Aliyepoteza huu Mzigo tafadhali anitafute haraka

Aliyepoteza huu Mzigo tafadhali anitafute haraka

Khaa!! Huyu ndiye wiseboy. Kwa kuweka kumbukumbu sawa tu..
Wakuu, mimi kijana wa Kanda ya Ziwa nipo hapa Dar kwa takriban wiki ya pili sasa. Leo katika kuzungukazunguka yangu usiku huu wakati narejea kulala majira ya saa mbili hivi nimeokota pochi yenye kiasi kikubwa hivi cha pesa pamoja na driving license maeneo ya ilala katika flat za wanajeshi kwenye njia inayochepukia kuelekea Kigogo.

Kwanza nimewaza sana iwapo hii ni bahati au lah! Nikajiuliza mara mbili mbili, baadae moyo ukaniambia kuwa mwenye huo mzigo yawezekana nae ana matatizo yake na hiyo pesa ndo alikuwa anaitegemea sana, kwa kuwa mimi kidogo nipo vizuri kiuchumi nimeona ni bora nitangaze, kwa yeyote aliyepoteza aniPM na aeleze jina lake kama lilivyo kwenye license na aseme kiasi halisi cha pesa, kisha tuonane nimpatie mzigo wake.

Warning: Kama huhusiki tafadhali pita sitaki usumbufu wala kejeli, heshima ni kitu cha bure.

Zaidi Ya Miaka Minne Nimefanya Kazi Ktk Kampuni Ya Barrick,kazi Ngumu Chini Ya Ardhi Na Nikikatwa Kodi Kubwa Sana Kuliko Hata Mafao Yangu Ya NSSF,kila Mwezi Nilikuwa Nakatwa Kodi Zaidi Ya Sh 250,000 Kwa Mwezi Na Mimi Kubaki Na Mshahara Wa Sh 800,000 Kodi Hiyo Ni Kubwa Sana Hasa Ukizingatia Maisha Yetu Yalivyo Duni,kilichonifanya Nidai Hiyo Pesa Ni Baada Ya Kuona Mawaziri Wako Kumbe Kodi Tunazolipa Wanagawana Wenyewe Tu Na Hazifanyi Maendeleo Kwa Taifa,hosp Nachangia,wanangu Nawasomesha,ni Kipi Serikali Yako Inanisaidia Kwa Kodi Kubwa Niliyokuwa Nalipa? Ktk Kila Laki Mbili Naomba Lakini Moja Tu,ina Maana Kwa Miaka Minne Niliyolipa Kodi Naidai Serikali Yako Mil 4.8 Naomba Pesa Zangu Tafadhali Maana Kina Muhongo Wamegawana Na Umemfukuza Kazi Tibaijuka Bila Kumpokonya Bil 1.6 Alizoiba Pesa Zetu Walipa Kodi,mimi Nitakuwa Mtanzania Wa Kwanza Kufungua Kesi Mahakamani Kudai Pesa Zangu,maana Huu Ni Ujinga Mh Rais,tunavuja Jasho Halafu Wengine Wanakwiba Mapesa Yetu,naomba Nirudishiwe Pesa Zangu,ushahidi Ninao.
Ndugu zangu wana JF,kwanza kabisa nawasalimu nyote kwa jina la Yesu,mwana wa MUNGU aliye hai,(samahani,hii ni kwa imani yangu tafadhali.) baada ya salamu,mimi ni kijana mwenye uchungu mkubwa sana na mafanikio,nikilenga hasa kuwasaidia wasio nacho.

Ninachoandika hapa ni kweli tupu,nilizaliwa katika familia maskini kupindukia,shuleni nilienda bila viatu,baadae nikaja kupata kazi ktk kampuni moja kubwa ya kuchimba dhahabu na nikawa nalipwa sh 850,000 kwa mwezi,kwa ndoto nilizonazo,nimetoka familia ya kimaskini ya watoto 12,wazazi wangu wananitegemea,na ndugu zangu pia,nikaamua ni bora nipite njia isiyopitwa na watu wengi.

Nayo ni kujiajiri na kusaidia wengine,nilikuwa Kigali nimetoka huko leo,nawaomba sana wale wote walioni pm,kwa nyakati tofauti nitawasiliana nao na kumaliza haja zao,MUNGU wangu awabariki sana wana JF wenzangu kwa kunifariji baada ya ajali kubwa ya gari ambayo ilitaka kuchukua roho yangu,nawapenda sana ndugu zangu iko siku nitawaalika wote ktk hafla maalumu MUNGU akipenda,mbarikiwe nyote kwa yote amen.

===============================================================================================================


Ilikuwa saa 11 alfajiri ya 16/10/2014,wakati nilipomaliza kusali na kumsihi MUNGU wangu anilinde ktk safari yangu ya kwenda Kahama mjini kutoka Bulyanhulu,nilielekea kituo cha basi kwa lengo la kusubiri basi la kunipeleka stend kuu ya mabasi ya mwanza na kahama,ni km 12 kuifikia stend hiyo kutoka kijiji cha ilogi nilipokuwa,basi halikutokea,bahati nzuri akaja dada mmoja na gari lake GX 100 akielekea kazini,akanipa lift,safari ikaanza kwa mbele kidogo ghafla likatokea tela la punda,kwa kuwa alikuwa speed alipojaribu kulikwepa gari ikayumba,ikagoma kurudi barabarani,ikapinduka na kuviringika zaidi ya mara 3,ikajikita kwenye kichaka up side down.

Huwezi amini sikuwa nimefunga mkanda,gari ipo nyang'anyang'a lakini nimetoka salama pamoja na yule dada,hakuna aliyeumia hata mmoja kati yetu,kwa hili nasema,ASANTE SANA MUNGU WANGU,SINA CHA KUKULIPA MUNGU WANGU,NITAJITAHIDI SANA KUTENDA MEMA,NA KUWASAIDIA WOTE WENYE SHIDA KWA KADRI YA UWEZO WANGU,JINA LAKO LIBARIKIWE MUNGU WANGU MKUU,AMEN!

Nitajenga Makanisa 50 Tanzania nzima
Na ndiyo maana MUNGU kaninusuru na kifo ktk ajali ya gari alfajiri ya leo, asante sana MUNGU wangu, leo natoa siri, jamani mimi tayari ninamiliki kampuni ambayo itaanza kazi mwezi ujao,ni kampuni ndogo tu ya ku process mchanga wa dhahabu,na tayari nimepata wadhamini kutoka Australia wamenipa vitendea kazi vingi sana (Tahadhari, siandiki haya kwa lengo la kujitapa au kutafuta shareholder, bali naandika kuwashuhudia mjue ni kiasi gani MUNGU anabariki)

Mimi kwa miaka mingi sana japokuwa namtenda dhambi MUNGU wangu nimekuwa na mzigo rohoni mwangu wa kuwasaidia watu wenye dhiki kuu, kama wajane, watoto yatima, watoto wa mitaani na n.k. Tayari kuna kanisa lipo mbezi(nahifadhi jina) limejengwa kwa misingi yangu, sasa MUNGU akinibariki kampuni yangu itakuwa inaingiza sh mil 150 kwa mwezi, kwa hiyo kama sadaka kwa mambo mema ambayo MUNGU wangu amekuwa akinitendea, nitajenga makanisa 50 katika mikoa yote ya Tanzania, hiyo ndo nadhiri niliyoiweka kwa MUNGU WANGU.

Mbarikiwe jamani.
Ama kweli mshahara wa dhambi ni mauti!

Ni mwaka mmoja sasa umepita tangu nilipoenda Dar kwa lengo la kununua pikipiki ya Kijapan, nikiwa huko tamaa ikawaka, ilikuwa ni mara yangu ya pili kwenda kununua, japokuwa mi mwenyeji huko, nikamtuma dalali wangu pale Jangwani anitafutie mrembo wa kunifariji usiku, ilikuwa kama matani, tukiwa tumegonga bia kadhaa, mara kweli jamaa akaja na binti mrembo mwenye umri kati ya miaka 21 au 24, ambaye wazazi wake wanaishi na kufanya biashara ya almasi Botswana naye anasoma UK alikuwa likizo.

Yule dalali anayejishughulisha pale jangwani akanihakikishia ni mtoto wa ukweli, usiku ule aligoma kulala na mimi, akarudi alikofikia, kesho yake akanitaka tukapime kwanza HIV, nilikubali, na sote tukawa negative, hapo ndo penz likaanza, kuanzia hapo hadi leo amening'ang'ania japokuwa anajua mi mume wa mtu, nimejaribu kumwambia kuwa siwezi kumfikia sina hela, ananirushia hadi lak 5 kwenye M-Pesa, kimbembe sasa, anadai asiponiona hadi Dec atani find aniue naye ajiue, amerudi toka UK amefura.

Nifanyeje jamani?
 
Chunga ndugu yangu huo wema usije ukakuponza.....mimi yalishawahi kunikuta.....mimi binafsi sikushauri kufanya hivyo....
 
Mungu atakuja kukupa kikubwa kuliko hicho ambacho ungeamua kukaa nacho kimya ubarikiwe sana mkuu

Amesema anatoka kanda ya Ziwa na bila shaka ndo mara yake ya kwanza kufika Dar. Du! jinga kweli. Lingekuwa toto langu ningelilibadilisha kwa gunia la mahindi. Ati ubinadamu, kwani umeiba???? Halafu bila shaka ni Msukuma. Wabheja bhabha!!
 
Jana majira ya saa tisa Alasiiri mchana nilipokea ujumbe kwenye PM juu ya mtu aliyekuwa kapoteza pochi yenye pesa. Ujumbe ule uliambatanishwa na namba ya simu, na jina halisi la mwenye pesa kama tu lilivyokuwa kwenye driving license na akataja kiasi halisi cha pesa. Wanajamvi mlinitaka akipatikana mwenye mali nilete feedback, nami nimefanya hivyo.

Ilivyokuwa;

Mwenye pesa si mwana JF mwenzetu, ila rafiki yake ndo mwana JF ambaye alikuwa na taarifa za rafiki yake kupoteza pesa, alipoteza pesa hizo katika ugomvi na mpenzi wake walipokuwa wakitokea bar ya Afri center, nimekutana nao wote jana na wakakubali majina yao niyaweke humu na pesa alizokuwa kapoteza ilikuwa sh 635,000 zikiwa kwenye mkoba mdogo wa kike. Mpotezaji anaitwa Herieth Kanakaitwa mrembo wa haja, rafiki yake ambaye ndo mwana JF mwenzetu anaitwa Zuhura saidi, amegoma nisiweke ID yake.

Walinipa laki mbili kama shukrani, dada huyu katokea kunipenda sana tena sana, amelia sana machozi ya furaha, alijua ndo basi tena, anasema mimi sasa nimekuwa ndugu yake, bravo JF.
 
Jinsi unavyomsifia unazidi kumharibia kwa huyo Mpenzi wake waliegombana, nipe picha yake tafadhali nikawapatanishe
 
Baada ya hapo malizia hivi: Binti mrembo aliyepoteza pochi na mimi kumrudishia anataka ndoa jf nishaulini!
 
Nimemtafuta Google nimemkosa nimepata jina la Grace Kanakaitwa ila Zuhura nimempata, na yeye pia mambo yake si mabaya sana.
 
Jinsi unavyomsifia unazidi kumharibia kwa huyo Mpenzi wake waliegombana, nipe picha yake tafadhali nikawapatanishe

kesi kama hizi weka mbali na mkuu Elli
 
Last edited by a moderator:
Hahaha kweli wewe ni wiseboy. Ila siku ukiwa wiseman utakuja kujua makosa yako
 
Nimemtafuta Google nimemkosa nimepata jina la Grace Kanakaitwa ila Zuhura nimempata, na yeye pia mambo yake si mabaya sana.

Kuna watu humu ndani ni zaidi ya FBI. Mpwa Elli uko juu katika ufatiliaji kwa kina.
 
Last edited by a moderator:
Ukiwa muongo bhana! hauta enda mbali Kabla hujashikwa uongo wako.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom