Heisenberg
JF-Expert Member
- Apr 26, 2017
- 1,683
- 2,906
Kampuni ya mawasiliano ya Airtel Tz imekuja na huduma ya eSIM ambayo imekua ikisubiliwa sana.
Huduma hii itawapa watumiaji nafasi ya kutumia zaidi ya namba moja kwenye simu moja bila kuongeza (Phisical SIM) Nyingine.
Watumiaji wa Iphone wengine hasa kuanzia iphone 11 wana hii huduma kwenye simu zao ila kwa muda mrefu wamekua hawawezi kupata hii huduma ya eSIM
Nchi kama USA ina huduma hii kwa muda mrefu, huku nchi zinazoendelea tukiendelea kusugua benchi.
Sasa Airtel tanzania wametutoa kimasomaso.
Kwa watumiaji hususani wa iphone ili kujua kama simu yako ina hii huduma bonueza *#06# itatokea picha kama hiyo utaona simu ina IMEI namba mbili licha ya kuwa simu ni ya line moja.
Pia lazima Simu yako iwe EID. namba hii hutumika na carrier wako (Airtel) wakati wa kuisajili huduma hii.
Tembelea branch yoyote ya airtel kwa msaada.