Nimeweka link hapo juu, alikamatwa na akakiri kabisa mwaka jana mwezi wa 5 lakini wananchi wanashangaa yupo bado mtaani.
 
Pole kwa familia,ndugu na jamaa,may his soul R.I.P.
Mob justice ni mbaya,wangempeleka mbele ya vyombo vya sheria,haki itendeke,ukute alisingiziwa au kafananishwa.
Nani angeenda kutoa ushahidi kuithibitishia mahakama kuwa aliua? Mahakama haiwezi kupata ushahidi wa uhalifu, jamii inayomzunguka ndiyo inayomjua. Hayajawahi kukukuta ndiyo maana unasema R.I.P kwa muuwaji aliyeuawa. Wakati mwingine tukubali tu kuna wahalifu tunaishi nao kwenye jamii zetu inatakiwa wasiishi wanasumbua kuanzia wazazi wao. Jamii za zamani wazazi walikuwa wana declare kwamba huyu katushinda wazee wanamaliza wenyewe. Huwezi kuishi mtaani mnashindwa hata kutuma mtoto dukani kwa sababu ya pimbi mmoja ambaye mnamjua
 
Mafisadi hayooo yanatanua tu! Washenzi wamekunja bilioni 345 kiulainii. Halafu wewe upo unakimbizana na TRA na kiduka chako cha mtaji wa milioni 5 ili watoto wako wale na kusoma. Hawa ndiyo wanakuja kujenga mahekalu ya kutisha na kucheka vijana kuwa siyo wabunifu na kwamba elimu yao haijawasaidia.

Kwenye hukumu hizi kuna ubaya gani kusema kuwa pesa zote zilizoibwa zirudishwe na kila walichonacho kinataifishwa?

Halafu yule mama masikini wakampiga mvua 22 kisa kakutwa na vipande 12 vya nyama ya swala eti nyara za taifa 😬😬😬😬

 
Alhamisi iliyopita nilipata taarifa kwa kijana wa Handeni kuwa Kuna mzee anakuja kumaliza kazi kwani nasikia dogo babu yake wa huko iringa alikuwa anamlinda kimazungara

Chezea Tanga wewe
 
Siku yake ilishafika na alikuwa anakitafuta kifo kwa kila namna ...

Kwa mujibu wa kituo cha Sunrise redio huyo Ally Dangote alikuwa anafanya mauaji na kisha kupotea na baada ya muda anarudi eneo lile lile alilofanya tukio ...

Jana inasemekana alikamatwa na kina mama na bahati ikawa upande wake akafanikiwa akaponyoka na baada ya muda akarudi tena eneo lile lile alilokoswa kukamatwa ..

Cha kushangaza Maeneo yale kuna kituo cha Polisi cha Unga Ltd lakini walishindwa kumdhibiti kwa wakati, hadi kufikia mahakama ya mtaa kutoa hukumu.

Apumzike anapostahili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…