ikimaana kujitahidi, kujitolea, mashaka na tabu.
Katika uislamu Jihad inamaana kujitolea ili ndoo la MUNGU liwe lenye kutawala na watu wahukumiwe na Sheria ya Mungu.
Jihadi ina maana kupigana mtu na nafsi yake kuacha maaswi ni jihadi.
Mtu kulingania wengine kuacha maovu na kufanya mema pia ni jihadi.
Na pia jihadi inapiganwa kwa njia ya vita ya siraha.
Jihadi ya siraha hupiganwa baada ya jihadi ya maneno kufeli na kukatokea upinzani wa kivita kutoka kwa wenye kuipinga sheria ya Mungu.
Jihadi hii
Ina masharti yake na vizuizi yake.
Miongoni mwa masharti hayo ni pamoja kutokuuwa wasiohusika ktk vita bali vita iwe kwa wale wanaokupiga tu.
Pia hairuhusiwi kuua watoto, wanawake, wazee na watu wote wasiohusika.