Pan-Africanist, Mapinduzi ya Zanzibar, Muungano wa Tanzania kuelekea Muungano wa Afrika

Leslie Mbena

JF-Expert Member
Nov 24, 2019
207
677
PAN AFRICANIST,MAPINDUZI YA ZANZIBAR,MUUNGANO WA TANZANIA KUELEKEA MUUNGANO WA AFRIKA.

Leo 13:00hrs 12/01/2021

Pan Afrikanist,Mwalimu Julius Nyerere, aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanganyika,na hatimaye Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,ndiye Pan Afrikanist mbeba maono aliyebuni na kusanifu Muungano wa Tanzania,kuundwa kwa Shirikisho la Afrika Mashariki pamoja na mashirikisho ya EAF,ECOWAS Shirikisho la Afrika Magharibi na SADC ikiwa Shirikisho la Kusini mwa Afrika,

Mwanachama dhahiri wa vuguvugu la muungano wa Afrika,Pan Africanist,Julius Nyerere aliiongoza Tanganyika kupata uhuru kutoka Uingereza na baadae akaiunganisha na Visiwa vya Zanzibar na kuunda Tanzania ya leo,Licha ya mapungufu yake,sera yake ya Ujamaa inasifiwa kwa kuipa Tanzaniautambulisho wa kitaifa.

Pan Africanist,Mwalimu Julius Nyerere alipenda sana kuiona Afrika inaungana na kuwa moja. Hili lilikuwa jambo muhimu lakini lenye changamoto kubwa na tete sana kwa sababu ya utofauti mkubwa wa lugha, tamaduni, dini, makabila na kadhalika. Mwalimu alikazia Afrika kuungana hatua kwa hatua; lakini kwanza kuungana kikanda ili polepole nchi majirani zijilee na kuzoea kuungana kabla Afrika yote kiujumla haijaungana,Lakini alipingana na Kwame Nkrumah wa Ghana katika suala hilo.

Pan Africanist,Mwalimu Nyerere alitaka hatua ya kwanza iwe kuungana kwa nchi za Afrika Mashariki, wakati Nkrumah akigombania kuungana kwa nchi zote za Afrika kwa wakati mmoja. Kwa kushirikiana hata hivyo, waliunda Umoja wa nchi huru za Afrika, OAU. Nyerere aliwakaribisha wapiganaji wa uhuru. Baaada ya kupata uhuru wa nchi yake, aliwakaribisha na kuwaunga mkono waasi waliokuwa wakizipinga serikali za Msumbiji, Afrika Kusini, Namibia na nyinginezo.

New Africa Hotel ndiyo hotel yenye historia ya kukutanisha wanamapinduzi wengi,Pan Africanist wa bara la Afrika kwa pamoja,Pale juu New Africa Hotel kulikuwa na baa,watu wakinywa kahawa na vinywaji vingine,Hapo walikusanyika wanaharakati za kimapambano ya ukombozi wa Afrika kutoka kona mbalimbali,Mahali hapa ilipangwa mikakati,kwenye meza moja unaweza kumwona Edward Mondlane wa Frelimo kutoka Msumbiji akiongea na Kenneth Kaunda wa Unip,kutoka Zambia,

Meza nyingine utawaona Pan Africanist,Abeid Karume akiongea na Chisiza wa Malawi,Patrice Lumumba kutoka Kongo Kinshasa akiongea na Ernesto Guevara,utamuona Samora Machel akiongea na Water Ulyate Sisulu kutoka Afrika ya Kusini,Oliver Tambo na Albert Luthuli wakiongea na Neto,Ndwaitah na Sam "Mwakangale" Nujoma ambaye alikuja kuwa Rais wa kwanza wa Namibia.

Maeneo ya kuishi ambapo Mwalimu Julius Nyerere alitoa hifadhi ya kuishi kwa Pan Africanist,Wanamapinduzi wote na Wanaharakati wote barani Afrika ni pamoja na Nachingwea Mkoani Lindi,Kongwa Mkoani Dodoma,Mgagao-Kihesa Mkoani Iringa,Mazimbu na Dakawa Mkoani Morogoro,Kaole Bagamoyo Mkoani Pwani na Dar es Salaam.Wapigania Uhuru waliopata hifadhi na kuhudumiwa na Mwalimu Julius Nyerere ni kutoka vyama vya Ukombozi vya Angola Mpla,Anc na Pac vya Afrika ya Kusini,Frelimo cha Msumbiji,

Zapu cha Zimbabwe,Swapo cha Namibia na wajumbe wote wa kamati ya kupigania Uhuru Afrika kutoka Umoja wa Nchi huru za Afrika (OAU)Pia Mwalimu Nyerere alitumia muda huo kusuluhisha migogoro mbalimbali barani Afrika. Umahiri wake kaama mwalimu, uling'aa katika mioyo na macho ya wengi,Aliwakutanisha waliotofautiana na kutumia muda kuwaelekeza na kuzungumza nao kwa busara,upole na utulivu wa hali ya juu,Alisisitiza kwamba watu wasiokubaliana na kutoelewana wanapaswa kujifunza kukubali na kuwa tayari kuishi pamoja, licha ya tofauti zao.

-Ushawishi wa Pan Africanist haukuwa Nigeria,Ghana au Tanzania tu,bali Afrika Nzima.

Wakati utumwa ukikomeshwa Marekani mwaka 1865 watumwa kutoka Afrika waliosalia hai walikuwa chini ya 4,000,000 ambapo uzao wao ulituletea akina Martin Luther King,Malcom x Watumwa kutoka Afrika waliobaki hai katika visiwa vya Karibbean na West Indies walikuwa 1,370,000 ambao uzao wao ulituletea Pan Africanist kama George Padmore na Marcus Garvey na watumwa waliobaki katika makoloni ya muingereza huku Afrika walikuwa ni 700,000

Uzao wa Watumwa wa Afrika ukatuletea Nnamdi Azikiwe kutoka Biafra nchini Nigeria,Kwame Nkrumah,Julius Nyerere,Jomo Kenyatta,kukomeshwa kwa biashara ya watumwa na utumwa karne ya 19 kulitokana na maendeleo ya mapinduzi ya kiviwanda kwa nchi za Ulaya ambapo uzalishaji mali ulianza kutegemea nyenzo za mashine badala ya nguvu kazi ya watumwa.

Filosofia ya “Pan-Africanism” kama ilivyobuniwa na Daktari William Du Bois, ilikuwa juu ya “nguvu ya kisiasa na heshima ya mtu mweusi ulimwenguni kote”. Kwa Du Bois na Marcus Garvey ambaye alikuja na falsafa nyingine "Garveyism" ikimaanisha Afrika kwa Waafrika,

Moto wao ulikuwa ni heshima kwa mtu mweusi “heshima ya watu wote wenye asili ya Kiafrika”.Kwa masaibu waliyoonja chini ya mfumo wa utumwa nchini Marekani,wenye kutweza na kudhalilisha utu wa binadamu na umiliki wa binadamu kama mtumwa ilikera zaidi pale utumwa ulipojikita kwa mtu mweusi tu na mwenye kumiliki mtumwa akiwa ni mtu mweupe,

Sasa Pan Africanist wakiongozwa na Daktari William Du Bois,Marcus Garvey aliyekuwa tajiri mweusi mwenye kumiliki Kampuni na Kampuni ya Meli ambaye ndiye aliyekuwa mtoa ajira nyingi kwa Waafrika nchini Marekani huku gazeti lake la Marcus Garvey and Universal Negro Improvement Association Papers,

Volume I-VII likitoa mwelekeo na namna ya Watumwa wenye asili ya kiafrika kurudi nyumbani Afrika,The long-awaited African Volumes Edition VIII,IX na X ,liliafikiana na jamii yote watumwa weusi na kufikia uamuzi kwamba dharau hii ingekoma kama Afrika ingekuwa huru,Marcus Garvey aliazimia kutoa Meli zake kurudisha Watumwa wote nyumbani Afrika,na tulishuhudia wakiletwa hadi Siera Leone,Liberia katika Majiji yalitopewa majina ya Monrovia na Free Town ikimaanisha sasa tupo huru katika miji huru ya Afrika.

-Mapinduzi ya Zanzibar

Tarehe 12 Januari 1964 asubuhi na mapema, mwanachama wa ASP John Okello kutoka Uganda aliongoza wanamapinduzi 600–800 wa kisiwa kikuu cha Unguja kushinda polisi wa nchi na kuteka silaha zao.Halafu walielekea Zanzibar Town walipompindua Sultani Jamshid bin Abdullah na serikali yake.

Mwanamapinduzi John Okello ndiye aliyekuwa field kuongoza Mapinduzi kumng'oa Sultan Jamshid Bin Abdullah ili kuipata Zanzibar huru itakayoungana na Tanganyika kupata Tanzania moja,Field Marshall John Okello akaipindua Zanzibar ya Sultan na kuirudisha kwa Wazanzibari huku John Okello akiwa Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kabla ya kuikabidhi Zanzibar kwa Pan Afrikanist,Mzee Abeid Karume na kukamilisha Uhuru wa Zanzibar.

Pan Africanist,Mzee Abeid Karume alifanikisha majadiliano ya kuunganisha Zanzibar na Tanganyika ili kuunda hatimaye muungano wa Tanzania; vyombo vya habari vilitafsiri muungano huo kuwa juhudi za kuzuia Ukomunisti kugeuza Zanzibar.Mapinduzi yalikomesha miaka 200 ya utawala wa Waarabu Zanzibar, na yanaadhimishwa kila mwaka kama sikukuu ya taifa zima la Tanzania.

Bila shaka Mapinduzi ya Zanzibar ni chimbuko la Muungano wa Tanganyika na Zanzibar,Daima unapoitaja Tanzania basi unataja vyama vya TAA,TANU,ASP,CCM,Hivyo basi kwa Mtanganyika yeyote Jambo la Zanzibar ni Jambo lake,tupo jirani mno na tuna historia ya pamoja,ni ndugu wa damu, Zanzibar ina WaZanzibar wenye asili ya Unyamwezi,Usukuma,Unakonde,Uluguru,Uzaramo,Undengereko,Uarabu na Ushiraz,kama ingewezekana Zanzibar isogezwe na upepo wa bahari na iwe mbali kabisa na Tanganyika basi huenda ingekuwa nafuu,ni Vigumu kwa Tanganyika kuondokana na Zanzibar katika uhalisia uliopo,

Nimalizie kwa kusema Mapinduzi ya Tarehe 12 January 1964 yalikuwa mpango na malengo sahihi ya waasisi wa Muungano,kuwa yaanze Mapinduzi matukufu kumpindua Sultan Jamshid Bin Abdullah halafu uje Muungano wa Tanzania wa Serikali mbili kwa lengo la kwenda kwenye Serikali moja,na kuunganisha vyama vya Afro Shiraz na TANU ulikuwa ni mwanzo wa safari ya kuelekea kwenye kuyafikia malengo ya Serikali moja ya Tanzania kwa maono ya baadae kuja kupata Serikali moja ya Afrika.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Kibunduga,Tawa
Matombo, Morogoro
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.
-Master of Leadership and Management.

Recent Publication;
-Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
Huu uhuni unaitwa umoja wa Afrika huwa mnautoa wapi? Kama hapa nchi moja tu ya Tanzania tunaongozana kwa shuruti kwa wengine kuiba, huku viongozi wakipendelea vijijini walivyotoka kimachomacho, huo umoja wa Afrika utakaa utokee?
 
Fabricated Story! Kuhusu Mapinduzi kama zilivyo story zingine ukweli hautajwi na Mchango wa John Okello hauthaminiki...
 
Hii ndio generation tuliyokua nayo mavyeti kibao ila kichwani hamna kitu,bado utamaduni wa kuzamisha vichwa vyetu kwenye mchangani na kujifanya hatuoni hali halisi ya wananchi on the ground,kinachofanyika now hapa Africa ni Authoritarian pandemic,angalia chaguzi za Tanzania,zimbabwe,Uganda (muda huu wamekata mawasiliano yote ya social networks)halafu msomi mkubwa kama wewe unakuja na mada kama hii,wake up
 
Back
Top Bottom