Aliyepoteza huu Mzigo tafadhali anitafute haraka

Polisi wa bongo sio watu, unaenda kutoa taarifa unageuziwa kibao
Kwanza akipeleka hiyo wallet na hela zake aliyepoteza hatazipata hizo pesa

Wata mwambia kunamtu alikabwa akapoteza vitu kama hivyo, kwahiyo watamuweka ndani asaidie police.
 
tafadhari sana mods nachelea kuamini habari za huyu jamaa na nasema ni MUONGO wa kutupwa kutokana na historia ya thread zake... Anashusha hadhi ya JF kwenye critical matters...

Ombi langu, naomba muingie inbox yake muone kama ana pm ya hivi alivyoandika, kama ni muongo naomba mumpige ban ya maisha... Kama ni kweli nipo radhi mnipige mimi ban.. Hii tabia si nzuri kabisa!!!! Na mkimpiga ban mmoja wetu naomba mtangaze hapa JF.. Ila waongo waache na wasioamini wajifunze!!

wiseboy weka screen shoot tofauti na hapo story yako ni ya kupika! huu ni mwezi wa kwanza na hela ilivyo mbinde kuipata nitakuwa wa mwisho kuamini
 
Last edited by a moderator:

Kama ana account mbili anaweza kutengeneza.
 
Last edited by a moderator:
Rohombaya kaweka reference nzuri sana na kwa hilo mimi binafsi simwamini huyu anayejiita wiseboy.
 
Wakuu, mimi kijana wa Kanda ya Ziwa nipo hapa Dar kwa takriban wiki ya pili sasa. Leo katika kuzungukazunguka yangu usiku huu wakati narejea kulala majira ya saa mbili hivi nimeokota pochi yenye kiasi kikubwa hivi cha pesa pamoja na driving license maeneo ya ilala katika flat za wanajeshi kwenye njia inayochepukia kuelekea Kigogo.

Kwanza nimewaza sana iwapo hii ni bahati au lah! Nikajiuliza mara mbili mbili, baadae moyo ukaniambia kuwa mwenye huo mzigo yawezekana nae ana matatizo yake na hiyo pesa ndo alikuwa anaitegemea sana, kwa kuwa mimi kidogo nipo vizuri kiuchumi nimeona ni bora nitangaze, kwa yeyote aliyepoteza aniPM na aeleze jina lake kama lilivyo kwenye license na aseme kiasi halisi cha pesa, kisha tuonane nimpatie mzigo wake.

Warning: Kama huhusiki tafadhali pita sitaki usumbufu wala kejeli, heshima ni kitu cha bure.
Kwani lazima useme unatokea kanda ya ziwa?issue hapo ni kurejesha mzigo kwa mwenyewe kama kweli sual la uichumi wako si muhimu
 
Wakuu, mimi kijana wa Kanda ya Ziwa nipo hapa Dar kwa takriban wiki ya pili sasa. Leo katika kuzungukazunguka yangu usiku huu wakati narejea kulala majira ya saa mbili hivi nimeokota pochi yenye kiasi kikubwa hivi cha pesa pamoja na driving license maeneo ya ilala katika flat za wanajeshi kwenye njia inayochepukia kuelekea Kigogo.

Kwanza nimewaza sana iwapo hii ni bahati au lah! Nikajiuliza mara mbili mbili, baadae moyo ukaniambia kuwa mwenye huo mzigo yawezekana nae ana matatizo yake na hiyo pesa ndo alikuwa anaitegemea sana, kwa kuwa mimi kidogo nipo vizuri kiuchumi nimeona ni bora nitangaze, kwa yeyote aliyepoteza aniPM na aeleze jina lake kama lilivyo kwenye license na aseme kiasi halisi cha pesa, kisha tuonane nimpatie mzigo wake.

Warning: Kama huhusiki tafadhali pita sitaki usumbufu wala kejeli, heshima ni kitu cha bure.
Imenitisha kidogo sentensi nilioipigia mstari, inamaana kama hali yako ingekuwa mbaya ungekula jiwe sio na kula hiyo bingo????. Hata hivyo hongera kwa moyo wako wa huruma
 
Wakuu, mimi kijana wa Kanda ya Ziwa nipo hapa Dar kwa takriban wiki ya pili sasa. Leo katika kuzungukazunguka yangu usiku huu wakati narejea kulala majira ya saa mbili hivi nimeokota pochi yenye kiasi kikubwa hivi cha pesa pamoja na driving license maeneo ya ilala katika flat za wanajeshi kwenye njia inayochepukia kuelekea Kigogo.

Kwanza nimewaza sana iwapo hii ni bahati au lah! Nikajiuliza mara mbili mbili, baadae moyo ukaniambia kuwa mwenye huo mzigo yawezekana nae ana matatizo yake na hiyo pesa ndo alikuwa anaitegemea sana, kwa kuwa mimi kidogo nipo vizuri kiuchumi nimeona ni bora nitangaze, kwa yeyote aliyepoteza aniPM na aeleze jina lake kama lilivyo kwenye license na aseme kiasi halisi cha pesa, kisha tuonane nimpatie mzigo wake.

Warning: Kama huhusiki tafadhali pita sitaki usumbufu wala kejeli, heshima ni kitu cha bure.

i dont buy this

unataka uonekane kuwa wewe ni mwema, halafu uko vizuri kiuchumi ili uwatege kina dada humu
 
Kati ya mambo yanayodhalilisha nchi hii ni watu kushindwa kutunga hadithi za kusisimua. Kuanzia bongo movie, mtu akiziangalia dk 5 za mwanzo anaweza kupredict matukio yote mpaka mwisho!

Mtu mzima anatunga hadithi hata mtoto mdogo anajua huu ni uongo wa wazi. Ukisoma hadithi kwenye vitabu vya shule za msingi utaelewa kwa nini watu wanamaliza la 7 bila kujua kusoma na kuandika.

Watoto wanajifunza kirahisi kwa hadithi za kuvutia na kusisimua sio viroja vya kina wiseboy!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom