.........sijui ndo kutofautiana akili au mawazo, ninavyofahamu mimi mtu yeyote anapofikia uamuzi wa kujiua ni kwamba anakua tayari kashaathirika kisaikilojia kwa kiasi kikubwa........hivyo basi hii Ina maana anakuwa out mind anaona hakuna msaada wowotektk maisha yake, amekata tamaa, na hili la kujiua kujiua lina sababu kuu mbili 1.kuzidiwa na matatizo yoyote yale 2.Kurogwa (kwa wanaoamini hili)........
.......Sasa katika hayo utaona kwamba kumbe mtu akipata msaada katika hayo basi atapona katika kifo, kwa hiyo kumbe tunaweza kuokoa vifo vya wanaotaka kujiua kwa kuwazuia kujiua na kuwasaidia ktk shida zao, au kwa kuwakamata na kuwafanyia tiba kama ni maombi au ni uganga(Incase wamerogea).........
...........Sasa kinachonishangaza hapa ni komenti za wadau eti alistahili kufa coz alitaka mwenyewe!!, wengine eti hapo kosa la Jamaa ni korekodi pekee na sio kuruhisu kifo kutokea ktk mazingira aliyopo!!, imenishangaza sana hii!... eti ndio tunajiita great thinkers, kwamba tunaona huyo mama kujiua kwake ilikuwa ni starehe na ameinjoy, eti Jamaa hajakosea....
......nishauri tu kuwa ikitokea umekutana na mtu yupo kwenye hali ya kutaka kujiua tafadhali msaidie kwa namna yeyote, coz kisaikilojia mtu huyo anakuwa sio yeye tena, hata akifa kinakuwa ni kifo cha bahati mbaya kama ajali tu ndo mana watu wanaokolewa, tubadili mindset wakuu...je angekuwa ndugu yako ndo au mama zetu tungeacha wafe kisa wametaka wenyewe?!!!.....