Aliyekuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari na Willy Qulwi Qambalo wa Karatu wajiunga CCM na kupokelewa na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa

Anatoka mtu CCM mnampa ticket ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mnawaacha wanachama wenu waliokitengeneza chama mpaka hapo kilipofikia, mtu anahamia leo kesho mnampa aipeperushe bendera ya chama kwenye mbio za Urais, mtu hata chama hakijui
Angalia Sura Zao Hawajapenda Mamluki Kuvamia Chama Chao..anatoka Mtu upinzani anaingia CCM anakuwa balozi,naibu Waziri,mkuu wa wilaya na Das wao vijana wa ccm wapo wanasugua mabenchi kwenye vijiwe vya kahawa hata bendera za chama hawataki kupandisha wanawaachia Wafungwa.
 
I am sure CHADEMA walishajua huyu hawanaye tena kitambo sana. Ukwepaji wa makusudi wa vikao vya Bunge ilikuwa ni strategy yake ila cha kushangaza sana CHADEMA waliendelea kumtetea.
 
Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki kupitia Chadema, Joshua Nassari na mbunge wa sasa wa Karatu,
Willy Qulwi Qambalo wameondoka rasmi ndani ya chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Wamepokelewa na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa pamoja na viongozi wengine wa Chama mkoa wa Arusha.

Nasari amekishukuru CHADEMA kwa kumlea tangia akiwa mdogo na sasa ameamua kutumikia nchi yake na sina nia ya kugombea nafasi yoyote, kilichopo mbele yake ni kumsaidia Rais John Magufuli.


View attachment 1500808
Joshua Nassari nakiwa na Willy Qulwi Qambalo​


Hongera sana waache nafasi kwa wengine
 
Hata mnyika ni swala la muda ama hata aki last mjue tu ni pandikizi kama mashinji
 
CCM bado lazima kujiuliza sana,hasa wanachama wake,why wote wanaotoka opposition wanapewa post haraka na wanasisiemu wanabaki kushangilia......inamaana sisiemu hakuna wenye uwezo wa kuwa madc,RC,Ded na madas?
Kwa ukilaza walio nao hata hiki unacho wastua bado hawawezi kukuelewa.

Kule imejaa mizigo, si unaona hata meko anawatumbua kwa mipasho baadae anarudia matapishi yake sababu hamna wenye nafuu.

Kuna mawaziri mizigo - by Kinana, by then he was General Secretary ccm.
 
Anatoka mtu CCM mnampa ticket ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mnawaacha wanachama wenu waliokitengeneza chama mpaka hapo kilipofikia, mtu anahamia leo kesho mnampa aipeperushe bendera ya chama kwenye mbio za Urais, mtu hata chama hakijui




Mbona wewe wenzio wanapewa UDC lakini wewe unabaki kupewa T.shirt na kofia.
 
Vijana wa CCM wameshtuka, wamevumilia mengi lakini now wapinzani wanye uchu wa madaraka wanaona pakukimbilia ccm
 
Katika jambo ambalo Upinzani hauta fanikisha kufikia malengo yao hapa nchi ni udhaifu wa viongozi wao.
Mboe mwenyewe kila kukicha anabembeleza siasa ya Maridhiano kwenye meza kuu na katika sherehe za ccmm.
Licha kupigwa, kuumizwa, kufungwa, nk bado analilia mariadhiano.
Kwani amekosea nini na lini ?

Upinzani ninaouona kwamba una.msimamo japo kidogo ni wa Maalim Seif, aliyeanza na CUF na sasa ACT Wazalendo.
Hawa akina Mbowe, Lipumba, sijui Mbatia ni mambo ya Ajira tu.
Mwakani Wabunge wote wa Chadema watahamia CCM, pamoja na Mwenyekiti wao Mbowe.
Ni walewale. Yaani.
 
Kama hawamtaki waondoke wao,Hawajui kama huo usajili umeigharimu chama pesa nyingi..
 
Ndio hivyo Dada utulize mpira, wakihama kutoka Chadema kwenda CCM wanapewa uDas na wakihama toka CCM kwenda Chadema wanapewa ticket ya kuwa mgombea urais, so usiteseke
Mbona wewe wenzio wanapewa UDC lakini wewe unabaki kupewa T.shirt na kofia.
 
Nasaruu ni mfano wa vijana wapumbavu wa nchi hii!! wakati vijana kwa mamilioni wakiteseka na njaa na ukosefu wa ajira yeye akapata ajira kubwa nchi hii inayolipa ya ubunge!! akaidharau akapuuza kuhudhuria vikao wakamtupia virago!

bahati haiji mara mbili!! huyu amekwisha habari yake!! hana mvuto tena hana maajabu!!

kwanza alipata demu wa kizungu aliempenda sana eti lilivyo jinga likamtosa kwa kujaa kiburi cha ubunge pumbavu kabisa huyu kijana!!
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Back
Top Bottom