Aliyekuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari na Willy Qulwi Qambalo wa Karatu wajiunga CCM na kupokelewa na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa

mbinguni

JF-Expert Member
Jan 2, 2013
2,746
1,051
Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki kupitia Chadema, Joshua Nassari na mbunge wa sasa wa Karatu,
Willy Qulwi Qambalo wameondoka rasmi ndani ya chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Wamepokelewa na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa pamoja na viongozi wengine wa Chama mkoa wa Arusha.

Amesema kuwa haikuwa kazi rahisi hata kidogo kufanya hayo maamuzi na akasema kuwa amekwenda Chama Cha Mapinduzi mchana kweupena si usiku kwa sababu moja tu, anachokifanya na alichokuwa anafanya ni swala lililowazi lenye mwanga na la kuelekeza.

Amesema kuwa hakwenda kuzunguza na wao kwa kuwa wamevaa kijani labda kuna kitu anataka hapana ila ni kwa sababu anaipenda nchi yake amesema angeamua kubaki huko duniani atengeneze pesa au kuitunza familia yake na afanye kazi akiwa huko duniani, wamsome kwenye magezati ya kimaaifa akiwa huko angeweza.

Nasari amekishukuru CHADEMA kwa kumlea tangia akiwa mdogo na sasa ameamua kutumikia nchi yake na sina nia ya kugombea nafasi yoyote, kilichopo mbele yake ni kumsaidia Rais John Magufuli.

Siku zote nafanya siasa za kiungwana. Nimeshawaandikia barua Chadema na kiukweli naishukuru Chadema ilinichukua nikiwa mdogo wakanisikiliza wakaona kuna potential ndani yangu. Nawashukuru kwa kunilea nitakuwa mjinga kama sitoikumbuka historia." - Joshua Nassari

qambalo.jpg

Joshua Nassari nakiwa na Willy Qulwi Qambalo​

Sasa ndio nimeamini, kumbe ile strategy yake ya kuwa mtoro bungeni ilikuwa "project" waliyoitengeneza ili akimbie Chadema.

Nilidhani kajamaa kameishia tu kuwa na sura ya kitoto, kumbe mpaka akili, binafsi nilimshangaa sana kwa lile kosa la kitoto alilofanya wakati ule, kumbe alitumwa.
 
Sasa ndio nimeamini, kumbe ile strategy yake ya kuwa mtoro bungeni ilikuwa "project" waliyoitengeneza ili akimbie Chadema.

Nilidhani kajamaa kameishia tu kuwa na sura ya kitoto, kumbe mpaka akili, binafsi nilimshangaa sana kwa lile kosa la kitoto alilofanya wakati ule.
Acha hasira, si mlikuwa mnaulizia lile kundi litalojiunga Ccm hamlioni? Subirini muone wanavyohama.
 
Kuna taarifa kwamba mtajwa hapo juu anapokelewa muda huu CCM mkoa Arusha sasa hivi. Mdau yeyote mwenye taarifa rasmi aiweke hapa.

View attachment 1500768
View attachment 1500769

=======

Joshua Nassari ameanza kwa kuwasalimia wana CCM kwa salamu ya chama “CCM OYEEE” na kusema kuwa hakuwa waza kama kuna siku angesema maneno hayo.

Back
Top Bottom