Ripoti TCRA: Dar yaongoza kwa idadi kubwa ya Watumiaji wa huduma za Simu Tanzania

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
Katika kipindi cha miaka 5 kumekuwa na ongezeko la Watumiaji 16,327,131 wa Huduma za Simu Nchini kutoka 47,685,232 mwaka 2019, sawa na 88% ya Idadi ya Watu hadi 64,088,651, sawa na 101.5% ya Idadi Watu

Mikoa yenye Idadi kubwa ya Watumiaji wa Huduma za Simu Tanzania Bara ni Dar es Salaam (18.68%), Mwanza (6.72%) na Arusha (6.11%). Yenye idadi ndogo ni Njombe (1.79%), Lindi (1.76%) Rukwa (1.67), na Katavi (1.05%)

Kati ya Aprili hadi Juni 2023, Watumiaji wa Huduma za Simu wamefikia 64,088,651 (Ongezeko la 3.6%) kutoka Milioni 61.9 Machi 2023. #Vodacom imeongoza kwa idadi kubwa ya Watumiaji waliofikia 19,116,166 (30%)

#Airtel imefikisha Watumiaji 17,505,139 (27%), #Tigo 17,484,387 (27%), #Halotel 8,410,029 (13%), #TTCL 1,559,090 (3%), #Smile 13,840 (0%) na imepoteza Watumiaji 1,331. Kwa mujibu wa #TCRA kuna ongezeko la 1.5% kulinganisha na ongezeko la 0.59% Januari - Machi 2023

Hii inamaanisha kuwa #TaarifaBinafsi za Watumiaji zaidi ya Milioni 64.1 ziko kwa Wakusanyaji na Wachakataji. Je, unafahamu Taarifa Binafsi zako zinatumikaje na zinalindwaje?
1689755680236.jpeg
 
Back
Top Bottom