SoC02 Almasi katikati ya miiba

Stories of Change - 2022 Competition

Ivyson

Member
Aug 31, 2022
22
29
Vipi nikikuambia kuwa leo hii inawezekana kutumia viumbe hai vidogo visivoonekana kwa macho kama Bakteria au Kuvu kutengeneza kinga ya mwili, dawa kwa ajili ya kutibu magonjwa yanayaothiri afya zetu, au kusafisha mazingira, au kutengeneza bidhaa mbalimbali kama pombe, maziwa, sabuni, dawa za kuua wadudu wanaoharibu mazao ya shambani.

Au vipi pia nikikwambia kua leo hii inawezekana kuzalisha mazao ambayo yana virutubisho zaidi ya vile vinavopatikana katika zao husika kwa mfano mchele wenye protini, vitamini na wanga kwa Pamoja kwa wingi, au kutengeneza mimea ambayo inaweza kustahimili magonjwa, wadudu waharibifu, na mabadiliko ya hewa, inavutia si ndio?

Basi karibu katika ulimwengu wa bioteknolojia, ambao unatumia viumbe hai au bidhaa zinazozalishwa na viumbe hai kutengeneza bidhaa au michakato iliyobadilishwa kwa ajili ya kunufaisha binadamu. Kwa mfano hujawahi kujiuliza pombe ya mnazi inapatikanaje? Je, ni kwamba mnazi unazalisha pombe moja kwa moja? Sio kweli bali ni wadudu kama bakteria na kuvu ambao huingia kwenye chombo chenye maji maji yatokayo kwenye mnazi na kumeng’enya na kuyachachua kuwa pombe. Mifano ya bidhaa nyingine zitokanazo na teknolojia hii ni kama protini, maziwa, vitamini, dawa na nyingine nyingi.

1.jpg

(Chanzo: Daily Post Nigeria - Nigeria News, Nigerian Newspapers)
Picha ya juu: Pombe ya mnazi, moja ya bidhaa za bioteknolojia itengenezwayo kienyeji

Je ni changamoto gani zinazoikumba bioteknnolojia nchini Tanzania?

Licha ya kuwa na faida kubwa sana katika kuchochea maendeleo katika sekta mbalimbali kama za kilimo, Afya, Mazingira na Viwanda, teknolojia hii nchini Tanzania bado haifahamiki na watu wengi na baadhi wanaoifahamu wanaipinga kutokana na habari potofu, ukosefu wa elimu ya kina kuhusu bioteknolojia, hofu, pia maadili yamechangia.

Pia uwepo wa vituo vichache vya utafiti, vifaa vya utafiti na misaada kutoka serikalini imepelekea Tanzania kutoitumia bioteknolojia kikamilifu kuongeza uzalishaji wa bidhaa zitokanazo na teknolojia hii ndio maana mpaka leo hii bidhaa nyingi zinaagizwa nje ya nchi wakati ingewezekana kuzalisha wenyewe na kuepuka gharama hizo ili kuongeza uzalishaji wa bidhaa hizi nchini kama dawa na chanjo kwa sekta ya afya.

Kwa nini teknolojia hii ni muhimu kukuza maendeleo ya nchi na ina faida gani kwa binadamu?

Kwa kuanza na Sekta ya Afya je, unafikiri chanjo za magonjwa kama Uviko, Tetekuwanga, Polio, Surua, Tetanasi na zinginezo zinapatikanaje? Au dawa za magonjwa kama ya Kisukari, Ukimwi, Kifua kikuu, Malaria na mgonjwa mengine mengi zinapatikanaje? Jibu ni rahisi kupitia bioteknolojia yote haya yamewezekana kwa kutengeneza chanjo na dawa mbali mbali ambazo mpaka leo hii zimeweza kuimarisha afya zetu na kupunguza vifo. Pia tiba za jeni zimesaidia sana kutibu magonjwa ambayo si rahisi kutibiwa na dawa za kawaida.​

2.jpg
(Chanzo: bionews-tx.com)

3.jpg
(Chanzo: writeopinions.com)

4.jpg
(Chanzo: worthview.com)

Picha ya juu: (juu) Jeni yenye matatizo ya kutengeneza insulin inarekebishwa, (katikati) Insulini iliyotengenezwa kutibu kisukari. (chini) mgonjwa wa kisukari anajidunga sindano yenye insulin kutibu kisukari

Kwenye sekta ya kilimo bioteknolojia inasaidia hasa kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula kwa wingi na yaliyo bora kwa kusaidia mimea kukua vizuri kwa njia nyingi kama kuibadilisha na kuifanya kustahimili magonjwa, wadudu waharibifu, na mabadiliko ya hewa. Pia kwa kuirekebisha iweze kuzalisha mazao bora na yenye virutubisho ili kuongeza uwepo wa vyanzo vya chakula kwa binadamu. Baadhi ya mazao yaliyobadilishwa vinasaba na kuruhusiwa kutumika ni kama mahindi, pamba, maharage ya soya ambayo yanaweza kujikinga na wadudu waharibifu na magonjwa bila kutumia dawa.
R.jpg

Chanzo(agfax.com)
Picha ya juu: kushoto ni mahindi ya bt ambayo yanajikinga na wadudu na magonjwa na kulia ni mahindi ya kawaida
Kwenye sekta ya Viwanda bioteknolojia imepelekea uzalishaji wa bidhaa nyingi kwa urahisi kwa kutumia viumbe hai kama bakteria na Kuvu kutengeneza bidhaa kama pombe na mvinyo, sabuni, virutubisho kama protini na vitamini, vimeng’enya, dawa za kuua wadudu wa shambani, siki. Maziwa, mikate na bidhaa nyingine nyingi.​

5.png

Picha ya juu: Baadhi ya bidhaa zinazotokana na bioteknolojia viwandani

Kwenye sekta ya mazingira bioteknolojia inasaidia kusafisha mazingira ili yawe rafiki kwa binadamu mfano bakteria wanatumika katika kusafisha maji machafu kwenye miji mikubwa ambayo hurudishwa na kutumiwa upya na watu hivo kupunguza uhaba wa maji. Pia utengenezaji wa nishati ya mimea husaidi kupunguza matatizo yanayosababishwa na mafuta ya visukuku kama ongezeko la joto na mabadiliko ya tabia nchi. Utengenezaji wa bioplastiki unaweza ondoa tatizo la uchafu unaosababishwa na plastiki za kawaida.
Is-Hemp-Plastic-Biodegradable-scaled.jpg

Chanzo: theboonroom.com
Picha ya juu: Bioplastiki ambazo zinaweza kuharibika na kuepusha uchafu wa plastiki za kawaida

Je vijana wanaweza kujiajiri vipi ili kunufaika na bioteknolojia?

Nikutoe shaka kijana kuwa kunufaika na bioteknolojia sio lazima uingie Chuo kikuu Cha Dar Es Salaam ukae darasani uanze kufundishwa kwani kuna bidhaa nyingi na zenye soko ambazo hazihitaji elimu kubwa ijapokuwa kuna bidhaa nyingine zinahitaji elimu kubwa.

Kwa vijana waliosomea bioteknolojia wana upana mkubwa wa kujiajiri kwani bidhaa nyingi wataweza kuzitengeneza na kuingiza sokoni kama dawa za kuua wadudu wanaoharibu mazao ya shambani za kibayoteki au wanaweza kutengeneza mivinyo, pia wanaweza kuzaisha vimeng’enya vitumikavo viwandani, bidhaa nyingine kama protini, mbegu za uyoga, na vinginevo. Baadhi wanaweza pata bahati ya kuajiriwa pia ambamo yote ni kheri na faida.

Kwa vijana wasiosomea bioteknolojia pia wanaweza kunufaika kwa kutengeneza bidhaa ambazo zinahitaji kupewa elimu ndogo mifano, mvinyo, mtindi, mikate, siki, au kilimo cha uyoga vyote ambavyo vina soko na bidhaa nyinginezo.

Siku zote chenye faida hakikosi hasara.

Baadhi ya hasara zitokanazo na Bioteknolojia ni kama zifuatozo; ikitumika na watu wenye malengo mabaya inaweza ikasababisha kutengenezwa kwa silaha za bio mfano znazosambaza ugonjwa au sumu, pia ikitumika na watu wasio na vigezo vya elimu inaweza pelekea kutengeneza bidhaa zinazoweza hatarisha afya ya binadamu na michakato ya mimea. Pia kutumika sana kwa bidhaa za bioteknolojia inaweza kupelekea uzalishaji wa aina fulani ya mimea kwa wingi kuliko kawaida au kwa binadamu inaweza badilisha mfumo wa kawaida wa kazi ya mwili sehemu fulani na kuhatarisha afya.

Serikali ya Tanzania katika kudhibiti madhara yatokanayo na bioteknolojia

Licha ya kuwa na hasara nikutoe hofu kuhusu bioteknolojia kwakua serikali ya Tanzania imetengeneza Mfumo wa kitaifa wa usalama wa bio kwa Tanzania (“The National Biosafety Framework for Tanzania”) ambao unalinda watanzania dhidi ya bidhaa zitokanazo na bioteknolojia ambazo zinaweza kuwadhuru kwa kuwana elementi ambazo ni Sera za kitaifa zinazoongoza utumiaji wa bioteknolojia, utawala wa udhibiti, taratibu za kiutawala, Utaratibu wa ufuatiliaji, na taratibu za uhamasishaji na ushiriki wa umma.

Pia serikali ya Tanzania inatumia tahadhari kusimamia bidhaa zilizotengenezwa kwa vinasaba nchini. Kutokana na kifungu kikali cha dhima katika Kanuni za usalama wa bio za mwaka 2009, hakuna bidhaa za vinasaba zinazoingizwa au kuuzwa nchini Tanzania. Kanuni hiyo inaunda marufuku ya bidhaa za vinasaba na vinginevyo kutokana na mapungufu mengi, kama vile ukosefu wa msingi mzuri wa kisayansi, na uwezo wa kupotosha vipaumbele vya udhibiti.

Mwisho ningependa kuishauri serikali na wananchi wa ujumla kuongeza uchochezi wa kutoa elimu hii iwafikie wengi na utumiaji wa bioteknoljia uongezeke kwani faida zake ni nyingi kuzidi uzito wa hasara zinazoweza kutokea na kwa kuwa serikali imeshajiandaa kudhibiti madhara yanayoweza sababishwa na teknolojia hii usalama wa watumiaji wa bidhaa hizi ni mkubwa kwani mpaka ifike kwa jamii imeshakaguliwa na kuhakikishwa zipo salama kwa matumizi.

Vijidudu vinaweza kukupa unachotaka, ujue tu jinsi ya kuuliza.

Asante kwa kusoma Makala hii.

Marejeo
VICE PRESIDENT’S OFFICE 2004, The National Biosafety Framework for Tanzania.
Okafor N and Okeke B 2017, Modern Industrial Microbiology and Biotechnology 2nd Edition

Ndugu msomaji unaombwa kupigia makala hili kura wa kubofya alama hii ^ chini mwisho wa makala kama umependezwa nayo

Pia karibuni kwa maswali na nyongeza
Asante
 
Vipi nikikuambia kuwa leo hii inawezekana kutumia viumbe hai vidogo visivoonekana kwa macho kama Bakteria au Kuvu kutengeneza kinga ya mwili, dawa kwa ajili ya kutibu magonjwa yanayaothiri afya zetu, au kusafisha mazingira, au kutengeneza bidhaa mbalimbali kama pombe, maziwa, sabuni, dawa za kuua wadudu wanaoharibu mazao ya shambani.

Au vipi pia nikikwambia kua leo hii inawezekana kuzalisha mazao ambayo yana virutubisho zaidi ya vile vinavopatikana katika zao husika kwa mfano mchele wenye protini, vitamini na wanga kwa Pamoja kwa wingi, au kutengeneza mimea ambayo inaweza kustahimili magonjwa, wadudu waharibifu, na mabadiliko ya hewa, inavutia si ndio?

Basi karibu katika ulimwengu wa bioteknolojia, ambao unatumia viumbe hai au bidhaa zinazozalishwa na viumbe hai kutengeneza bidhaa au michakato iliyobadilishwa kwa ajili ya kunufaisha binadamu. Kwa mfano hujawahi kujiuliza pombe ya mnazi inapatikanaje? Je, ni kwamba mnazi unazalisha pombe moja kwa moja? Sio kweli bali ni wadudu kama bakteria na kuvu ambao huingia kwenye chombo chenye maji maji yatokayo kwenye mnazi na kumeng’enya na kuyachachua kuwa pombe. Mifano ya bidhaa nyingine zitokanazo na teknolojia hii ni kama protini, maziwa, vitamini, dawa na nyingine nyingi.

View attachment 2343984
(Chanzo: Daily Post Nigeria - Nigeria News, Nigerian Newspapers)
Picha ya juu: Pombe ya mnazi, moja ya bidhaa za bioteknolojia itengenezwayo kienyeji

Je ni changamoto gani zinazoikumba bioteknnolojia nchini Tanzania?

Licha ya kuwa na faida kubwa sana katika kuchochea maendeleo katika sekta mbalimbali kama za kilimo, Afya, Mazingira na Viwanda, teknolojia hii nchini Tanzania bado haifahamiki na watu wengi na baadhi wanaoifahamu wanaipinga kutokana na habari potofu, ukosefu wa elimu ya kina kuhusu bioteknolojia, hofu, pia maadili yamechangia.

Pia uwepo wa vituo vichache vya utafiti, vifaa vya utafiti na misaada kutoka serikalini imepelekea Tanzania kutoitumia bioteknolojia kikamilifu kuongeza uzalishaji wa bidhaa zitokanazo na teknolojia hii ndio maana mpaka leo hii bidhaa nyingi zinaagizwa nje ya nchi wakati ingewezekana kuzalisha wenyewe na kuepuka gharama hizo ili kuongeza uzalishaji wa bidhaa hizi nchini kama dawa na chanjo kwa sekta ya afya.

Kwa nini teknolojia hii ni muhimu kukuza maendeleo ya nchi na ina faida gani kwa binadamu?

Kwa kuanza na Sekta ya Afya je, unafikiri chanjo za magonjwa kama Uviko, Tetekuwanga, Polio, Surua, Tetanasi na zinginezo zinapatikanaje? Au dawa za magonjwa kama ya Kisukari, Ukimwi, Kifua kikuu, Malaria na mgonjwa mengine mengi zinapatikanaje? Jibu ni rahisi kupitia bioteknolojia yote haya yamewezekana kwa kutengeneza chanjo na dawa mbali mbali ambazo mpaka leo hii zimeweza kuimarisha afya zetu na kupunguza vifo. Pia tiba za jeni zimesaidia sana kutibu magonjwa ambayo si rahisi kutibiwa na dawa za kawaida.​

View attachment 2343836
(Chanzo: bionews-tx.com)

View attachment 2343845
(Chanzo: writeopinions.com)

View attachment 2343848
(Chanzo: worthview.com)

Picha ya juu: (juu) Jeni yenye matatizo ya kutengeneza insulin inarekebishwa, (katikati) Insulini iliyotengenezwa kutibu kisukari. (chini) mgonjwa wa kisukari anajidunga sindano yenye insulin kutibu kisukari

Kwenye sekta ya kilimo bioteknolojia inasaidia hasa kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula kwa wingi na yaliyo bora kwa kusaidia mimea kukua vizuri kwa njia nyingi kama kuibadilisha na kuifanya kustahimili magonjwa, wadudu waharibifu, na mabadiliko ya hewa. Pia kwa kuirekebisha iweze kuzalisha mazao bora na yenye virutubisho ili kuongeza uwepo wa vyanzo vya chakula kwa binadamu. Baadhi ya mazao yaliyobadilishwa vinasaba na kuruhusiwa kutumika ni kama mahindi, pamba, maharage ya soya ambayo yanaweza kujikinga na wadudu waharibifu na magonjwa bila kutumia dawa.
View attachment 2344011
Chanzo(agfax.com)
Picha ya juu: kushoto ni mahindi ya bt ambayo yanajikinga na wadudu na magonjwa na kulia ni mahindi ya kawaida
Kwenye sekta ya Viwanda bioteknolojia imepelekea uzalishaji wa bidhaa nyingi kwa urahisi kwa kutumia viumbe hai kama bakteria na Kuvu kutengeneza bidhaa kama pombe na mvinyo, sabuni, virutubisho kama protini na vitamini, vimeng’enya, dawa za kuua wadudu wa shambani, siki. Maziwa, mikate na bidhaa nyingine nyingi.​

View attachment 2343883

Picha ya juu: Baadhi ya bidhaa zinazotokana na bioteknolojia viwandani

Kwenye sekta ya mazingira bioteknolojia inasaidia kusafisha mazingira ili yawe rafiki kwa binadamu mfano bakteria wanatumika katika kusafisha maji machafu kwenye miji mikubwa ambayo hurudishwa na kutumiwa upya na watu hivo kupunguza uhaba wa maji. Pia utengenezaji wa nishati ya mimea husaidi kupunguza matatizo yanayosababishwa na mafuta ya visukuku kama ongezeko la joto na mabadiliko ya tabia nchi. Utengenezaji wa bioplastiki unaweza ondoa tatizo la uchafu unaosababishwa na plastiki za kawaida.
View attachment 2343919

Thread nzuri ila nngependa kuuliza kwa nini almasi katikati ya miiba.
 
Swali zuri, ni kwasababu kupata faida hizi tunatumia viumbe hai vidogo kama virusi, bakteria na kuvu ambao ni hatarishi kwa afya ya binadamu kama wasipotumiwa kama inavotakiwa. Kwa mfano chanjo ya UVIKO ambayo ina virusi vilivopunguzwa nguvu ikitumiwa kwa mtu mwenye upungufu kwa kinga mwilini badala ya kumsaidia inaweza kumletea ugonjwa. Hivo tunapata faida kutoka kwenye wadudu hatarishi ambayo ni miiba
 
Thread nzuri sana na yenye madini. You have my vote.
 
Andiko zuri, ila nngependa kujua je, bioteknolojia ni salama?
 
Ndio, ikiwa imedhibitiwa vizuri, kama ilivyo kwa vyakula vyote. Mashirika mengi ya kimataifa - kama vile Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa(FDA), Shirika la Afya Duniani(WHO), na Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo - wametambua kwamba teknolojia ya kibayoteknolojia, inapotumiwa vizuri, haiathiri usalama wa bidhaa. Nchini Marekani kwa mfano vyakula vilivyotengenezwa kupitia bioteknolojia vinakabiliwa na mahitaji yale yale ya udhibiti ambayo Utawala wa Chakula na Dawa hutumia kulinda vyakula vingine na viambato vya chakula sokoni. Hakuna ushahidi kwamba vyakula vya kibayoteki kwa sasa kwenye soko vinaleta hatari kwa afya ya binadamu.
 
Mimi naitwa Lumola Nimekupigia Kura Naomba na Mimi unipigie Kura kupitia SoC 2022 - Tufuge nyuki kwa maendeleo endelevu na tuwalinde kwa wivu mkubwa
 
SoC 2022 - Agizo lolote linapotelewa, muongozo wa mbadala wake utolewe, ili kuepusha kukiukwa kwa agizo hilo Kaisome hii, utanishukuru baadae
 
Back
Top Bottom