Che Guevara alitamani sana kuonana na Mwanamapinduzi Field Marshall John Okello

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
10,468
23,744
Anasimulia mzee wangu ambaye alikuwa Mwalimu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam miaka hiyo Che Guavera alikuja Tanzania mwaka 1965. Anasema Che alijaribu kuulizia habari za Mwanamapinduzi aliyesaidia kuipatia Zanzibar Uhuru wake John Okello.

Kwa his disappointment alishtuka kuambiwa the Man alifukuzwa mara baada ya kumaliza jukumu lililomleta Zanzibar kuwaondoa Waarabu waliokuwa wakiitawala Zanzibar.

John Okello Baba wa Taifa la Zanzibar ataendelea kukumbukwa kila tutakapoadhimisha Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Baada ya hapo John Okello alirudi kwao kwenda kuendeleza mapambano dhidi ya udhalimu na hatimaye alikuwa kama mtu wa kawaida tu pasipo makuu. Hakulipwa yeye wala familia yake. Kabla ya Mwaka 1967 Che Guevara kufariki aliwahi mtumia mzee wangu barua akimtaka amtafute John Okello wajiunge naye kwenye harakati huko Msumbiji na Angola.

Mzee hakujua aanzie wapi.

AKUMBUKWE BABA WA TAIFA LA ZANZIBAR JOHN OKELLO.
 
Katika taarifa hiyo ya mwendesha uzu hatujapata kuona akieleza sababu zilizosababisha Okelo kufukuzwa.

Tusiilaumu serikali ya Zanzibar kuchukua hatua hiyo Kwani,hatujui kilichoendelea kati ya Okelo na serikali.
 
Katika taarifa hiyo ya mwendesha uzu hatujapata kuona akieleza sababu zilizosababisha Okelo kufukuzwa.Tusiilaumu serikali ya Zanzibar kuchukua hatua hiyo Kwani,hatujui kilichoendelea kati ya Okelo na serikali.
Ukitokea nini man hatujui
 
Wazanzibar waliukataa uhuru aliowatafutia John Okello ndio maana wanatawaliwa na Tanganyika kwa mgongo wa muungano. Muungano wenyewe hauna muundo rasmi.
 
Laana ya Zanzibar Kumkataa aliyewaletea Mapinduzi na Uhuru mpaka leo inawatafuna.
 
Zanzibar hawakumtendea haki.

Baada ya kufanya mapinduzi huko Zanzibar, John Okello alianza kuonyesha tabia ambazo zimekuwa zikionyeshwa na baadhi ya viongozi waliongia madarakani kwa mtutu.

Mwl Nyerere na aliyekuwa rais wa Zanzibar wakati huo wakaamua kusuka mpango wa kumfurusha John Okello ili asilete machafuko.
 
Allah awajaalie qauli thabit waislamu/waarabu wote waliokufa katika vita iliyoongozwa na kafiri okello laanatullah alaihi firauni mmoja huyo.

Hata siku moja haitatokea nishabikie ama kumuenzi huyo kafiri okello na wenzie alioshirikiananao kwa namna moja ama nyingine dhidi ya uvamizi huo na kuuwa waislamu/waarabu.

Dahh very sad 😔😔😔 kuna watu walikua makatili sijapata kuona, waliwanyanyasa sana na kuwauwa,,, wakina mama, wazee, watoto na wamama wajawazito, wengi waliuawa na hayo majahili😡😡😡. na pia walikuwemo baadhi ya waislamu walioshiriki vita hivyo na kuuwa waislamu wenzao, ivi kweli unamshikia ndugu yako bunduki na kumuuwa kweli, inakupa roho!

Waliofanya ukatiri huo walidhani wataishi milele eee. Leo hatunao, imebakia kumbukumbu tu.

Karume + okello + n.k walioshiriki Watayakuta malipo yao kwa udhaalim waliowafanyia ndugu zetu waislamu/waarabu.
 
Baada ya kufanya mapinduzi huko Zanzibar, John Okello alianza kuonyesha tabia ambazo zimekuwa zikionyeshwa na baadhi ya viongozi waliongia madarakani kwa mtutu.

Mwl Nyerere na aliyekuwa rais wa Zanzibar wakati huo wakaamua kusuka mpango wa kumfurusha John Okello ili asilete machafuko.
John Okello alikuwa mentally unstable tangu mwanzo.
 
Anasimulia mzee wangu ambaye alikuwa Mwalimu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam miaka hiyo Che Guavera alikuja Tanzania mwaka 1965. Anasema Che alijaribu kuulizia habari za Mwanamapinduzi aliyesaidia kuipatia Zanzibar Uhuru wake John Okello.

Kwa his disappointment alishtuka kuambiwa the Man alifukuzwa mara baada ya kumaliza jukumu lililomleta Zanzibar kuwaondoa Waarabu waliokuwa wakiitawala Zanzibar.

John Okello Baba wa Taifa la Zanzibar ataendelea kukumbukwa kila tutakapoadhimisha Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Baada ya hapo John Okello alirudi kwao kwenda kuendeleza mapambano dhidi ya udhalimu na hatimaye alikuwa kama mtu wa kawaida tu pasipo makuu. Hakulipwa yeye wala familia yake. Kabla ya Mwaka 1967 Che Guevara kufariki aliwahi mtumia mzee wangu barua akimtaka amtafute John Okello wajiunge naye kwenye harakati huko Msumbiji na Angola.

Mzee hakujua aanzie wapi.

AKUMBUKWE BABA WA TAIFA LA ZANZIBAR JOHN OKELLO.

John Okello ni nani? Ilikuwaje alishiriki mapinduzi ya Zanzibar? Nani aliyemhamasisha au nini kilimsukuma aende kule? Je, baada ya Mapinduzi nini kilimfanya apotee kabisa na kusahaulika?
 
Back
Top Bottom