Afya ya Mfalme wa Oman yaendelea kuimarika

Ami

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
2,743
2,000
Leo Jumanne televisheni ya taifa ya Oman imetangaza kuwa Afya ya Mfalme wa nchi hiyo inaendelea kuimarika na kwamba hatua za matibabu zinaendelea kama kawaida.

Mheshimiwa Qaboos bin Said Albusaidy wiki mbili zilizopita alirudi kutoka kwenye matibabu nchini Ubelgiji alikokaa takriban wiki moja.Alipoondoka kwa ajili ya safari hiyo ya matibabu aliwaaga raia zake lakini aliporudi haikuelezwa zaidi kuhusiana na afya yake.

Kwenye misikiti ya nchi hiyo kumekuwa na hamasa kubwa ya wananchi kumuombea afya nzuri. Dua kama hizo zimefanyika maeneo mbali mbali ya Tanzania ikiwemo Dar es salaam na Zanzibar.

Mfalme Qaboos bin Said mwenye umri wa miaka 79 ni mshirika mkubwa wa nchi za Magharibi tangu pale alipompindua baba yake katika mapinduzi baridi mwaka 1970 kwa msaada wa Uiengereza.

Baada ya mapinduzi hayo ameiongoza nchi hiyo na kupata maendeleo makubwa ya kiuchumi kwa kutumia rasilimali ya mafuta.

Mfalme Qaboos bin Said inajulikana hana mke na wala hana watoto ambao wangeweza kuchukua nafasi yake kama mapishano ya kifalme ya nchi nyengine yanavyokuwa.

Kwa katiba ya nchi hiyo mfalme hamtaji mrithi wake hadharani kabla ya kifo chache na ni jukumu la baraza maalum la mpito kumchagua mtu wanayemuona anafaa kukalia kiti hicho. Lakini kama wakishindwa baada ya siku tatu utafunguliwa usia wa mfalme na kutajwa jina alilolichagua na ndiye atakayekuwa mfalme mpya.

Pamoja na uhusiano mkubwa wa kidugu kati ya Oman na Tanzania lakini mfalme huyo pamoja na kukalia kiti cha ufalme kwa muda mrefu sina kumbukumbu kwamba amewahi kutembelea nchi hiyo.

1577883619238.png
 

Victoire

JF-Expert Member
Jul 4, 2008
19,500
2,000
Yupo kwenye terminal cancer ya Colon. Soon ataaga dunia. Ila nampenda sana huyu Sultan. Alifinance ujenzi wa makanisa ya catholics na protestants .Ni Sultan aliyeibadili Oman na kuwa nchi tamu ilivyo leo. Bahati mbaya hana mtoto. Sasa sijui alimchagua nani arithi mikoba yake,maskini.
 

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
12,422
2,000
December 31, 2019

Muscat: The Diwan of Royal Court yesterday issued a statement reading as follows: “His Majesty Sultan Qaboos bin Said is in stable condition, thanks and praise be to the Almighty Allah, and is continuing the programme of prescribed treatment.

His Majesty the Sultan, May the Almighty Allah protect him, expresses his deep thanks and appreciation to the noble people of Oman, all over the beloved homeland, for their heartfelt sentiments, sincere wishes and for rallying of support around their leadership.

His Majesty the Sultan prays to the Almighty Allah to protect Oman and its loyal people and to grant them further progress and prosperity so that the triumphant march of development and growth will attain its planned goals, God willing.”
Source: His Majesty the Sultan is in stable condition
 

Ami

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
2,743
2,000
Si asilimia kubwa ni kweli kuna kabila Oman linaongea Kiswahili na wengi chimbuko lao ni Unguja na Pemba.
Sio kabila dada!.Ni watu wa makabila yote ya Oman kuna wazungumzaji wa Kiswahili tena safi kuliko cha kwetu.Hata ukifika ndani majabalini na kwenye mitende mtanzania hawi mgeni.Akizungumza kiswahili tu atapata wenyeji chungu nzima.
 

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
51,040
2,000
Sio kabila dada!.Ni watu wa makabila yote ya Oman kuna wazungumzaji wa Kiswahili tena safi kuliko cha kwetu.Hata ukifika ndani majabalini na kwenye mitende mtanzania hawi mgeni.Akizungumza kiswahili tu atapata wenyeji chungu nzima.
Nimeishi na Waoman hawajui Kiswahili lakini walikubali kuwa kuna wanaoongea Kiswahili ila si wengi
 

Mokaze

JF-Expert Member
Aug 3, 2018
9,089
2,000
kuna kabila Oman linaongeaNi kabila gani hilo???, alichosema mwenzako ndiyo sahihi, Waarabu wengi waliopo zanzibar asili yao ni Oman, pia waarabu waliopo Shinyanga, Mwanza, Tabora, Kigoma hususan Ujiji wanayo asili ya Oman, walikulia Tanzania na baada ya oman kugundua utajiri wa Mafuta wengi wao Walirudi huko oman katika Miaka ya 1970 hadi 80s na 90s, hivyo walirudi huko wakiwa wanajua kiswahili tu ila wale baba zao ndiyo waliokuwa wanajua kiswahili na kiarabu. Wapo rafiki zangu (waarabu) ambao wapo huko, wanafika karibu 10 na zaidi, kumbuka walipo hamia huko walienda familia zote, fanya familia moja walikuwa 10- 15, watoto wote walikuwa wanaongea kiswahili tu, ndiyo maana Oman kiswahili kimetamalaki.

Waziri wao wa nishati ni mswahili pure, si alikuja hapa Tz.??!!.
 

KISIWAGA

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
2,807
2,000
Yupo kwenye terminal cancer ya Colon. Soon ataaga dunia. Ila nampenda sana huyu Sultan. Alifinance ujenzi wa makanisa ya catholics na protestants .Ni Sultan aliyeibadili Oman na kuwa nchi tamu ilivyo leo. Bahati mbaya hana mtoto. Sasa sijui alimchagua nani arithi mikoba yake,maskini.
Hana hata mke
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom