Alama ya nyota na mwezi misikitini humaanisha nini?

Alama ya nyota na mwezi misikitini humaanisha nini?

ibrahim huyu ni nabii wa ALLAH ambaye alioteshwa kumchinja mwanaye ismail
Tafadhli, Soma maelezo yangu vizuri na ujibu kwa evidence ili tufikie muafaka. Jibu lako halijitoshelezi wala halijajibu hoja yangu
 
  • Thanks
Reactions: PNC
SURAT ASH-SHAMS 1-3
1. Naapa kwa usiku ufunikapo, 2 kwa mchana uingiapo, 3. na kwa aliye umba kiume na kike..

Hivi mtu anaye apa kwa mwengine anakuwa Mungu au binadamu? Je, nani kaumba hapo. Maana Allah anaapa katika aliye umba, na kuumba ni sifa ya Mungu. Kumbe Allah ambaye sie Yehova hakuumba.

Zaidi ya hapo, Allah anaapa kwa usiku. Kumbe usiku una mamlaka zaidi ya Allah. Allah anaapa kwa mchana, kumbe mchana una mamlaka zaidi ya Allah.

Mbona katika SURAT ASH-SHAMS Allah anaapa kwa (1) Usiku (2) Mchana (3) kwa aliye umba kiume na kike?

Je, ni nani huyu aliye umba Kiume na Kike ambaye Allah wa Islam anaapa kwake? Endelea kusoma...kutoka Biblia Takatifu….

Yeremia 27: 5 Mimi nimeiumba dunia hii, wanadamu na wanyama walio juu ya uso wa nchi, kwa uweza wangu mkuu, na kwa mkono wangu ulionyoshwa; nami nawapa watu kama inipendezavyo.

Sasa tunamsoma Yehovah ambaye ni Mungu wa Biblia kuwa yeye ndie aliye umba kila kitu, pamoja na Kiume na Kike ambacho Allah wa Islam anaapa kwake. Kwahiyo, Jehovah aliumba kiume na kike, na Allah wa Islam anaapa kwake, sasa jaza mwenyewe nani ni Mungu?

Je, Mungu anaweza kuapa kwa Mwengine? Endelea kupata elimu …

Waebrania 6:13 Mungu alipompa Abrahamu ahadi, aliapa kwa jina lake mwenyewe, maana hakuna aliye mkuu kuliko Mungu ambaye kwa huyo angeweza kuapa.

Jehova anasema hakuna Mkubwa wangu wa kuapa kwake, lakini Allah katika Kuran anasema kuwa yeye anaapa kwa aliye umba kiume na kike.
Hii inaonesha Allah siyo Mungu,maana anaapa kwa aliyeumba kike na kiume, no nani aliyeumba kike na kiume huyo ndio Mungu yaani Yehova
 
  • Thanks
Reactions: PNC
sio baba yao ibrahim watoto wake ni ismail na ishaq tu qur,an ilikuepo mbinguni ALLAH kaihifadhi katika kitu kinaitwa lauhu mahfudh ilkua inasubiri muda wa kushuka tu .
Watoto wa Ibrahim ni Isaka na Ishmael aliyezaa na mjakazi wake hajiri. Mimi nilikuwa nakuonesha kuwa Ibrahim hakuwahi kuwa muislam kwa maana ya dini wala hakujenga kaaba arabuni na ushahidi soma post zangu zilizotangulia. Kama unapinga toa maelezo kwa nini unapinga ili tuelewane.
 
  • Thanks
Reactions: PNC
ALLAH yeye anaweza kukiapia chochote katika kiumbe chake kwa sababu yeye ndie mmiliki na hapagwi na yoyote.
Kwa maelezo yako unaweza kuapia hata simu yako maana unaimiliki? elezea kidogo. Maana kiapo huapiwa mkuu kwako mfano Mungu.
 
  • Thanks
Reactions: PNC
kupinga wewe si wa kwanza pia ukitaka kujua uislam ndio dini ya kweli angalia ulaya na america watu wanavyoingia katika uislam
Kuingia kwenye uislam haimaanishi ni ya kweli, maana hata kwenye uchawi,ushirikina,dini ya shetani kwote huko watu huingia ila haimaanishi ni kuzuri. Mimi nilitaka utafute ujue Allah alikuwa mungu wa wapagani na kamwe hawezi kuwa Mungu na Ibrahim
 
  • Thanks
Reactions: PNC
sina sababu ya kutafuta chochote , sababu nikiangalia vitu ambavyo tunatumia na vilivyomo katika hii dunia inatosha kujua ALLAH ndie muumbaji
Mwenye hekima hutafuta maarifa ajue yupo sawa au si sawa. Ni uhuru wako kutafuta au kuacha ila ukweli utabaki.
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Acha upoyoyo na porojo.

Unafikili nina umri gani, nina hela kiasi gani , na kazi ninayofanya, nchi nilizotembea !?
Lugha za kimataifa ninazotumia Kwa ufasaha ni zaidi ya 5 ukiondoa Kiswahili na lugha Mama. Kwa hiyo Mimi siyo kuwa niko gizani bali naelewa vizuri sana upoyoyo na porojo rukuki na uchwara wa dini zote uzijuazo na usizozijua ambazo Mimi nazifahamu.

Nakuzidi wewe kilaza na Wajinga Wenzako wanaojitoa mhanga kila siku.
Halafu wewe unaniambia Mimi kuwa niko gizani na kupotea!?

Nimekwambia, dini zote ni unafiki mtupu na uchwara na Pumba.fu sana.

I was born free, I'm free and I must live free from any obstacles such as religions including; christian, islam, Judaism, budha, hindu, freemason, or local religions or any secret society (s) you many know or not.

I am not a member and I will never ever be a member of any of the above crazy religions yours included.

My parents and my country taught me values, norms and respect, hard work and respect for others without any alignments to any created things including your crazy religions.
Hongera kwa kuona mengi. Ila unafikiri ushajua tote, so kweli. Kuona siyo kujua, kutembea nchi mbalimbali siyo kujua nk. Endelea kujifunza yumkini utaelewa kweli ya unachodharau.
 
Hii inaonesha Allah siyo Mungu,maana anaapa kwa aliyeumba kike na kiume, no nani aliyeumba kike na kiume huyo ndio Mungu yaani Yehova
huyu mkuu nishaona njaa imeanza kumkaba japo saa 11 kala maana nampa na ushahidi wa quran kuwa allah anaapa kwa aliyeumba kike na kiume jamaa bado mbishi
 
Allah alitokea wapi?

Uislamu unajinadi kwamba Allah ndiye Mungu yuleyule aliyejishughulisha ya Wayahudi tokea nyakati za Ibrahimu katika Agano la Kale. Je, jambo hilo ni kweli?

Uislamu ulianza na Muhammad kwenye miaka 600 baada Kristo. Je, kabla yake imani za Waarabu zilikuwaje? Je, yako mambo yoyote kutoka kwenye imani hizo ambayo yaliingia kwenye Uislamu? Kwa maneno mengine, je, Uislamu hauna upagani ndani yake?

Fuatana nami kwenye makala haya marefu yanayochambua chimbuko la Uislamu ili tuweze kuona iwapo upo uhusiano wowote kati ya Uislamu na upagani uliokuwa ukitawala miongoni mwa jamii za Waarabu kabla ya kutokea kwa Muhammad?

Asili Ya Allah

Jamii za wanadamu KOTE duniani zimekuwa na kawaida ya kujiuliza ni wapi ulimwengu huu umetokea, nini maana ya maisha na wapi watu huenda baada ya kufa. Matokeo yake, kila jamii ilifikia kuamini kuwa kuna aliye na nguvu (au walio na nguvu) kuliko wanadamu wote ambao ndio wanapaswa kuabudiwa na kuombwa msaada pale matatizo yanapotokea.

Hawa wenye nguvu wakajulikana kwa majina mbalimbali kwenye jamii tofauti. Vilevile, kila jamii ilianzisha utaratibu maalum wa kuwasiliana na hawa wenye nguvu, yaani miungu.

Lakini jambo moja ni dhahiri, kwamba UKIACHA JAMII YA WAYAHUDI PEKE YAO, jamii zote za wanadamu zilizobakia duniani – iwe ni Afrika, Ulaya, Asia, n.k. - zimeanzia kwenye ibada za kipagani. Jamii hizi ziliabudu miungu mbalimbali. Na miungu hii iliwakilishwa na vitu kama vile milima, miti mikubwa, jua, mwezi, majoka makubwa, sanamu, wafalme, n.k. Kwa mfano, Warumi walikuwa na miungu kama vile artemi, jupiter, minerva, atlas, n.k. Tazama hapa. Wagiriki walikuwa na miungu kama vile chronos, dionysus, eros, ares, appolo, hermes, poseidon, n.k. Tazama hapa. Wahindi wana miungu kama vile durga, ganesha, garusha, brahma, n.k. Tazama hapa. Imani hizi za kipagani ziliweza hata kukua sana na kuenea maeneo mengi. Kwa mfano, imani ya ubudha ni imani ya kipagani lakini iliweza kuenea sehemu kubwa sana ya Asia – India, Japan, Sri Lanka, Uchina, n.k.

Kwa hiyo, jamii za Kiarabu, kama ilivyo kwa wanadamu wengine, vilevile hazikuwa tofauti. Jamii hizi nazo zilikuwa zina ibada zao za kipagani.

Waarabu walikuwa wakiabudu kile ambacho kinajulikana leo kama “star family”, au “familia ya nyota.” Tazama hapa. Inaitwa ‘familia ya nyota’ kwa sababu walichukulia miungu yao kwa tabia za kibinadamu. Mwezi ulichukuliwa kuwa ni mungu mwanamume na jua kama mke wa mwezi. Kisha hawa walizaa watoto. Kwa mfano, waliaminika kuwa walikuwa na mabinti watatu waliojulikana kwa majina ya al-lat, al-uzza na manat.

Ndiyo maana hata quran ikasema: Have you considered Al-Lat and Al- Uzzah, and another, the third (goddess) Manat? (Sura 53:19-20).

Yaani: Mmemwona Al-Lat na Al – Uzza, na mwingine, wa tatu (mungu mke) Manat?

Na hata Muhammad alikuwa akiabudu miungu hii kabla ya kuanzisha Uislamu. Tunasoma kutoka Hisham al-Kalbi, Kitab al-Asnam (Book of Idols), uk.17 kwamba:

'We have been told that the Apostle of Allah once mentioned al-Uzza saying, "I have offered a white sheep to al-'Uzza, while I was a follower of the religion of my people."

Yaani:
Tulishaambiwa kwamba Mtume wa Allah aliwahi kumtaja al-Uzza akisema, “Nilitoa kondoo mweupe kwa al-Uzza, wakati nilipokuwa nikifuata dini ya watu wangu.” Watu wake ni Waquresh.

Jina Allah linatokana na al-llah. Al ni kama neno la Kiingereza, yaani article ‘a’; na ilah ni mungu. Kwa hiyo, al-ilah maana yake ‘a god’ au tu mungu kwa Kiswahili – maana Kiswahili hakina neno linalofanana na ‘a’.

Kwa sababu lugha huenda ikibadilika, ndipo jina hili likafupishwa na akuwa ‘allah’. Ni kama unavyoona kwenye Kiswahili utasikia mtu akisema ‘mambo ndo ivo bwana.’ Kumbe ‘ndo ivo’ ni kifupi cha ‘ndiyo hivyo’. Huenda miaka hamsini au mia ijayo watu hawatajua kuwa kumbe asili ya ‘ndo ivo’ ni maneno ‘ndiyo hivyo.’

Sasa, allah alikuwa ni nani? Allah alikuwa ni mungu mwezi, ambaye tumesema mke wake alikuwa ni jua na watoto (mabinti zao) walikuwa ni al-lat, al-uzza na manat. Hawa ndio walik uwa wakichukuliwa kuwa ni miungu wakuu miongoni mwa mamia ya miungu iliyokuwa ikiabudiwa na Waarabu kabla ya Uislamu – kipindi ambacho Waislamu hukiita ‘Jahiliyah’.

Na jina hili ‘Allah’ ni jina la kiume (masculine); na ndiyo maana binti yake mmoja akaitwa ‘al-lat’, ambalo ni jina la kike (feminine). Ni kama unavyoona Francis na Fortunatus ni wanaume lakini Francisca na Fortunata ni wanawake – japo majina haya asili yake ni ileile. Ndivyo ilivyo kwa Allah na al- Lat. Yote ni jina lilelile, tofauti tu kwamba moja ni la kiume na jingine la kike.

Mojawapo ya jamii iliyokuwa ikimwabudu sana Allah ilikuwa ni jamii ya Waquresh, ambayo ndiyo jamii alikotokea Muhammad.

Watu wasioelewa wanadhani kuwa Allah alijulikana baada ya Muhammad kutokea. Na wengine nao watasema kuwa Allah alijulikana tangu wakati wa Ibrahimu kama anavyojulikana leo. Kama hilo lingekuwa ni kweli, inabidi wajiulize ilikuwaje Allah wa Ibrahimu akapotea hadi ikawa kwamba kuna Allah wa kipagani?

Mathalani, inafahamika wazi kwamba baba yake Muhammad hakuwa mwislamu bali alikuwa mpagani.

Sitashaangaa endapo baadhi ya Waislamu watasema kuwa baba wa Muhammad alikuwa mwislamu. Hata hivyo, huyu mtu alikufa kabla hata ya Muhammad kuzaliwa. Na je, Muhammad mwenyewe anasema nini kuhusiana na baba yake?

Tunasoma hivi:

Anas reported: Verily, a person said: Messenger of Allah, where is my father? He said: (He) is in the Fire. When he turned away, he (the Holy Prophet) called him and said:Verily my father and your father are in the Fire. (Sahih Muslim, Book 001, Number 0398).

Yaani:
Imeripotiwa na Anas: Hakika, mtu mmoja alisema: Mjumbe wa Allah, baba yangu yuko wapi? Akasema: Yuko motoni. Alipogeka kuondoka, (Mtume mtakatifu) akamwita na kusema: Hakika baba yangu na baba yako wako Motoni.

Na swali ambalo tungependa wajiulize ni kuwa, kwa nini baba yake Muhammad, ambaye alikuwa mpagani aliitwa ‘Abdullah’?

Na kwa kuwa ‘Abdullah’ maana yake ni ‘mtumwa wa Allah’, hii ni ishara ya wazi kwamba wapagani wa kipindi cha jahiliyah walikuwa wakimwabudu Allah hadi kufikia kuwapa watoto wao majina kwa heshima ya Allah – kama ambavyo Wayahudi nao walikuwa wakiwapa watoto wao majina kwa heshima ya Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo.

Kwa mfano:
Yoshua – Yahwe ni wokovu;
Yothamu – Yahwe ni mkamilifu;
Yehoahazi – Yahwe ameshikilia;
Hezekia – Yahwe ametia nguvu;
Elisha – Mungu ni wokovu, n.k.

Jibu liko wazi. Allah alikuwa ni mungu wa kipagani aliyeabudiwa kabla ya Uislamu kuja. Na mungu huyu alikuwa ni ‘mungu mwezi’, yaani ‘al-ilah’. Jina lake jingine aliitwa ‘hubal.’ Mungu huyu wa kipagani aliabudiwa kote mashariki ya kati; wala si kwa Waarabu peke yake.

Hili ni jambo ambalo limeshathibitishwa tena na tena na wanaakiolojia – ambao hufukua masalia ya vitu vya kale – hawa wameshafukua vitu vingi sana ambavyo vinaonyesha jinsi kuabudu mwezi na jua na nyota kulivyokuwa kumeshamiri sana katika eneo la mashariki ya kati.

Na ndiyo maana baba yake Muhammad, yaani Abdullah, alikoswakoswa kuchinjwa na babu wa Muhammad, yaani Abdul Muttalib. Abdul Muttalib alitaka kumchinja mwanawe huyo kama sadaka kwa Allah. Lakini mjomba wake Abdullah akamwokoa na hatimaye walichinjwa ngamia 100 badala yake. Na ifahamike kwamba machinjo hayo yalifanyikia kwenye kaaba (hili tutaliangalia huko mbeleni).

Tunaambiwa kwamba:
An arrow showed that it was 'Abdullah to be sacrificed. 'Abdul-Muttalib then took the boy to Al-Ka'bah with a razor to slaughter the boy. Quraish, his uncles from Makhzum tribe and his brother Abu Talib, however, tried to dissuade him. They suggested that he summon a she-diviner. She ordered that the divination arrows should be drawn with respect to 'Abdullah as well as ten camels. … the number of the camels (finally) amounted to one hundred. (Ibn Hisham 1/151-155; Rahmat-ul-lil'alameen 2/89, 90).

Maana yake:

Mshale ulionyesha kwamba Abdullah ndiye aliyetakiwa kutolewa kafara. Kwa hiyo, Abdul Muttalib alimchukua yule kijana hadi kwenye Al-Kaaba pamoja na wembe kwa ajili ya kumchinja. Qura aish, mjomba wake kutoka kabila la Makhzum na kaka yake Abu Talib, hata hivyo, walijaribu kugeuza mawazo yake. Walipendekeza kwamba amwite mwaguzi wa kike. Huyo aliagiza mishale ya uaguzi ichorwe baina ya Abdullah na ngamia kumi … hatimaye idadi ya ngamia ikafikia mia moja.

Ndiyo maana Mungu wa Biblia alikuwa akiwaonya sana wana wa Israeli juu ya tabia za kipagani za jamii zilizowazunguka kuhusiana na masuala ya kuabudu familia ya nyota au jeshi la mbinguni. Kwa mfano, anasema:

….. tena usije ukainua macho yako hata mbinguni, na ulionapo jua, na mwezi, na nyota, jeshi la mbinguni lote pia, ukashawishiwa na kuviabudu, na kuvitumikia, ambavyo Bwana, Mungu wako amewagawanyia watu wote chini ya mbingu zote. (Kumbukumbu la Torati 4:19).

Ikiwa ameonekana katikati yako, ndani ya malango yako mojawapo, upewayo na Bwana, Mungu wako, mtu mume au mke afanyaye yaliyo maovu machoni pa Bwana, Mungu wako, kwa kuvunja maagano yake,….. naye amekwenda kutumikia miungu mingine na kuiabudu, au jua, au mwezi, au vilivyo katika jeshi la mbinguni vyo vyote, nisivyoagiza mimi (Kumbukumbu la Torati 17:2-3).

Kwa maana akapajenga tena mahali pa juu alipopaharibu Hezekia baba yake; akamjengea Baali madhabahu, akafanya Ashera kama alivyofanya Ahabu mfalme wa Israeli. Akajiinama mbele ya jeshi lote la mbinguni na kulitumikia. (2 Wafalme 21:3).

Akajenga madhabahu kwa ajili ya jeshi lote la mbinguni katika behewa mbili za nyumba ya Bwana. (2 Wafalme 21:5).

Akawaondosha wale makuhuni walioabudu sanamu, ambao wafalme wa Yuda waliwaweka ili kufukiza uvumba katika mahali pa juu, ndani ya miji ya Yuda, na katika kila mahali, pande zote za Yerusalemu; na hao pia waliomfukizia uvumba Baali, na jua, na mwezi, na sayari, na jeshi lote la mbinguni. (2 Wafalme 23:5).

… nao wataitawanya mbele ya jua, na mwezi, na jeshi lote la mbinguni, walivyovipenda, na kuvitumikia, na kuandamana navyo, na kuvitafuta, na kuviabudu haitakusanywa pamoja tena, wala kuzikwa; itakuwa ni samadi juu ya uso wa nchi. (Yeremia 8:2).

…. na nyumba za Yerusalemu, na nyumba za wafalme wa Yuda, zilizotiwa unajisi, zitakuwa kama mahali pa Tofethi; naam, nyumba zote ambazo juu ya dari zake wamelifukizia uvumba jeshi lote la mbinguni, na kuwamiminia miungu mingine sadaka za kunywewa. (Yeremia 19:13).

…. na wale walisujudiao jeshi la mbinguni juu ya dari za nyumba; na hao waabuduo, waapao kwa Bwana na kuapa pia kwa Malkamu (Zefania 1:5).

...............................................
Katika mwaka 570 BK, mwaka uleule ambao Muhammad alizaliwa, alikuwapo mtawala mmoja wa dola ya Aksum ya Ethiopia ambaye alikaa Yemen. Huyu aliitwa Abrahah al- Ashram. Inaelezwa kwamba alikuwa na wivu na mji wa Makka kwa jinsi ambavyo watu wengi walikuwa wakienda kuhiji (yaani hija ya kipagani), hivyo na yeye naye akajenga kanisa kubwa kule Sanaa, Yemen akitarajia kuvuta watu wengi, jambo ambalo halikutokea.

Matokeo yake, aliamua kwenda kuvamia Makka kwa lengo la kuiharibu kaaba. Alisafiri na watu wake wengi juu ya kundi kubwa la tembo - ndiyo maana hata mwaka ule ukajulikana kama mwaka wa tembo.

Koo za Kiquresh ziliungana ili kujaribu kuikoa kaaba. Abdul Mutaleb (babu yake Muhammad) aliwaambia watu wakimbilie kujificha milimani wakati yeye na baadhi ya watu walibakia karibu na kaaba.

Lakini kwa sababu ya ukubwa na nguvu ya jeshi la yule Abrahah, Abdul Mutaleb alisema:

"The Owner of this House is its Defender, and I am sure He will save it from the attack of the adversaries and will not dishonor the servants of His House."

Yaani:
Mmiliki wa nyumba hii ndiye atakayekuwa Mlinzi wake, na nina uhakika ataiponya dhidi ya kushambuliwa na maadui na hawatawafedhehesha watumishi wa nyumba yake."

Mapokeo yanasema kwamba wakati Abrahah anasonga mbele kuiendea kaaba, lilitokea kundi kubwa la ndege ambao walianza kumdondoshea mawe kama mvua hadi wakamjeruhi. Hivyo, azma yake ya kuiharibu kaaba haikufanikiwa, badala yake akarudi kwake akiwa ameumizwa.

Sasa, swali ni kuwa, kama wakati ule Muhammad alikuwa bado kichanga, na hivyo Uislamu ulikuwa haujaanza; na pale kwenye kaaba inajulikana kwamba kulikuwa na mamia ya miungu ya kipagani; je, Mmiliki wa Nyumba anayetajwa na Abdul Mutaleb ni nani?

Ni wazi kwamba huyu ni mungu wa kipagani, yaani allah aliyekuwa akiabudiwa na kutumikiwa na Abdul Mutaleb, yaani mungu mwezi.

Na swali kubwa zaidi ni kuwa, Quran inasema katika sura Al-Fil (au Tembo) 105:1-5:

"Have you not seen how your Lord dealt with the owners of the Elephant? Did He not make their treacherous plan go astray? And He sent against them birds in flocks, striking them with stones of baked clay, so He rendered them like straw eaten up."

Yaani:

Kwani hukuona jinsi Mola wako Mlezi alivyo watenda wale wenye tembo? Kwani hakujaalia vitimbi vyao kuharibika? Na akawapelekea ndege makundi kwa makundi, Wakiwatupia mawe ya udongo wa Motoni, Akawafanya kama majani yaliyo liwa!

Swali ni kuwa:
Mambo haya yalitokea wakati Uislamu haupo, bali ulikuwa ni wakati wa upagani. Mtumishi wa mungu wa kipagani Abdul Mutaleb alisema kwamba Mmiliki wa Nyumba ile (kaaba) angeitetea.

Je, Mmiliki wa nyumba aliyetajwa na Abdul Mutaleb alikuwa yupi na Mola wako anayetajwa na Quran kwenye sura hii ni yupi? Au tuseme kulikuwa na miungu miwili iliyoshirikiana kumpiga mawe Abrahah na tembo wake?

Abdul Mutaleb hakumjua Allah wa Muhammad, kwa hiyo kwa namna yoyote ile hangeweza kumtaja huyo (kama kweli Allah wa Muhammad ni tofauti na wa Abdul Mutaleb).

Mazingira yote yanaonyesha kwamba mungu mwezi, aliyeabudiwa na Abdul Mutaleb ndiye aliyeilinda kaaba dhidi ya tembo wa Abrahah. Kwa hiyo, aya hii ya Quran haina uwezo wa kujinadi kwamba inamtaja mungu tofauti na huyo!!

Hitimisho

Kama wewe ni Mwislamu, je, haujiulizi inakuwaje kwamba mwezi ndio wenye usemi juu ya mambo mengi ya muhimu kwenu Waislamu?

Kwa nini ni lazima mwezi uonekane ndipo mfungo uanze?
Kwa nini ni lazima mwezi uonekane ndipo mfungo uishe?
Kwa nini alama kuu juu ya kila msikiti ni nusu mwezi na nyota? Ni nini asili ya vitu hivyo?
Man please anzisha trend ya huu uzi mzuri sana na una elimisha
 
Watoto wa Ibrahim ni Isaka na Ishmael aliyezaa na mjakazi wake hajiri. Mimi nilikuwa nakuonesha kuwa Ibrahim hakuwahi kuwa muislam kwa maana ya dini wala hakujenga kaaba arabuni na ushahidi soma post zangu zilizotangulia. Kama unapinga toa maelezo kwa nini unapinga ili tuelewane.
huyo hakuna kitu sababu quran inasema nami (mudy) nimekuwa wa kwanza kwa wenye kusilimu cha ajabu anasema habar za Ibrahimu 😀 😀
 
Hongera kwa kuona mengi. Ila unafikiri ushajua tote, so kweli. Kuona siyo kujua, kutembea nchi mbalimbali siyo kujua nk. Endelea kujifunza yumkini utaelewa kweli ya unachodharau.

Tuambieane mengine lakini siyo dini uchwara hizi za kigeni.
 
SURAT ASH-SHAMS 1-3
1. Naapa kwa usiku ufunikapo, 2 kwa mchana uingiapo, 3. na kwa aliye umba kiume na kike..

Hivi mtu anaye apa kwa mwengine anakuwa Mungu au binadamu? Je, nani kaumba hapo. Maana Allah anaapa katika aliye umba, na kuumba ni sifa ya Mungu. Kumbe Allah ambaye sie Yehova hakuumba.

Zaidi ya hapo, Allah anaapa kwa usiku. Kumbe usiku una mamlaka zaidi ya Allah. Allah anaapa kwa mchana, kumbe mchana una mamlaka zaidi ya Allah.

Mbona katika SURAT ASH-SHAMS Allah anaapa kwa (1) Usiku (2) Mchana (3) kwa aliye umba kiume na kike?

Je, ni nani huyu aliye umba Kiume na Kike ambaye Allah wa Islam anaapa kwake? Endelea kusoma...kutoka Biblia Takatifu….

Yeremia 27: 5 Mimi nimeiumba dunia hii, wanadamu na wanyama walio juu ya uso wa nchi, kwa uweza wangu mkuu, na kwa mkono wangu ulionyoshwa; nami nawapa watu kama inipendezavyo.

Sasa tunamsoma Yehovah ambaye ni Mungu wa Biblia kuwa yeye ndie aliye umba kila kitu, pamoja na Kiume na Kike ambacho Allah wa Islam anaapa kwake. Kwahiyo, Jehovah aliumba kiume na kike, na Allah wa Islam anaapa kwake, sasa jaza mwenyewe nani ni Mungu?

Je, Mungu anaweza kuapa kwa Mwengine? Endelea kupata elimu …

Waebrania 6:13 Mungu alipompa Abrahamu ahadi, aliapa kwa jina lake mwenyewe, maana hakuna aliye mkuu kuliko Mungu ambaye kwa huyo angeweza kuapa.

Jehova anasema hakuna Mkubwa wangu wa kuapa kwake, lakini Allah katika Kuran anasema kuwa yeye anaapa kwa aliye umba kiume na kike.
We mbabaishaji mi stakuacha kila ukileta ubabaishaji wako.
Kwanza nami nathibitisha Allah ameumba kike na kiume kisha ntakujibu kuhusu kuapa.
Quran 4.1
"Enyi watu! Mcheni Mola wenu Mlezi aliye kuumbeni kutokana na nafsi moja, na akamuumba mkewe kutoka nafsi ile ile. Na akaeneza kutokana na wawili hao wanaume na wanawake wengi. Na tahadharini na Mwenyezi Mungu ambaye kwaye mnaombana, na jamaa zenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaangalieni"
Nimethibisha hili kwanza kwakua umeifumbia macho aya hii inayosema Allah kaumba mwanaume na mwanamke.
Kisha tuje kwenye kuapa.
Katika uislam kiapo anachokifanya kiumbe hakitakiwi ila kufanywa kwa Allah pekee.
Allah pekee anaapaa kwa viumbe wake na hilo ni katika hiyari yake kuapa kwa kile akitakacho.
Sasa wewe thibitisha kuna mahusiano gani baina ya Allah kuapa kwa kiumbe na kua yeye si mola wa haqqi ikiwa una hoja.
 
Kama kumwabudu Mungu mmoja ni uislam, basi huo wa wakina Ibrahim sio uislam kwa maana ya dini yako unayoabudu leo ila ni maana ya neno na siyo dini ya Islam maana uislam wa dini umeanza kwenye karne ya sita. Ni kama Wakristo wa Kiarab kutumia neno Allah kumaanisha Mungu wanamaanisha Mungu anayeabudiwa na Wakristo na siyo Mungu wa Waislam.
Pili nilikuambia kabla kuwa maandiko yanaonesha dhahiri kuwa Ishmael alifukuzwa mapema sana na hakuendelea kuishi na babake na kuthibitisha nikakuambia kuwa kaburi la Sara mkewe Ibrahim lipo eneo moja na la Ibrahim hiyo inaonesha aliendelea kuishi na mkewe Sara tofauti na maelezo yako.
Kuthibitisha zaidi hilo hata vizazi vya Ibrahim vinatajwa vinavyotokana na Isaka na siyo Ishmael,
Kingine ni kuwa Kaaba haikujengwa ni jiwe jeusi kwa hiyo kama unakataa ni kimondo at least tutakubaliana ni jiwe, swali jiwe huwa linajengwa au hutokea naturally?
Hapa napata shaka hata huyo Ibrahim mnaemzungumzia yumkini ni mtu mwingine kabisa.
Kilichobaki ni ubishaji usio na tija. Wakati unasoma hoja ulipothitishiwa Ibrahim muislam ukashindwa kuthibitisha Ibrahim alikua mkristo.
Tusaidie hapo Ibrahim alikua dini gani? Ikiwa ukristo kaleta Yesu?
Hujajua kwamba manaabii wote waliokuja baada ya Ibrahim walitokea kizazi cha Ishaqa isipokua mmoja tu kutoka katika kizazi cha Ismail?
Ismael ni mtoto Hajar na si wa Sara kuhusu Ibrahim kuzikwa na sala sehem moja hujathibitisha na hata ikiwa hivyo haijabadili uhalisia wowote.
Kuhusu madai yako ya kaaba kimondo sjui jiwe hayana msingi wowote sitakuzingatia baada ya sasa.
 
Mkuu mimi sijaumbwa na allah mimi nimeumbwa kwa udongo tena na MUNGU MWENYE UWEZO WOTE JEHOVAH sio allah ambaye yeye anadai anaumba watu kwa damu Quran 96:1-2 Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba,

2. Amemuumba binaadamu kwa tone la damu, umeona hapo allah anawaumba watu kwa tone la damu 😀 😀 😀 kweli allah msanii
Utasafishwa matongo tongo yte taliyojaa usoni kwako. Huwezi kubaibaisha mbele ya wasomi
Quran 22.5
"Enyi watu! Ikiwa nyinyi mna shaka ya kufufuliwa basi kwa hakika Sisi tulikuumbeni kutokana na udongo, kisha kutokana na manii, kisha kutokana na kipande cha damu ilio gandana, kisha kutokana na kipande cha nyama chenye umbo na kisicho kuwa na umbo, ili tukubainishieni. Nasi tunakiweka katika matumbo ya uzazi tunacho kitaka mpaka muda ulio wekwa. Kisha tunakutoeni kwa hali ya mtoto mchanga, kisha mfikie kutimia akili. Na wapo katika nyinyi wanao kufa, na wapo katika nyinyi wanao rudishwa kwenye umri wa unyonge kabisa, hata mtu awe hajui kitu baada ya kuwa anakijua. Na unaiona ardhi imetulia kimya, lakini tunapo yateremsha maji juu yake husisimka na kututumka, na kumea kila namna ya mimea mizuri."
 
We mbabaishaji mi stakuacha kila ukileta ubabaishaji wako.
Kwanza nami nathibitisha Allah ameumba kike na kiume kisha ntakujibu kuhusu kuapa.
Quran 4.1
"Enyi watu! Mcheni Mola wenu Mlezi aliye kuumbeni kutokana na nafsi moja, na akamuumba mkewe kutoka nafsi ile ile. Na akaeneza kutokana na wawili hao wanaume na wanawake wengi. Na tahadharini na Mwenyezi Mungu ambaye kwaye mnaombana, na jamaa zenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaangalieni"
Nimethibisha hili kwanza kwakua umeifumbia macho aya hii inayosema Allah kaumba mwanaume na mwanamke.
Kisha tuje kwenye kuapa.
Katika uislam kiapo anachokifanya kiumbe hakitakiwi ila kufanywa kwa Allah pekee.
Allah pekee anaapaa kwa viumbe wake na hilo ni katika hiyari yake kuapa kwa kile akitakacho.
Sasa wewe thibitisha kuna mahusiano gani baina ya Allah kuapa kwa kiumbe na kua yeye si mola wa haqqi ikiwa una hoja.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] wewe umetaka mwenyewe mimi nagonga nyundo tu ila kabla ya kuendelea nakuonya tena mkuu kama allah alivyokwambia

[emoji116] [emoji116] [emoji116] [emoji116]
quran 5:101

Enyi mlio amini! Msiulize mambo ambayo mkidhihirishiwa yatakuchukizeni. Na mkiyauliza inapo teremshwa Qur'ani mtabainishiwa. Mwenyezi Mungu amesamehe hayo. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghfira Mpole.
 
Kilichobaki ni ubishaji usio na tija. Wakati unasoma hoja ulipothitishiwa Ibrahim muislam ukashindwa kuthibitisha Ibrahim alikua mkristo.
Tusaidie hapo Ibrahim alikua dini gani? Ikiwa ukristo kaleta Yesu?
Hujajua kwamba manaabii wote waliokuja baada ya Ibrahim walitokea kizazi cha Ishaqa isipokua mmoja tu kutoka katika kizazi cha Ismail?
Ismael ni mtoto Hajar na si wa Sara kuhusu Ibrahim kuzikwa na sala sehem moja hujathibitisha na hata ikiwa hivyo haijabadili uhalisia wowote.
Kuhusu madai yako ya kaaba kimondo sjui jiwe hayana msingi wowote sitakuzingatia baada ya sasa.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] mnapalamiana limkitaby lenu linashida sana mwenzio hapo juu hujamuona kasema Ishmael ndio altaka kuchinjwa na Ibrahim nikashangaa nikajua itakuwa ana janaba[emoji23] sasa na wewe wampinga sheikh mwenzio[emoji23]
 
Utasafishwa matongo tongo yte taliyojaa usoni kwako. Huwezi kubaibaisha mbele ya wasomi
Quran 22.5
"Enyi watu! Ikiwa nyinyi mna shaka ya kufufuliwa basi kwa hakika Sisi tulikuumbeni kutokana na udongo, kisha kutokana na manii, kisha kutokana na kipande cha damu ilio gandana, kisha kutokana na kipande cha nyama chenye umbo na kisicho kuwa na umbo, ili tukubainishieni. Nasi tunakiweka katika matumbo ya uzazi tunacho kitaka mpaka muda ulio wekwa. Kisha tunakutoeni kwa hali ya mtoto mchanga, kisha mfikie kutimia akili. Na wapo katika nyinyi wanao kufa, na wapo katika nyinyi wanao rudishwa kwenye umri wa unyonge kabisa, hata mtu awe hajui kitu baada ya kuwa anakijua. Na unaiona ardhi imetulia kimya, lakini tunapo yateremsha maji juu yake husisimka na kututumka, na kumea kila namna ya mimea mizuri."
ila allah atakuwa hamnazo hivu huyu allah ni nani na hiyo quran 96:1-2 ni maneno ya nani?

si yeye ndiyo kasema kakuumba kwa tone[emoji98] la damu[emoji23] [emoji23] [emoji23] au alikuwa anapuliza akawa hajielewi

NDIO SABABU UKIISOMA QURAN SANA UNAKUWA CHIZI
 
Kilichobaki ni ubishaji usio na tija. Wakati unasoma hoja ulipothitishiwa Ibrahim muislam ukashindwa kuthibitisha Ibrahim alikua mkristo.
Tusaidie hapo Ibrahim alikua dini gani? Ikiwa ukristo kaleta Yesu?
Hujajua kwamba manaabii wote waliokuja baada ya Ibrahim walitokea kizazi cha Ishaqa isipokua mmoja tu kutoka katika kizazi cha Ismail?
Ismael ni mtoto Hajar na si wa Sara kuhusu Ibrahim kuzikwa na sala sehem moja hujathibitisha na hata ikiwa hivyo haijabadili uhalisia wowote.
Kuhusu madai yako ya kaaba kimondo sjui jiwe hayana msingi wowote sitakuzingatia baada ya sasa.
eti ibrahimu alikuwa muislamu[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]

Msome mudy anavyokwambia

quran 6:14
. Sema: Je, nimchukue rafiki mlinzi asiye kuwa Mwenyezi Mungu, ambaye ndiye Muumba mbingu na ardhi, naye ndiye anaye lisha wala halishwi? Sema: MIMI NIMEAMRISHWA NIWE WA KWANZA WA WENYE KUSILIMU. Na wala kabisa usiwe miongoni wa washirikina.

mkuu nakusubiria kwa povu [emoji36] [emoji36] [emoji36]

Ila allah anamatatzo sana yani anaweza kukwambia nguruwe dhambi ila ukiwa na njaa kula sasa sijui nani anakulaga akiwa ameshiba[emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2]

au anakwambia pombe dhambi halafu pepo yake ukienda anakwambia utakunywa hadi uache[emoji3] [emoji3] [emoji3]
 
Wabongo mmeletewa dini,ila mnajifanya mnajua kuliko waliowaletea mzungu kawaletea ukirsto na mwarabu kawaletea uislam Alf dini zote izo zimekopi kwa myaudi, dini nimambo zakutengsnisha jamii vhakuamini niMUNGU yupo sio izo mambo zenu zakufa kwwajili ya mungu flank kwakua yeye amepigakimya bora ya wakristo wakitukanwa wao wanavunga cos wanaamini MUNGU wao anaweza kujisaidia mjipange mlioletewa dini na wafanyabiashara wakizungu nawakiarabu
 
  • Thanks
Reactions: PNC
eti ibrahimu alikuwa muislamu[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]

Msome mudy anavyokwambia

quran 6:14
. Sema: Je, nimchukue rafiki mlinzi asiye kuwa Mwenyezi Mungu, ambaye ndiye Muumba mbingu na ardhi, naye ndiye anaye lisha wala halishwi? Sema: MIMI NIMEAMRISHWA NIWE WA KWANZA WA WENYE KUSILIMU. Na wala kabisa usiwe miongoni wa washirikina.

mkuu nakusubiria kwa povu [emoji36] [emoji36] [emoji36]

Ila allah anamatatzo sana yani anaweza kukwambia nguruwe dhambi ila ukiwa na njaa kula sasa sijui nani anakulaga akiwa ameshiba[emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2]

au anakwambia pombe dhambi halafu pepo yake ukienda anakwambia utakunywa hadi uache[emoji3] [emoji3] [emoji3]
Ukaafir hautakuacha salama
 
Back
Top Bottom