Developing story; Mwanamke aliyekufa kwa kunywa sumu huku akirekodiwa na mumewe

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,789
699,431
Mume wa marehemu
DJ Brown anaandika

Nilipomfumania mke wangu (red handed) mara mbili na rafiki yangu kipenzi hakuwepo yeyote kunisaidia kutatua maswala yetu!

Kila nilipoleta maswala hayo, alikuwa akinitishia kujitoa uhai, nilichotakiwa kufanya nikumpa kila kitu alichotaka mwanamke huyu. hakuwahi kukosa chochote, chaguo lake ilikuwa lazima liheshimiwe!

Je utajisikiaje kumkamata mkeo akiwa kitandani na rafiki yako wa karibu? sijali ninini watu wengine (watasema..) lilikuwa chaguo lake na nitawaeleza watoto wangu muda ukifika! wapumbavu wengi wenu wananihukumu bila kujua niliyopitia ....Nina furaha sasa na amani sijutii chochote.

djbrownskin_fullu kamili

Zaidi soma!

Wananchi wengi hasa nchini Kenya wamebaki midomo wazi baada ya kuona video iliyovuja ikimuonesha jinsi Dj Brownskin akimrekodi mkewe Sharon Mwangi akijitoa uhai hadi kufa mbele za Watoto wake.

Video hiyo ilianza pale ambapo mkewe anaonekana akikoroga mchanganyiko wa dawa zenye sumu kwenye kikombe, huku akimwambia mumewe kuwa anataka kujiua na baada ya hapo alikunywa na kutupa kikombe na kisha kuketi kwenye kochi.

Dakika chache baadae anaanza kutokwa na povu jingi mdomoni na kuwaambia watoto wake kuwa “nakufa wanangu” – lakini muda wote huo Brownskin haonekani kuchukua hatua yoyote ya dharura kujaribu kuokoa maisha ya mkewe, bali anaendelea kumrekodi akijigaragaza kwenye kochi kisha kuanguka sakafuni.

Baada ya kuanguka sakafuni, Brownskin anamuita msichana mmoja - anayedhaniwa kuwa mjakazi - aliyefika kwenye sebule na kumtaka kumpa maziwa.“Kuna maziwa, hebu mpe maziwa, mlazimishie akunywe,” Brownskin anasikika akimwambia msichana yule.

Hata hivyo, mkewe wakati huu anaonekana kulemewa kabisa na sumu na yuko sakafuni anajigaragaza kutokana na makali ya sumu mwilini, hawezi hata kushika kikombe cha maziwa.

Ikumbukwe Marehemu Sharon Mwangi aliaga dunia mwaka uliopita lakini video imevuja Leo Jumapili , Aprili 2, 2023.
IMG-20230404-WA0270.jpgPia soma:
Wakenya waomba polisi kumkamata DJ Brownskin kwa kumrekodi mkewe akijitoa uhai
 
Huo ndio uwanaume sasa. hawa wanawake wa siku hizi (sio wote) wamekuwa watu wakupenda drama sana tena wanazitumia kusawazisha maovu yao. Yan uFanye uchufu wako alafu ujidai unatishia kujiua ata mm nakuacha ufe ili ukaone yaliyoko upande huo.

hivi hao watoto ana uhakika ni wake?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom