Airtel "Imeolewa" na Diamond - lakini Je, huduma zimeboreshwa?

Baadhi ya wabongo wanapenda sana umbeya,wamechukia sababu tu walilokuwa wakilitarajia hawajaliona na Mondi naye akaona fursa akapita nalo hivyo hivyo kutengeneza pesa.
 
Aitel wezi wa bando
Sio wezi tu hiyo 4G yao tu miyeyusho badala ya kujikita katika kuboresha wanaleta kiki, kitu kizuri Tanzania watu watakuja tu na Tanzania hapa watu wao wanatizama bei kwanza kabla ya ubora jikite huko halafu Tangaza. Mimi niliwahi kuwa mteja wa muda mrefu wa Airtel miaka ya nyuma na sababu ilikuwa wengi katika family tuko huko lakini na miaka kama 3 nimetoka huko sababu ya Net yao sio speed.
 
Ndio ulikuwa mtandao wangu wa kwanza kabisa kutumia ila walinichosha sana nikaachana nao, in short huu mtandao ni wa kishua cc watu wa hali ya kawaida tubaki Tigo
 
Baadhi ya wabongo wanapenda sana umbeya,wamechukia sababu tu walilokuwa wakilitarajia hawajaliona na Mondi naye akaona fursa akapita nalo hivyo hivyo kutengeneza pesa.
Lengo la kiki yao limefanikiwa 100% na nahisi uwa wanawatumia watu wa ndani pia kuvujisha taarifa za siri fake kwa watu kama akina soud brown wazitoe wakiamini kweli kumbe fake.
Wamefanikiwa sana kwakweli
 
Network coverage, QoS, bei za vifurushi n.k vyote hivi hupelekea customer experience nzuri au lah...

Kuna watu wanaishi eneo Airtel ipo vibaya sana au vizuri sana likewise kwa mitandao mingine...

Hivyo siku zote ukiona mtandao mmoja unakuzingua, jaribu mwingine sababu huwa hakuna mtandao mbaya au mzuri muda wote...
 
Back
Top Bottom