Aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho Jimbo la Buchosa, Jaji Tasinga arejea CCM

elivina shambuni

JF-Expert Member
May 31, 2018
461
295
1574085788411.png


CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),kimeendelea kupata pigo baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho Jimbo la Buchosa, Jaji Tasinga kutangaza kurejea CCM Tasinga ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa muda wilaya ya Sengerema, alisema sababu mojawapo iliyomsukuma kuondoka Chadema na kurejea CCM ni mazingira ya kisiasa.

Amesema awali akiwa ndani ya CCM mwaka 2015 alikumbana na dhahama kwa familia yake kupewa misukosuko kutokana na sababu za kisiasa zilizosababishwa na baadhi ya watu wilayani humo. “Nilikuwa najaribu kuomba msaada wa viongozi wa CCM lakini hawakunisikiliza licha ya kwamba alikuwa mtu mmoja tu alikuwa akiitikisa sana familia yangu ndio nikaamua kuhamia Chadema,” amesema.

Tasinga ambaye kabla ya kuhamia Chadema mwaka 2015, aliwahi kuwa Mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo ya Sengerema, alipokelewa jana na wajumbe wa Mkutano wa Jimbo uliokuwa umeitishwa na Mbunge wa Jimbo hilo, Dk Charles Tizeba katika kijiji cha Nyehunge.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mkutano huo, Tasinga alisema anamshukuru kada wa CCM mkoani Mwanza, Eric Shigongo kwa kumtia moyo na kuona umuhimu wa kurejea ndani ya chama hicho. Pia aliwashukuru Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Sengerema Agustino Makoye , Mwenyekiti wa UWT Constancia Faida na Mzee John Maduka kwa kuunga mkono kurudi kwake CCM.

Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Salum Kalili alishukuru kurejea kwa Tasinga na kubainisha kuwa baada mkutano kumalizika atazungumza kwa kina kuhusu mapokeo ya kiongozi huyo. Tasinga alikuwa Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya yaSengerema kwa muda wa miaka 10 kuanzia 1998 hadi 2008, Mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo kuanzia mwaka 2007 hadi 2012 kabla ya kuhamia Chadema mwaka 2015.
 
.... wacha arudi nyumbani, but nimpongeze kidogo angalau yeye kajitahidi kuvumilia mpaka mwaka wa nne, wenzake walikimbia toka mwaka wa kwanza!

NB. lile wimbi la kukimbilia nyumbani soon litarejea tukielekea 2020.

#get ready!
 
Najaribu kuwaza huyo mbunge aliempokea kajisikiaje kutokuwepo kwenye Acknowledgment (sijui ndo Dibaji kwa Kiswahili), wametajwa wengine tu.
Kilichonifanya niwaze zaidi ni kutajwa kwa Ndugu Erick Shigongo, tena kapewa sifa kuwa ndie kada wa CCM aliemtia moyo na kumshawishi kurejea ndani ya CCM, ikumbukwe Shigongo amehusishwa mara kadhaa kulitaka jimbo hilo, je hii sio dalili ya kupanga safu ya mashambulizi dhidi ya Tizeba huyohuyo aliempokea Jaji Tasinga?
 
Back
Top Bottom