Uchaguzi 2020 Je, Wabunge Waliojiuzulu na kuhama vyama vyao vya Upinzani, Wataweza kutetea nafasi zao kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2020?

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,494
54,906
Wakuu Salaam.

Kwenye bunge la kumi na moja, na ndani ya Serikali ya awamu wa Tano, Viongozi Wakuu wa Vyama vya Upinzani na Baadhi ya Wabunge, Wamehamia Chama cha Mapinduzi, kwa kile walichosema ni kuunga mokono Juhudi za rais Magufuli katika kuletea Maendeleo Tanzania.

Wabunge Wengi wa Upinzani Walijiuzulu kwenye vyama vyao na Ubunge na kisha kugombea Kupitia CCM na kushinda na kufanikiwa kurudi Bungeni chini ya Mwamvuli wa chama kingine.

Kuna wengine Wamejitoa kwenye vyama vyao wakati bunge linaisha ili Wakagombee kupitia CCM.

Je, Watafanikiwa kupenya na Kurudi Bungeni kwa Tiketi ya CCM?

1. Hivi karibuni Mbunge wa Ubungo, aliyemaliza muda wake, Saed Kubenea alijiondoa ndani ya CHADEMA na kujiunga na chama cha ACT-Wazalendo leo na kupokelewa na Mwenyekiti Maalim Seif Sharif Hamad. Je, atafanikiwa kushinda Ubunge kupitia ACT Wazalendo na Kurudi Bungeni? Aliyekuwa Mbunge wa Ubungo kupitia CHADEMA, Saed Kubenea amejiondoa ndani ya chama hicho na kujiunga na ACT-Wazalendo

2. Aliyekuwa Mbunge wa Kilombero, Peter Ambrose Lijualikali (35), alijiondoa kwenye Chama chake cha Chadema, Wakati bunge likiendelea. Lijualikali alitangaza kuondoka Chadema, tarehe 18 Mei 2020 na kujiunga CCM. Hali hii ilitokea baada ya kuwepo mvutano kati yake yeye na Chama chake. Mbunge Lijualikali alia bungeni kwa unyanyasaji anaofanyiwa na Mbowe ajiuzulu ubunge amuomba Ndugai CCM wampokee

3, Julius Kalanga aliyekuwa Mbunge wa Monduli, aliondoka Mwenyewe ndani ya chama kwa kile alivhodai ni kufurahishwa na kazi anazofanya rais Magufuli. Katika Uchaguzi wa Marudio aliweza kushinda kupitia CCM na kurudi Bungeni. Je Uchaguzi mkuu wa 2020 ataweza kurudi kupitia CCM? Elections 2015 - Mbunge wa Jimbo la Monduli, Julius Kalanga (CHADEMA), ajiuzulu na kuhamia CCM

4. Ryoba Marwa aliyekuwa Mbunge wa Serengeti kwa tiketi ya CHADEMA, alijiuzulu ubunge na kujiunga CCM kwa alichodai ni kuunga Juhudu za Rais Magufuli na baadaye kwenye Uchaguzi wa Marudio akafanikiwa Kurudi Bungeni. Je, Uchaguzi Mkuu wa 2020, CCM watamrudisha tena? MARA: Mbunge wa Serengeti(CHADEMA), Mwl Marwa Ryoba Chacha ajivua uanachama na kujiunga CCM

5. Joseph Mkundi aliyekuwa Mbunge wa Ukerewe kupitia CHADEMA, alijiuzulu Ubunge na kujiunga CCM ambapo Uchaguzi wa Marudio alifanikiwa Kurudi Bungeni. Je Uchaguzi Mkuu 2020 atafanikiwa kurudi kupitia CCM? Mwanza: Mbunge wa Ukerewe, Joseph Mkundi(CHADEMA) ajiuzulu Ubunge

6. James Ole Millya alikuwa Mbunge wa Simanjiro kupitia CHADEMA, aliunga Juhudi na kujiunga CCM baada ya Kujiuzulu Ubunge. Je, Uchaguzi Mkuu 2020 atafanikiwa Kurudi Bungeni kwa tiketi ya CCM? Mbunge wa Simanjiro, James Ole Millya(CHADEMA) ajiuzulu Ubunge na kujivua uanachama, ahamia CCM

7. Pauline Gekul alikuwa Mbunge wa Babati Mjini Kupitia CHADEMA, alijiuzulu Ubunge na kujiunga CCM kuunga mkono Juhudi za Rais Magufuli. Je Uchaguzi Mkuu wa 2020 ataweza kurudi Bungeni kwa tiketi ya CCM? Pauline Gekul, Mbunge wa Babati Mjini(CHADEMA) ajiuzulu na kujivua uanachama, ajiunga na CCM

8. Mwita Waitara alikuwa Mbunge wa Ukonga kwa Tiketi ya CHADEMA , akaunga Juhudi za Magufuli na Kurudi CCM. Uchaguzi wa Marudio alifanikiwa kushinda na kupewa Unaibu Waziri Wizara ya Elimu. Je, atafanikiwa kududi kupitia CCM? Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara(CHADEMA) ajiuzulu na kuhamia CCM

9. Dk Godwin Mollel alikuwa Mbunge wa Siha kupitia CHADEMA aliunga Juhudi na Uchaguzi wa Marudio akashinda Ubunge kwa tiketi ya CCM na kufanikiwa kupata Unaibu Waziri wa Afya. Je, ataweza kurudi Bungeni kwa Tiketi ya CCM Uchaguzi Mkuu wa 2020? Mbunge wa Jimbo la Siha, Godwin Aloyce Mollel(CHADEMA) ajivua wadhifa huo na kuhamia CCM

10. Anthony Komu, aliyekuwa mbunge wa Chadema katika jimbo la Moshi Vijijini Chadema alijiondoa kwenye chama chake na kujiunga na NCCR- Mageuzi. akasema, atabaki Chadema hadi kumalizika kwa muda wa ubunge wake na kwamba watagombea tena nafasi hiyo kupitia NCCR. Je Uchaguzi Mkuu wa 2020 atafanikiwa kurudi bungeni? Mbunge wa Moshi Vijijini, Anthony Komu (CHADEMA) kuhamia NCCR-Mageuzi

11. Joseph Selasini, aliyekuwa mbunge wa Rombo, alitangaza kuondoka Chadema na kujiunga na NCCR- Mageuzi. akasema, atabaki Chadema hadi kumalizika kwa muda wa ubunge wake na kwamba atagombea tena nafasi hiyo, kupitia chama hicho kipya cha NCCR Mageuzi. Je Uchaguzi Mkuu wa 2020 atafanikiwa kurudi bungeni? Mbunge wa Rombo, Joseph Selasin kuondoka CHADEMA na kujiunga NCCR Mageuzi

11. Joshua Nassari, alikuwa mbunge wa Arumeru Mashariki, alipoteza Ubunge kwa kuvuliwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai. Spika Ndugai alisema, Nassari amepoteza sifa za kuwa mbunge kwa kuwa amekuwa “Mtoro bungeni.” Uchaguzi ulipotangazwa wa Arumeru Mashariki, Chadema na baadhi ya vyama vya upinzani havikushiriki vikidai mazingira ya uchaguzi si sawa; hivyo mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Pallangyo akashinda. Baadae Nassari aijiunga CCM July 2020 na kutangaza Kugombea Arumeru Mashariki Kupitia CCM. Je, atafanikiwa Kushinda na kurudi CCM? Aliyekuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari na Willy Qulwi Qambalo wa Karatu wajiunga CCM na kupokelewa na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa

12, Cecil Mwambe aliyekuwa mbunge wa Chadema katika jimbo la Ndanda, yeye alitangaza kuondoka chama hicho, tarehe 15 Februari 2020 na kujiunga na CCM. Je, atafanikiwa Kushinda Uchaguzi Mkuu wa 2020 na kurudi Bungeni? Mbunge wa Ndanda, Cecil Mwambe ajivua uanachama wa CHADEMA na kujiunga CCM

KUNA WABUNGE WA CHADEMA WALIOFUKUZWA NA CHAMA:

Chadema ilichukua uamuzi huo kufuatia uamuzi wa wabunge hao, kuhudhuria mkutano wa Bunge, kinyume na kile kilichodaiwa, kutotekeleza “maelekezo ya viongozi.” Wabunge wanne - Anthony Komu, Joseph Selasini, David Silinde na Wilfred Lwakatare wafutwa uanachama wa CHADEMA

Ni mkutano huo huo wa Kamati Kuu, ndio umefikia maamuzi ya kuwafukuza

13. David Silinde ambaye amejiunga CCM na kutangaza nia ya Kugombea Ubunge kupitia CCM mwenye jimbo Tunduma,Je, atweza rudi Bungeni? Mbunge wa Momba, David Silinde rasmi ahamia CCM

14. Willfred Lwakatare, mbunge wa Bukoba Mjini alikuwa kashatangaza hatagombea, lakini alipofukuzwa Alijiunga na chama chake cha Zamani cha CUF. Je, Akiamua kugombea Ubunge, ataweza kurudi Bungeni kwenye Uchaguzi Mkuu 2020? Wilfred Lwakatare arejea CUF baada ya kufutwa uanachama CHADEMA. Kutumika kuiangamiza CHADEMA

WABUNGE WA CUF WALIOHAMA VYAMA

15, Said Mtulia aliyekua Mbunge wa Kinondoni kwa tiketi ya CUF aliunga Juhudi za rais Magufuli na kujiunga CCM Mbunge wa Kinondoni, Maulid Mtulia(CUF) ajivua uanachama na ubunge na kuhamia CCM

16. Aliyekuwa Mbunge wa Temeke kwa tiketi ya CUF, Abdallah Mtolea, alitangaza kujivua uanachama wa chama hicho na kujiuzulu ubunge kisha akajiunga CCM Mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea atangaza kujiuzulu Ubunge na uanachama wa CUF

17. Mbunge wa Liwale kupitia CUF, Zubeir Kachauka alijivua ubunge wake na uanachama wake na kujiunga na CCM Dar: Mbunge wa jimbo la Liwale(CUF) Zuberi Kuchauka atangaza kujiuzulu na kuhamia CCM

18. Mbunge wa Tandahimba Mkoani Mtwara (CUF) Katani Ahmed Katani amejiuzulu Ubunge wake na kutangaza kuhamia CCM

19. Juma Hamad Omari Mbunge wa Jimbo la Ole, Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba Zanzibar kwa tiketi ya CUF alijiuzulu CUF na kuomba kujiunga na CCM Pigo jingine kwa CUF, Zanzibar; Mbunge wa Ole ajivua vyeo vyote na kuomba kujiunga CCM

WABUNGE WENGINE 20 WA CUF, BAADA YA BUNGE KUISHA MUDA WAKE, WALIACHANA NA CUF KISHA KUJIUNGA NA ACT WAZALENDO. JE WATATETEA NAFASI ZAO KWENYE UCHAGUZI MKUU 2020?

WALIOHAMIA ACT NI:


19. Ndugu Suleiman S Bungara wa jimbo la Kilwa Kusini

20. Ndugu Juma Kombo Hamad wa Jimbo la Wingwi

21. Ndugu Masoud Abdallah Salim wa Jimbo la Mtambile

22. Ndugu Ally Saleh Ally Albator wa Jimbo la Malindi

23. Ndugu Ali Salim Khamis wa Jimbo la Mwanakwerekwe

24. Ndugu Hamad Salim Maalim wa Jimbo la Kojani

25. Ndugu Khalifa Mohamed Issa wa Jimbo la Mtambwe

26. Ndugu Mohamed Juma Khatib wa Jimbo la Chonga

27. Ndugu Twahir Awesu Mohamed wa Jimbo la Mkoani

28. Ndugu Khatib Said Haji wa Jimbo la Konde

29. Ndugu Haji Khatib Kai wa Jimbo la Micheweni

30. Ndugu Othman Omar Haji wa Jimbo la Gando

31. Ndugu Dr. Suleiman Ali Yussuf wa Jimbo la Mgogoni

32. Ndugu Mbarouk Salim Ali wa Jimbo la Wete

33. Ndugu Nassor Suleiman Omar wa Jimbo la Ziwani

34. Ndugu Yussuf Salim Hussein wa Jimbo la Chambani

35. Abdallah Haji Ali wa Jimbo la Kiwani

36. Ndugu Yussuf Haji Khamis wa Jimbo la Nungwi

37. Ndugu Mohamed Amour Mohamed wa Jimbo la Bumbwini

38. Ndugu Mgeni Jadi Kadika wa Mbunge Viti Maalum

Soma: News Alert: - Kuelekea Uchaguzi Mkuu: Chama cha ACT-Wazalendo chapokea Wabunge 21 waliokuwa Wabunge wa CUF

Sababu za kuhama ni kutokana na Migogoro ndani ya CUF. Je, Wataweza Kutetea nafasi zao za ubunge?
 
figganigga, Aisee mambo ni moto ila kwa haraka haraka kuna ambao tayari wameshakosa nafasi ya kurudi bungeni 99% mf. Nassari hana chake, Silinde hana chake Dr. Godwin hana chake etc
 
figganigga, Aisee mambo ni moto ila kwa haraka haraka kuna ambao tayari wameshakosa nafasi ya kurudi bungeni 99% mf. Nassari hana chake, Silinde hana chake Dr. Godwin hana chake etc
Kwa taratibu za CCM, kura za Maoni haimanishi mtu kapitishwa. Unaweza Ukashinda na Usipitishwe.
 
Back
Top Bottom