Akumbukwe John Okello, Baba wa Taifa la Zanzibar. Bila huyu leo Zanzibar wangekuwa bado Utumwani

End justifies the begining. Wengine walifeli hadi mpaka hapo okelo alipo oongoza mapinduzi na yakafanikiwa huku hao unaosema maplanner wakiwa wamejificha gest house tanganyika kama panya wajifichavyo mafichoni.

All in all okello apewe heshima yake katika mapinduzi ya zenji bila yeye yaaingetokea.

Kwanini hamtaki kumpa heshima yake badala yake wanapewa heshima waliojificha mashimoni wakati mwanaume akiongoza mapambano. ?
View attachment 2478861
Hawataki Kwa sababu ya jina lake wala sio kingine
 
End justifies the begining. Wengine walifeli hadi mpaka hapo okelo alipo oongoza mapinduzi na yakafanikiwa huku hao unaosema maplanner wakiwa wamejificha gest house tanganyika kama panya wajifichavyo mafichoni.

All in all okello apewe heshima yake katika mapinduzi ya zenji bila yeye yaaingetokea.

Kwanini hamtaki kumpa heshima yake badala yake wanapewa heshima waliojificha mashimoni wakati mwanaume akiongoza mapambano. ?
View attachment 2478861
Mohamed Said jamaa aliyeandika hapa ana hoja ya msingi sana. Nadhani tufikiw hatua tuepukane na ubaguzi. John Okello apewe sifa zake stahiki. Alipambana kiume na aliwatisha sana watu kwa nguvu zake. Hata sauti yake tu iliwafanya wawe na mhaho.
 
City...
City...
Okello anabebeshwa mzigo si wake.

ASP haikuwa na uwezo wa kupindua serikali.

Mipango yote ilifanyika Dar es Salaam ikisimamiwa na Oscar Kambona na Abdullah Kassim Hanga.

Waliweka kambi Kipumbwi ambako waliwaweka Wamakonde kutoka shamba la Mkonge la Sakura kwa ajili ya kuwavusha kuingia Zanzibar kuIpigIa kura ASP na kushiriki katika mapinduzi.

Kambi hii ilikuwa chini ya Ali Mwinyi Tambwe akiwa District Commissioner wa Tanga na Regional Commissioner Jumanne Abdallah.

Waliopewa kazi ya kuchagua vijana wa kuletwa kambini Kipumbwi walikuwa Victor Mkello kiongozi wa chama cha wakata mkonge na Mohamed Omar Mkwawa kijana wa Kidigo kutoka Tanga aliyepatakuwa mwanachama hodari wa ASP.

Ali Mwinyi Tambwe wakati wa ukoloni aliwatumikia Waingereza kama "mole" wao ndani ya TAA kisha TANU.

Mkwawa yeye ndiye aliyekuwa akiwavusha hawa Wamakonde kuwaingiza Zanzibar usiku kwa majahazi wote wamevaa kama wavuvi wa Kidigo.

Kipumbwi yote ilikuwa imezuiwa kwa watu kuingia ovyo.

Hawa Wamakonde ndiyo walioua Waarabu wengi wakulima wa kawaida tu waliokuwa mashambani Zanzibar.

Mpango huu ulifanyika kwa siri kubwa sana.

Mzanzibari aliyepata kufika Kipumbwi inasemekana ni Jimmy Ringo ambae aliuliwa baada ya mapinduzi kama walivyouliwa wana ASP wengine.

John Okello hakuwa katika mipango hii.

Kilichompa umaarufu ni kule yeye kupewa radio kutangaza kuwa serikali imepinduliwa na Karume arejee Zanzibar kukalia kiti chake.
Uhusika wake ni upi hata kupewa radio kutangaza kuwa serikali imepinduliwa?.
 
Wakati wa Mapinduzi Mwaka 1964.Karume Alikuwa amejificha Tanzania Bara.

John Okello Raia wa Uganda Akiongoza Mapinduzi na kupiga picha akiwa kama KIONGOZI wa nchi Baada ya Mapinduzi.

Alivamia Hadi kituo Cha utangazaji Zanzibar na Kujitangaza kuwa Rais.

Pia alijitangaza USHINDI dhidi ya sultan

Wazanzibari wantakiwa Wafahamu kuwa John Okello Ndiye Baba wa Taifa la Zanzibar.

Nakukubali sana jamaa yangu
CHIZI MAARIFA
 
Uhusika wake ni upi hata kupewa radio kutangaza kuwa serikali imepinduliwa?.

Yaani haiingii akilini eti wengine wafanye mapinduzi ila kwenye kutangaza kuwa wameshinda wanaogopa mpaka wakaenda mitaani kumtafuta Okello aje awatangazie. Huyu mzee side boi anatuona sisi kama watoto wadogo sana kwamba hatuwezi kuhoji wala kufikiri.

Sasa swali linakuja kwanini hao anaosema wapigania mapinduzi waliogopa kukaa front?mpaka wakakimbilia tanganyika.
 
Huyu John alikuwa ni wa nchi gani?alifikaje Zenj? malizia story
Yaani... nilikuwa niseme labda tumuite Mzee wetu ndio kahawa ya Asubuhi ikolee. Sina uhitaji wa kusema hayo....Ila Asubuhi hii, hata sambusa nashindwa kula kwa kucheka hapa kuhusu...

Wenye Lafudhi, Wachuma mkonge, Wamakonde walijibadilisha kuwa Wamakondigo, na kwa mara ya Kwanza kusikia Waarabu walikuwa wakulima wakawaida, yaani kama wao walikuwa wanalima hawana lile wala nini mara bin vuuu lisauti likawatisha wakafa😂
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😌😍🤪🤭🤔
Aiseee Kumbe saa nyingine afadhali kusoma soma kupunguza mihemeko, na mapovu.

Lugha za Mzee Mhhh

Moyoni nasema hapa ni Lazima atasema ni wakuja...akaongeza ana Lafudhi...

.Mie Sijui Nchi ilikombolewa na nani sasa manake kama Waarabu walikuwa wakulima, Wazenji walikuwa nani?

Amani iwafikie Asubuhi njema.
 
Kwa nini alipewa jukumu zito kama hilo ilhali alikuwa wakuja tu?
Hawezi kuja tena kutetea uongo wake ila anachokwepa hapa ni mambo mawili la kwanza
(1)Ni aibu na fedheha kumtangaza mgeni John Okello kuwa ndiye mwanamapinduzi.
(2)Lingine ni dini yake haiwezekani Zanzinzibar inajulikana nchi ya Kiislamu halafu umtukuze John Okello hawako tayari ndiyo maana nimesema Mohamed Said hana majibu tena wala hatarudi na endapo atarudi atarudia yaleyale.
 
Yaani haiingii akilini eti wengine wafanye mapinduzi ila kwenye kutangaza kuwa wameshinda wanaogopa mpaka wakaenda mitaani kumtafuta Okello aje awatangazie. Huyu mzee side boi anatuona sisi kama watoto wadogo sana kwamba hatuwezi kuhoji wala kufikiri.

Sasa swali linakuja kwanini hao anaosema wapigania mapinduzi waliogopa kukaa front?mpaka wakakimbilia tanganyika.
Sasa we ulitaka Mkisto awe baba wa Taifa la Zanzibar huoni Mohamed Said anavyo angaika na Mwalimu Nyerere kwa nini awe baba wa Taifa mwenye macho na akili haambiwi tazama watu wa Pwani kutetea uongo ni sahihi kwa imani yao maadamu lina maslahi kwao.
 
Vijana WA Leo msomeni sana Harith Ghassany, ''Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru,''

Pia msomeni sana Joseph Mihangwa RAIA MWEMA.

Jamaa wameandika vizuri sana historia ya Mapinduzi.

JOHN OKELO YOHANA MBATIZAJI NDIE BABA WA TAIFA WA ZANZIBAR.
inashangaza sana Wazanzibar kukataa Ujenzi wa makanisa wakati OKELO BABA WA TAIFA LAO NI MKRISTO.
 
City...
City...
Okello anabebeshwa mzigo si wake.

ASP haikuwa na uwezo wa kupindua serikali.

Mipango yote ilifanyika Dar es Salaam ikisimamiwa na Oscar Kambona na Abdullah Kassim Hanga.

Waliweka kambi Kipumbwi ambako waliwaweka Wamakonde kutoka shamba la Mkonge la Sakura kwa ajili ya kuwavusha kuingia Zanzibar kuIpigIa kura ASP na kushiriki katika mapinduzi.

Kambi hii ilikuwa chini ya Ali Mwinyi Tambwe akiwa District Commissioner wa Tanga na Regional Commissioner Jumanne Abdallah.

Waliopewa kazi ya kuchagua vijana wa kuletwa kambini Kipumbwi walikuwa Victor Mkello kiongozi wa chama cha wakata mkonge na Mohamed Omar Mkwawa kijana wa Kidigo kutoka Tanga aliyepatakuwa mwanachama hodari wa ASP.

Ali Mwinyi Tambwe wakati wa ukoloni aliwatumikia Waingereza kama "mole" wao ndani ya TAA kisha TANU.

Mkwawa yeye ndiye aliyekuwa akiwavusha hawa Wamakonde kuwaingiza Zanzibar usiku kwa majahazi wote wamevaa kama wavuvi wa Kidigo.

Kipumbwi yote ilikuwa imezuiwa kwa watu kuingia ovyo.

Hawa Wamakonde ndiyo walioua Waarabu wengi wakulima wa kawaida tu waliokuwa mashambani Zanzibar.

Mpango huu ulifanyika kwa siri kubwa sana.

Mzanzibari aliyepata kufika Kipumbwi inasemekana ni Jimmy Ringo ambae aliuliwa baada ya mapinduzi kama walivyouliwa wana ASP wengine.

John Okello hakuwa katika mipango hii.

Kilichompa umaarufu ni kule yeye kupewa radio kutangaza kuwa serikali imepinduliwa na Karume arejee Zanzibar kukalia kiti chake.
kwanini wawe wamakonde tu na sio kabila lingine?
 
Sasa we ulitaka Mkisto awe baba wa Taifa la Zanzibar huoni Mohamed Said anavyo hangaika na Mwalimu Nyerere mwenye macho na akili haambiwi ona.
Frank...
Sijapatapo kuhangaika na Nyerere ila nimeandika historia yake kwa kadri ya uwezo wangu.

Kuhusu Okello historia yake naifahamu vizuri kwa utafiti kwani nilikuwa Mtafiti Msaidizi wa Dr. Harith Ghassany wakati anaandika, "Kwaheri Uhuru Kwaheri Ukoloni.''

Siwezi kumlazimisha mtu kuniamini anaweza kuamini atakacho.
 
Maelezo yako yana upungufu.
Inawezekanaje mtu ambaye hakushiriki kuongoza mission apewe kutangaza ushindi ?
Wakati mission inaendelea kiongozi alikua na John Okello muda huo alikua wapi ?
Kwa akili ya kawaida watu wanaogopa sauti au wanaogopa mtu aliyeleta ushindi Kwa kutuma silaha ?
Inawezekana vp kiongozi aliyeongoza mapinduzi hayo ampe sifa Mpita njia ambaye hakushiriki !
Nikipata ufafanuzi wa hoja hizi ndipo nitakuelewa,nje ya hapo tusipindishe maneno tumtambue tu Jemedari J. Okello.
Dingi...
Siko hapa kubishana.

Mimi namweleza Okello kama nilivyomjua kutokana na utafiti.

Unaweza kuamini utakacho hata bila ya kutafiti.

Hakuna wa kukuzuia.
 
Mna...
Ni kweli lakini Wamakonde walitawala kazi hiyo.
kwa ushahidi upi wakati kwa uchache tu nimekueleza kuwa kulikuwa na wamwera pia? Unajua kuna mazoea ya wengi kuwa mtu akitoka kusini maana yake ni mmakonde kitu ambacho sio kweli je wewe si muumini wa hivyo?
 
Back
Top Bottom