Alichopost Mel Gibson katika mtandao wake wa kijamii

Alichopost Mel Gibson katika mtandao wake wa kijamii

Mkuu vyovyote utakavyopamba lakini sio neno la kistaarabu kwenye kujenga hoja
Ujinga = kutokujua kitu.

Hili ni neno descriptive.

Ustaarabu maana yake si kutoita ujinga kwa jina lake halisi la ujinga.

In fact, ukianza kukataa kuuita ujinga kwa jina lake ujinga, hapo ndipo unakosa ustaarabu.

Unaukumbatia ujinga, unaupamba ujinga, unaurembaremba ujinga, kwa kisingizio cha ustaarabu.

Huo si ustaarabu.

Ni kukosa ustaarabu.
 
Mimi nakataa hadithi ya mwanzo wa dunia ya Wayahudi.

Unaniitaje kuwa nimedanganywa na Zionist propaganda?

Of course you can't argue with me.

You do not have an argument.

You resort to ad hominem attacks. Logical fallacy.

Badala ya kujadili hoja, unamshambulia mtoa hoja.

Kwa sababu huna hoja.
Not all Jews are Zionist
 
The Problem of Evil.

1. Mungu anayesemwa yupo ana tabia za kuwa na uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote.

2. Mungu mwenye tabia hizo, kimantiki, yuko mutually exclusive na ulimwengu unaoruhusu mabaya kuwepo.

3. Ama Mungu huyo yupo, na ulimwengu unaoruhusu mabaya haupo. Ama ulimwengu unaoruhusu mabaya upo, na Mungu huyo hayupo. Viwili hivi, Mungu huyo na ulimwengu unaoruhusu mabaya, haviwezi kuwa vyote vipo.

4. Tunaona kwamba ulimwengu unaoruhusu mabaya upo, ndio huu tunaoishi.

5. Hivyo, Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.

Uwepo wa Mungu huyo na ulimwengu huu unaoruhusu mabaya ni contradiction. Contradiction hii haitatuliki na inatuonesha Mungu huyo hayupo.

Huyo Mungu yupo kwenye hadithi za kutungwa na watu tu, nje ya hizo hadithi za kiimani hayupo.
Kweli akili sio maarifa.
 
Madhehebu kwa leo utajichosha tu kikubwa ni kumjua Mungu, na kuelewa mambo namna yalivyo.
Biblia Matendo ya mitume

27 Naye akaondoka, akaenda; mara akamwona mtu wa Kushi, towashi, mwenye mamlaka chini ya Kandake malkia wa Kushi, aliyewekwa juu ya hazina yake yote; naye alikuwa amekwenda Yerusalemu kuabudu,
28 akawa akirejea, ameketi garini mwake akisoma chuo cha nabii Isaya.
29 Roho akamwambia Filipo, Sogea karibu na gari hili, ukashikamane nalo.
30 Basi Filipo akaenda mbio, akamsikia anasoma chuo cha nabii Isaya; akanena, Je! Yamekuelea haya unayosoma?
31 Akasema, Nitawezaje kuelewa, mtu asiponiongoza? Akamsihi Filipo apande na kuketi pamoja naye.
32 Na fungu la Maandiko alilokuwa akilisoma ni hili, Aliongozwa kwenda machinjoni kama kondoo, Na kama vile mwana-kondoo alivyo kimya mbele yake amkataye manyoya, Vivyo hivyo yeye naye hafunui kinywa chake.
33 Katika kujidhili kwake hukumu yake iliondolewa. Ni nani atakayeeleza kizazi chake? Kwa maana uzima wake umeondolewa katika nchi.
34 Yule towashi akamjibu Filipo, akasema, Nakuomba, nabii huyu; asema maneno haya kwa habari ya nani; ni habari zake mwenyewe au za mtu mwingine?
35 Filipo akafunua kinywa chake, naye, akianza kwa andiko lilo hilo, akamhubiri habari njema za Yesu.
Usiniletee hizo hekaya za wayahudi nipe dhehebu la Ethiopia likowapi nikasali kama dini hapa bongo imetokea kwa waafrika wenzetu Ethiopian nipeleke kanisani kwao
 
Kwa kifupi hujapata Neema ya kushudia Ukuu wa Mungu.

Hivyo vyote ulivyovitaja mwanadamu yeyote anaweza kwa juhudi binafsi hata na kuzidi.

Mimi sikupingi wala sikulaumu.

Lakini kwangu nimepata yale usiyoweza kamwe kuyapata kwa juhudi binafsi wala Elimu bali kwa uweza wa Mungu.

I wish siku moja tukae meza moja tufanye mjadala naweza kukueleza kila kitu.

Mimi mvivu sana kuandika
Mfate NyuYoku...mjungumje...
 
Mfate NyuYoku...mjungumje...
Ananiambia sijapata neema ya kushuhudia ukuu wa Mungu.

Yani huyo Mungu mchoyo hivyo aninyime neema ya kushuhudia ukuu wake?

Habari nzima ya Mungu kuwapa watu fulani neema ya kushuhudia ukuu wake, na kuwanyima wengine neema hiyo, inaonesha contradiction.

Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote angekuwepo, angetoa neema sawa kwa kila mtu ajue ukuu wake, wote tungemjua, kusingewezekana kuwapo na mjadala kuhusu uwepo wa Mungu.

Kwa sababu wote tungepata neema sawa ya kujua yupo, bila utata wowote.

Ukishasikia habari kwamba kuna watu wamefunguliwa neema ya kujua uwepo na ukuu wa Mungu, halafu wengine hatujafunguliwa, hapo ujue hakuna Mungu.

Kuna siasa za longolongo za watu tu.
 
Wanasema mwenye nacho huongezewa....huyu Mungu wao mchoyo sana.... Kama hauna unanyimwa kabisa.... Anawaumba wengine mteseke wakati Taifa lake ni Israel sisi wengine wabondei sijui ni WA Mungu yupi....
 
Aah, huyu Mungu ukimuweka kwenye mizani ya kimantiki unaona kabisa katungwa na watu tu, hayupo kwenye uhalisia.

Eti Mungu anakasirika, anapendelea watu wake, ana wivu, anawalipizia kisasi watoto kizazi na kizazi kwa makosa ambayo hawajayafanya wao.

Yani zile zile tabia za watu, watu wamempa Mungu.

Wanasema Mungu kaumba watu kwa mfano wake.

Wakati ukweli ni kuwa watu wamemuumba Mungu kwa mfano wao.
 
hayo ni mawazo yako bado sijaona point hapo siku njema
Inawezekana hata hujui point ni nini kwa sababu tupo dunia tofauti sana.

Kama hujui "The Problem of Evil" ni nini hata baada ya kutafsiriwa, naona hatuna cha kujadiliana.
 
Back
Top Bottom