Akumbukwe John Okello, Baba wa Taifa la Zanzibar. Bila huyu leo Zanzibar wangekuwa bado Utumwani

Mgeni,
ASP na Umma Party walikuwako wababe si Okello.

Okello alivuna kwenye "Mob Psychology."

Alikuwa mfano wa Musiba aliyekuwa anazungumza kwenye mitandao ya kijamii.

Ushamsikia tena Musiba?

Okello alipokutana na Hashil Seif (huyu ni comrade kasoma Cuba) ndani ya ndege Okello hakuweza kufanya lolote alisalimu amri.

Hakuweza kumkabili Hashil.

Wako wababe kutoka ASP ukihadithiwa unyama wao mwili utakusisimka.

Watu wenye uwezo wa kumzika mtu yu hai.

Nilikuwa nataka kuandika kuhusu kubakwa kwa binti mdogo wa Kihindi wakati mama yake anabakwa....

Nashindwa kuandika maneno ya huyu mama kuomba salama ya mwanae...

Aliyenihadithia ni kati ya hao washenzi...

Wengi mnaandika msiyoyajua.
Mzee Mohamed andika tujifunze.
 
Cuba na nchi nyingine ambazo Chegu wa 1 alishiriki kuzipa uhuru wanatambua nafasi yake, ni huku kwetu tu ndo tunatambua huyu Chegu wa EA kwa sauti yake redioni. Jokes!
 
Niwekee link mzee wangu.
Being...

Ni kweli, nilimuuliza Sheikh Said ikiwa Mapinduzi ni halali au ni haramu. Sijawahi kupata jibu zaidi ya ku'dance'

Kuna ''Mwarabu wa London'' Bw Rajab, yeye alijaribu lakini pia hakuwa na jibu la moja kwa moja.
Katika gazeti la Raia mwema, alisema ' kwamba ni halali au haramu inatagemea mtu yupo upande gani''

Ni nadra kumsikia Jussa akitamka neno Mapinduzi lakini ni kawaida sana kumsikia Mansour Himid akitamka.
Mifano hiyo inaonyesha sensitivity ya jambo zima na linavyowagawa Wazanzibar hasa kwa rangi na nywele

Niliwahi kumuuliza Mo ikiwa Mapinduzi ni haramu na yalifanywa na Watu kutoka Tanganyika kambi ya Kipumbwi, je, Wazanzibar wanaosherehekea wanafanya makosa kutukuza haramu?
Hakuna jibu hadi kesho, ana 'dance' tu

Kwa bahati mbaya katika wale 12 wa Baraza la Mapinduzi wengi wametangulia mbele ya haki, waliobaki wachache ni A.H.Mwinyi sina habari za Kanali S.Bakar. @JokaKuu kama una taarifa zaidi tafadhali

Wanamapinduzi 12 hawakuacha nyaraka kwa kimaandishi kama vitabu vya kueleza nini kilijiri, sijui kama walikatazwa au la. Tunabaki na simulizi za upande mmoja kutoka Oman au mrengo wa Kiimani.

Kinachosikitisha ni chombo kama TBC kinachoendeshwa kwa kodi zetu kinatumiwa 'kiharamia'

Tido alilipa gharama pia kwa kutaka kuiweka TBC huru. Aliahidi kuonyesha chaguzi mubashara. CCM hawakubaliani na mambo ya kwenye mwanga, wanapenda mambo kizani, Tido akalipia gharama.

Lakini pia kuna kauli nimeisikia na hapa Mohamed atanisahihisha kwamba ' kuna nyakati heri inafichwa ndani ya shari'' kule Buckingham palace wanasema '' a blessing in disguise' , Tido is better off today.
Nguruvi...
Bahati mbaya unaandika kwa kukejeli.
Umemkejeli Ahmed Rajab na umenikejeli mimi pia.

Laiti ungeandika kwa ustaarabu ningeweza kushawishika kuchangia.
Nimejifunza mengi kutoka kwa Ahmed Rajab katika historia ya Zanzibar.

Si mtu wa kuvunjiwa heshima yake hapa.

1705780111905.png

Mwandishi na Ahmed Rajab, Mhariri wa Africa Analysis, Barbican London 1991​
 
Being...
Asante mzee wangu mohamed upumzike sasa au unaangalia mechi?
 
Back
Top Bottom