Uncle bright
JF-Expert Member
- Feb 9, 2023
- 1,040
- 4,080
Yani hawa wahitimu wakitaka kuanza biashara unaweza kudhani hata hawakufika chuo, Unakuta mhitimu ana Diploma au Degree ya Business Administraion au Business Management lakini hawezi kufanya haya mambo ya kawaida, inabidi aelekezwe huko kwenye stationery tena wakati fulani anaelekezwa na mtu ambaye wala hajafika level yako ya elimu.
Mhitimu anamaliza chuo hana Tin Namba inayotolewa bure kabisa.
Mhitimu anamaliza chuo hana habari na Brela, na hata akiambiwa inabidi kwanza asajili jina la biashara, hawezi kujisajili mwenyewe, inabidi aende stationery alipe hela asaidiwe.
Mhitimu anamaliza chuo hawezi kujiombea leseni ya biashara hadi ashikwe mkono, wengi hata Mfumo wa Tausi wa kuomba leseni online hawaujui, inabidi waende stationery walipe hela wasaidiwe.
Mhitimu anaenda TRA kichwa kichwa kuomba kusajiliwa biashara bila mkataba wa frem, ni kwamba hakufundishwa inabidi afike huko aambiwe arudi kuufata
Mhitimu anamaliza chuo hajui process za kuipata tax clearance, inabidi aanze kuulizia kwa wengine ama asaidiwe na vishoka.
Mhitimu anamaliza chuo kafunzwa vipimo vya kodi vya 2004
Mwalimu wa chuoni wa ujasiriamali anategemea mshahara ku survive ama ana kaduka ka sidiria kuzugia kwamba ni mjasiriamali.